Hivi Mnajua Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba Kuifundisha Taifa Stars - TFF Wakamkataa!!!

chibingo

Member
Feb 7, 2009
46
8
Katika kumtafuta mrithi wa Marcio Maximo Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba kuifundisha Taifa Stars lakini TFF wakasema hakidhi vigezo (hana qualification), ikabidi wamuajiri Poulsen. Tujiulize, je huyu Poulsen katufikisha wapi na huyu Herve Renard "the chosen one" au Mourinho wa Africa amewafikisha wapi Chipolopolo? Nawasilisha.
 
Tatizo laTanzania sio kocha bali mfumo tulio nao sio wakutengeneza teaminayoweza kuleta ushindani kokote mfumo wetu unaruhusu wahuni kuingia katika team kubwa na hatimae taifa sasa leo Bongo hata akija Mourinho bado tutakuwa kichwa cha mwendawazimu
 
U-ccm ndio umetumaliza kila idara hapa nchini. utakuta hata kocha anachukuliwa toka nchi wahisani kwani ata kama hajui lolte ili wahisani hao warudishe pesa kupitia mlango wanyuma.atalipwa pesa nyingi mwisho wa siku ataondoka kama alivyokuja na pesa kibao
 
Tatizo ni Tenga na wenzie kuendesha soka kisiasa na si kisayansi TFF ni hopeless na ni afadhali arudi Maximo kwa kipimo kizuri ni challenge iliyopita tumeona tukiingia kwa kubebwa ati ni "best loser" kumbe ni worst losers tukaaibika kinoma. Wako vijana makini lakini kuwapanga namna ya kuwatumia tumeshindwa ila naye Poulsen hana kitu mtupuuuuuu!
 
2mekataa dhahabu,almas na tanzanite 2mekubal mawe ya bara2ni na kokoto za jangwani!Fool n rubbish country, TANZANIAAAAA................!
 
Hata aje Zagallo,TANZANIA HAMNA KITU.

Mwalimu ata awe mzuri vipi kama wewe hujibidiishi au ni mbumbu au uimewekwa pale kwa upendeleo hakuan matokeo chanya hata cku mpja yataonekana.
 
labda kwenye jina Tanzania kuna uchawi furani umetuloga watanganyika lol, si kila kitu hatuwezi aaarg
 
inawezekana tff walichemka kwenye dau, so ikabidi watuletee huyu babu ili mradi tu mzungu.......moja kati ya sifa ya kuchaguliwa ilikuwa ni mshahara atakaohitaji, mzee poulsen ndio aligizi vigezo vyote mpaka vya uzungu:A S-coffee:
 
Katika kumtafuta mrithi wa Marcio Maximo Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba kuifundisha Taifa Stars lakini TFF wakasema hakidhi vigezo (hana qualification), ikabidi wamuajiri Poulsen. Tujiulize, je huyu Poulsen katufikisha wapi na huyu Herve Renard "the chosen one" au Mourinho wa Africa amewafikisha wapi Chipolopolo? Nawasilisha.

Hapo umemchukulia Herve Renard kama ndio siri pekee ya mafanikio ya Zambia, kwamba angepewa kikosi chochote hata kama dhaifu kama hiki chetu basi angeweza tu kushinda CAN 2012! Si kweli bana...uwepo wa wachezaji wenye kiwango kikubwa ni moja ya sababu ilizoifanya Zambia ishinde, hatuna sisi wachezaje kama wale wa Zambia. Labda Paulsen angekuwa na mafanikio zaidi ya Renard kama angepata kikosi kama cha Zambia...nobody knows!
 
tanzania hata aje Mourinho hamna kitu
wachezaji kama Boban...bangi tupu
mazoezi mpaka wajisikie
 
Katika kumtafuta mrithi wa Marcio Maximo Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba kuifundisha Taifa Stars lakini TFF wakasema hakidhi vigezo (hana qualification), ikabidi wamuajiri Poulsen. Tujiulize, je huyu Poulsen katufikisha wapi na huyu Herve Renard "the chosen one" au Mourinho wa Africa amewafikisha wapi Chipolopolo? Nawasilisha.

Tatizo la Tanzania sio kocha bali ni tatizo la
1. kuchagua wachezaji ambao wengi ni wazee
2. Kukosekana kwa nia ya dhati kwa TFF kuinua mpira Tanzania. Mfano, vijana wale wa copa coca cola, kama wangechukuliwa na kuwekwa kambini, leo tungekuwa na timu bora ya Taifa.
3. TFF kuwa na mawazo kama CCM. Na hili watanzania wanachangia kwa kiasi kikubwa. Kubali uongozi wa kisiasa kunasababisha mambo mengine kufanikiwa,. Zambia wamebadilika kimawazo, wamechagua viongozi wa upinzani, sasa mambo mengine yanajileta bila hata wao kutumia nguvu kubwa.
 
Halafu kitu kingine, wazambia walishashiriki mashindano hayo mda mrefu, sasa kusema leo wameshinda kwa sababu ya kocha ni uongo. Halafu kama Taifa, tumeshindwa kurusha mashindano ya CAF, hii tu ni ishara kuwa Tanzania mpira sio kipaumbele, na hatuhitaji kufika huko walikofika Zambia
 
Tatizo la wachezaji wetu ni walewa sifa.Ulevi,bangi na mademu. Nidhamu hamna.Watafanikiwa saa ngapi?
 
Back
Top Bottom