Hivi Mungu aliweka nini kwenye ubongo wa mwanamke?

Nikifikiria kuoa nahisi kuchanganyikiwa,ngoja niendelee kula ujana.
Ingekuwa siku moja moja watu wanazungumzia na utamu wa ndoa, stara inayopatikana na heshma ya mwanandoa kwa jamii. Wakubwa na walio kwenye ndoa kuhamasisha watu waache uhuni waingie kwenye maisha mazuri ya ndoa.

Mitandao ya jamii inaongoza kwa kwa kutoa picha ya vijana wasithubutu kuingia kwenye ndoa..kila mtu akipost ni ushuhuda anavyoteseka na mke au mumewe. Mume anachepuka na wanawake mtaani, mke anatembea na wavulana wadogo mpk aibu.

Ukimchunguza sana bata huwezi kumla.
 
Ingekuwa siku moja moja watu wanazungumzia na utamu wa ndoa, stara inayopatikana na heshma ya mwanandoa kwa jamii. Wakubwa na walio kwenye ndoa kuhamasisha watu waache uhuni waingie kwenye maisha mazuri ya ndoa.

Mitandao ya jamii inaongoza kwa kwa kutoa picha ya vijana wasithubutu kuingia kwenye ndoa..kila mtu akipost ni ushuhuda anavyoteseka na mke au mumewe. Mume anachepuka na wanawake mtaani, mke anatembea na wavulana wadogo mpk aibu.

Ukimchunguza sana bata huwezi kumla.
Hujui kuwa habari mbaya ndio husambaa zaidi?
 
Na mtu akija akisifia ndoa yake humu mbona atajuta. Kwanza ataulizwa ndoa yake ina miaka mingapi, subiri mkeo/mumeo aanze kuchepuka khaaaa. Tunapenda story mbaya mweee
Sasa mtu ana furaha na amani na ndoa yake why ahangaike? Mara nyingi watu huelezea yale yanayowasibu.
Sidhani km ukiwa na furaha utahitaji ushauri!!

Na si kwamba kwakuwa yanakuja mabaya tu basi hakuna jema hata moja huko kwenye ndoa. Ndio ile hata umtendee mtu mema elfu, siku ukifanya baya moja tu,hilo ndilo litaloonekana na kufuta mema yooote!
 
Sasa mtu ana furaha na amani na ndoa yake why ahangaike? Mara nyingi watu huelezea yale yanayowasibu.
Sidhani km ukiwa na furaha utahitaji ushauri!!

Na si kwamba kwakuwa yanakuja mabaya tu basi hakuna jema hata moja huko kwenye ndoa. Ndio ile hata umtendee mtu mema elfu, siku ukifanya baya moja tu,hilo ndilo litaloonekana na kufuta mema yooote!
Ubinadamu kazi
 
Mm mwenyewe nilishakutana na mambo kama hyo lakini haina jinsi ni mke wngu namvumilia2....as long as umeondoka nyumbani ukirudi ongea nae kwa utaratibu atakuelewa
 
Mkuu kuwa mwanamke ni shida. Emotions za kike ziko hormone-controlled. Ndo kinachofanya tuwe very moody. Wewe either mpe hiyo pesa au ongea nae kwa upole mueleze hivo vitu. Hapo ukute hujamnunulia nguo siku nyingi sanaaaa halafu shosti wake anamringishia "My hubby this, my hubby that".
Maisha ni kama mtihani ambao kila mmoja ana paper yake tofauti na mwenzake... Ukidesa kwa mwenzako umekwenda na maji. Huyo bidada kama anataka kuishi maisha ya mashost zake ataibomoa nyumba yake kwa mikono yake.
 
mtafutie mchepuko atatia adabu nswaza ningekuwa mwanaume ningemfanyeje dah angesimulia
 
Am just thinking loudly.
siku mbili zilizopita nilisafiri kwa shughuli za kiofisi. Kama mjuavyo mambo ya serikali yetu hii, unajaza imprest, hela ya safari inachelewa kutoka, au unaweza kulipwa hata baada ya wiki au mwezi tangu urudi toka safari. Sasa mimi ndo yakanikuta. Ikabidi nijiongeze tu ili kuokoa ratiba zangu. Na kumbuka ni tarehe za karibia na mishahara. Nikaacha hela ya mahitaji, nikasisitiza kuwa tusifanye manunuzi yasiyo ya lazima kwa sababu tuko kwenye ujenzi na mafundi hivi wanatudai, hivyo mshahara ukitoka tu tuwalipe. Leo ndo nimerudi kutoka safarini na leo ndo mshahara umetoka. Nilikuwa nimechoka sana leo. Asubuhi nilikunywa kikombe cha maziwa na maandazi mawili, nikashinda nayo njia nzima mpaka nimefika home mida ya saa kumi na nusu. Tangu asubuhi nilijihisi siko vizuri kichwa kinaniuma, najisikia kuchoka. Nikiwa nimekaribia home nikampigia wife kuwa nakaribia kufika. Nashukuru nilifika salama. Njiani nikanunua vitu mbalimbali kama matunda na mboga.

Sasa kilichonifanya niwaze sana kuhusu hawa viumbe wanawake, nilipofika nilisalimia walio nje, then nikaingia ndani. Nikamkuta yuko chumbani amelala. Baada ya salamu, nikarudi nje binti wa kazi alikuwa anaosha vyombo. Nikakaa sebuleni kama dakika 10 nikaona hakuna anayekuja siyo yeye wala msichana. Nikachukua glasi nikanywa maji, nikarudi kukaa kwenye sofa. Nikaona watu wako bize na ratiba zao, Nikatoka nje binti bado anaosha vyombo. Nikarudi ndani chumbani. Nilipoingia nilikutana na swali, "mshahara wako umetoka?"Nikajibu ndiyo. Akasema "hata mimi wa kwangu umetoka, sasa naomba niongezee laki mbili niende mjini sasa hivi kuna nguo nataka nikanunue".

Niliwaza tuu haraka hata sijapewa maji ya kunywa, wala sijaoga niko na jasho la safari, hata sijapumzika, kichwa kinaniuma, njaa inaniuma (maana huwa sipendi sana kula hovyo hovyo njiani), hata hajaniuliza safari ilikuwaje; Nilijisikia kizunguzungu flani cha ghafla, nikatoka nikafunga mlango, nikaondoka zangu nikawasha gari kwenda mjini kutafuta sehemu ya kupumzika walau nipate hata uji au supu nipashe tumbo.

Mpaka sasa sijarudi nyumbani, nasubiria muda uende nikifika naoga nalala tuu. Inaniuma sana, hivi vitendo siyo mara ya kwanza. Mpaka sasa ana masanduku matatu makubwa yote yamejaa nguo zake bado anaona hana nguo, eee Mungu uwarehemu hawa viumbe. Mimi nawaza tumalizie ujenzi tuachane na nyumba ya kupanga, yeye wala haoni kama kuna shida. Alafu sisi wanaume tukichepuka tunalaumiwa sana na hawa wanawake kuwa tunatelekeza familia. Anyway, nafikiria kitakachotokea nikirudi nyumbani
hebu nenda hom ukasikilizie kwanza kama bado salam hakuna bora urudi ulikotokea maana utaua
 
Pole sana kwa mke wako kutokukujali. Hayo matatizo anayo Mke wako na si wanawake wote. Kwa kudhihilisha hilo unawaza kutafuta mchepuko ambaye ni mwanamke, kama wanawake wote wako kama mkeo , utachepuka na mwanaume mwenzio?
Acha lawama za jumla mlaumu mkeo sio wanawake wote.
 
Mkeo alivyo ndivyo ulivyomzoesha, hapakuwa na sababu ya wewe kuondoka kabla ya kumpa ya moyoni. Lakini na wewe baada ya kuona hivyo eti ukaondoka ni lini mtakaa muelezane mapungufu yenu? Yeye anaona poa sababu na wewe umeona poa
 
Back
Top Bottom