Hivi mtu aliyefanikiwa kimaisha ni lazima awe na vifuatavyo?

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Rafiki yangu mmoja amedikoza kuwa iliwahi kujadiliwa katika JF kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha ni lazima awe na vitu hivi.

Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail

Kwamba kama unakosa kimojawapo hujafanikiwa kimaisha.

Je mnakubalina na hoja hizo.
 
labda ningeelewa maana ya maisha kwanza ndio tuendelee
 
Rafiki yangu mmoja amedikoza kuwa iliwahi kujadiliwa katika JF kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha ni lazima awe na vitu hivi.

Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail

Kwamba kama unakosa kimojawapo hujafanikiwa kimaisha.

Je mnakubalina na hoja hizo.
Alhamdulillah kumbe Junius nimefanikiwa kimaisha...!!!
 
Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail .

Unaweza ukawa na nyumba lakini inavuja,
Unaweza ukawa na account ya bank salio halisomi kabisaaa,
Unaweza ukawa na cmu ukawa unaishia kubip,
Unaweza ukawa na mke/mme ukaishia kumegwa/kumega nje,
Unaweza ukawa na laptop nyumba unayo ishi haina umeme,
Unaweza ukawa na sanduku la posta usipate barua hata moja kwa mwaka mzima,
Unaweza ukawa na e-mail lakini huna pesa ya kwendea c@fe
 
dah, kumbe bado kabisaaaaaaaaaa

@preta wea r u?
 
Rafiki yangu mmoja amedikoza kuwa iliwahi kujadiliwa katika JF kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha ni lazima awe na vitu hivi.

Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail

Kwamba kama unakosa kimojawapo hujafanikiwa kimaisha.

Je mnakubalina na hoja hizo.
Uza kila ulichonacho ukawape maskini,kisha unifuate!!
 
siasa hizo................................toa maoni yako na wewe kwanza...
 
Actually ni kweli kuwa vitu hivyo ni muhimu kuwa navyo ingawa kufanikiwa unaweza ukakupima kwa njia nyingi inategemea na status.
For instance katika ukoo wetu ili tukuone umefanikiwa mbali na vyote hivyo juu lakini pia ni lazma angalau umiliki kakiwanda na uwe na angalau na ka'PHD.
Kama mimi ilinichukua muda mrefu kidogo kuvitimiza.
 
Mimi naamini,ukipata shibe nzuri ya uhakika kwa viwango vyako,ukalala nyumbani kwako mahali salama kwa viwango vyako,ukawa na amani moyoni na majirani zako,walau kicheko kinapatikana,pr yako iko vizuri,na kama una vitegemezi na vyenyewe viko salama kwa viwango vyako na vinapata mahitaji muhimu kwa uhakika,mimi naamini ni mafanikio.

Mbona wenye madudu yote ya anasa na wao wanaishia kupata mchele ule ule wa kyela? ambao na mimi ninayeishi kimanzichana bila e-mail wala umeme namudu kupata kama wao? Je mafanikio ni kutimiza malengo yako? je kama ulipanga kuiba na ukafanikiwa kuiba nayo tuite mafanikio?

Kwa ufupi,mafanikio ni kitu complex sana,hakuna straight defn.
 
Rafiki yangu mmoja amedikoza kuwa iliwahi kujadiliwa katika JF kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha ni lazima awe na vitu hivi.

Nyumba,Usafiri,Account ya bank,simu ya mkononi,mke/mme,laptop,sanduku la posta na e mail

Kwamba kama unakosa kimojawapo hujafanikiwa kimaisha.

Je mnakubalina na hoja hizo.

Haya uliyoyataja hayatoshi kukuletea mafanikio (furaha ya kweli) katika maisha hata kama baadhi ya hayo uliyoyataja ni ya lazima katika maisha. Ila ujue mafanikio ya kweli katika maisha ni mahusiano mema unayoyajenga kati yako na wanadamu wenzako , na kati yako na Mwenyezi Mungu. Haya mahusiano ndiyo yatakuleta furaha ya kweli, ambayo nadhani ndiyo mafanikio yenyewe ya maisha. Yote tunayoyafanya yanalenga kutuletea furaha ya kweli. Nje ya hii furaha mwanaume/mwanamke huwezi kusema umefanikiwa.
 
mimi ili uwe umefanikiwa kipimo changu ni umesomesha watoto wangapi yani si wakwako tu no wa wasiojiweza,jamii inayokuzunguka inanufaidikaje na utajiri wako,umefanyika baraka kwa watu wangapi maishani mwako, wangapi watasema namshukuru mungu kwa ajili yako,umesaidia wajane wangapi,umewavika nguo wangapi nk yani list ni kubwa ila kifupi pimamafanikio/utajiri wako na jinsi ulivyoweza kuisaidia jamii inayokuzunguka
 
Unaweza ukawa na nyumba lakini inavuja,
Unaweza ukawa na account ya bank salio halisomi kabisaaa,
Unaweza ukawa na cmu ukawa unaishia kubip,
Unaweza ukawa na mke/mme ukaishia kumegwa/kumega nje,
Unaweza ukawa na laptop nyumba unayo ishi haina umeme,
Unaweza ukawa na sanduku la posta usipate barua hata moja kwa mwaka mzima,
Unaweza ukawa na e-mail lakini huna pesa ya kwendea c@fe

sanduku la posta dizaini imekuwa outdated

hivi kuna watu bado wanaenda cafe kweli, dah modem mbona za kumwaga unaweka bando ya mwezi jamani dah.
 
Back
Top Bottom