Hivi mtu aliyefanikiwa kimaisha ni lazima awe na vifuatavyo?

Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?

Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.
Limekuwa suala kuu la udadisi kwa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.
labda ningeelewa maana ya maisha kwanza ndio tuendelee
 
sanduku la posta dizaini imekuwa outdated

hivi kuna watu bado wanaenda cafe kweli, dah modem mbona za kumwaga unaweka bando ya mwezi jamani dah.
Maisha yanabadilika kwa kasi sana na sasa hivi hivyo ulivyotaja kweli vinaonekana ni mshangao ila mimi sishangai kwani hata huu uzi ulikuwa posted April 2010....Miaka 5 mizuri ishapita kwa kipindi ile ilikuwa ipo kweye chart
 
Unaweza ukawa na nyumba lakini inavuja,
Unaweza ukawa na account ya bank salio halisomi kabisaaa,
Unaweza ukawa na cmu ukawa unaishia kubip,
Unaweza ukawa na mke/mme ukaishia kumegwa/kumega nje,
Unaweza ukawa na laptop nyumba unayo ishi haina umeme,
Unaweza ukawa na sanduku la posta usipate barua hata moja kwa mwaka mzima,
Unaweza ukawa na e-mail lakini huna pesa ya kwendea c@fe

Umeona eeenh!,maisha bhana ni km msitu mnene.
 
Kufanikiwa katika maisha as I see it is to HAVE PEACE OF MIND - DAILY.......... which is very hard to attain any way. Hayo mengine ni matokeo tu na siwezi kuyaita mafanikio maishani.
 
Ukishapata kile unacho wish au ulitaka kupata hapo kabla basi umefanikiwa
 
Mimi Nina zaidi ya hayo.
Nina mashine ya telex, Nina typewriter, nina accordion Nina friji ya mafuta ya taa, pasi ya mafuta ya taa na pia natumia mafuta ya AYu na Yolanda, perfume ya cobra, na nguo zangu zinetengenezwa kwa material ya kimplini
 
Mimi Nina zaidi ya hayo.
Nina mashine ya telex, Nina typewriter, nina accordion Nina friji ya mafuta ya taa, pasi ya mafuta ya taa na pia natumia mafuta ya AYu na Yolanda, perfume ya cobra, na nguo zangu zinetengenezwa kwa material ya kimplini

Kama moyo wako umeridhika basi wewe uko juu sana.
 
Rafiki yangu mmoja amedikoza kuwa iliwahi kujadiliwa katika JF kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha ni lazima awe na vitu hivi.

Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail

Kwamba kama unakosa kimojawapo hujafanikiwa kimaisha.

Je mnakubalina na hoja hizo.


Inategemea na kipimo cha kufanikiwa kwenye jamii unayotoka.
 
Mimi Nina zaidi ya hayo.
Nina mashine ya telex, Nina typewriter, nina accordion Nina friji ya mafuta ya taa, pasi ya mafuta ya taa na pia natumia mafuta ya AYu na Yolanda, perfume ya cobra, na nguo zangu zinetengenezwa kwa material ya kimplini

Mie navaa suruali za pekos, viatu vya rison, nina radio player changer, nisikiliza santuri za lipualipua, sosoliso, orch kiam pia nina mashati ya slim fit ya kimplini, nina saa ya moltima!
 
Kua na pesa,nyumba nzr,uwezo wa kupeleka watoto shule,chakula na mavazi na zaidi ya yote tafuta amani na watu wote,ishi maisha ya kumpendeza MUNGU,hakikisha unaepuka uadui ili kupata amani ya moyoni,tumia ulichojaliwa na muumba kuwasaidia wasichokua nacho,usitende dhambi kwa kusukumwa na utajili ulionao.ukiweza hayo elewa upo ndani ya mafanikio makubwa sana!
 
Back
Top Bottom