Hivi mmegundua kuwa joto limezidi sana hapa tanzania?

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Naamini kuna wana JF ambao ni wataalamu wa Hali ya Hewa Jamani.Juzi nilikuwa Shinyanga yaani Joto ni Kali kuliko Maelezo na Sasa Nipo Mtwara natamani Kuhamia Baharini.
Nini Kinaendelea na Je Nchi nyingine na Mikoa Mingine hali ni hivyohivyo?
 
Hata hapa Dar joto ni la kufa mtu. It's too damn hot. WTF!!??!!??
 
Nafikiri hili ni suala la kubadilika kwa hali ya hewa dunia,ambalo limesababishwa na uhalibifu wa mazingira!
Usisahau kumpigia kura Dr SLAA,tarehe 31 Oct 2010!
 
naamini kuna wana jf ambao ni wataalamu wa hali ya hewa jamani.juzi nilikuwa shinyanga yaani joto ni kali kuliko maelezo na sasa nipo mtwara natamani kuhamia baharini.
Nini kinaendelea na je nchi nyingine na mikoa mingine hali ni hivyohivyo?

mabadiliko ya tabia nchi.

Usisahau kuchampigia kura Rais mwenye uzoefu kwenye medani ya siasa. 31 october 2010
 
Ndugu yangu wala usiseme hali si shwari huku tuliko, jua la saa tatu ni kama la sa6 mchana linachoma mbyaaaaa na joto ndo usiseme.Hya ndio yalee mabadiliko ya tabia nchi, tumuombe Mungu atushushie mvua angalau maana hali ni mbya kwa joto.
 
mabadiliko ya tabia nchi.

Usisahau kuchampigia kura Rais mwenye uzoefu kwenye medani ya siasa. 31 october 2010

Wabongo Bwana mi naulizia Kuhusu Joto wao wanapiga Kampeni Ooh Rais mwenye Uzoefu!!! Uzoefu Huo ndo umetufanya Tuendelee Kuwa Maskini.Tunahitaji Mabadiliko
 
wakuu jana nimeshinda home tumbo wazi.joto utafikiri jua limeshuka kidogo!ila watoto walikuwa hawaamini kwamba baba yao nina kitambi!kila tukipishana nao ni vicheko,si unajua hawakuwahi kukiona!hadi h/g alikuwa akiniangalia kwa tabasamu!
 
Hata arusha nashangaa wanasema eti joto kali, jamani wenzetu huku wanachukua hatua kali juu ya hizi dalili ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya nishati ya umeme lakini bado tunazunguka zunguka wakati vitu vinaonekana.
 
Naamini kuna wana JF ambao ni wataalamu wa Hali ya Hewa Jamani.Juzi nilikuwa Shinyanga yaani Joto ni Kali kuliko Maelezo na Sasa Nipo Mtwara natamani Kuhamia Baharini.
Nini Kinaendelea na Je Nchi nyingine na Mikoa Mingine hali ni hivyohivyo?

Du heri yenu sisi huku sasa tunacheza na -5 degrees sijui ikifika january inakuwaje!
 
Nadhani kuzidi kwa joto siku chache zilizopita nchini Tanzania kumesababishwa na jua kubadili mwelekeo kutoka kaskazini mwa Equator na kuteremka chini. Hivi sasa jua linapita maeneo ya mipakani kusini mwa Tanzania na nchi jirani za kusini. Baada ya siku 2 au 3 jua litakuwa limeshahama usawa na Tanzania na baadae baada wiki 2 hivi hali itakuwa na uafadhali sio kama ilivyo sasa.
 
wakuu jana nimeshinda home tumbo wazi.joto utafikiri jua limeshuka kidogo!ila watoto walikuwa hawaamini kwamba baba yao nina kitambi!kila tukipishana nao ni vicheko,si unajua hawakuwahi kukiona!hadi h/g alikuwa akiniangalia kwa tabasamu!

Hatari hapo Mkuu Zamaulid
 
Nadhani kuzidi kwa joto siku chache zilizopita nchini Tanzania kumesababishwa na jua kubadili mwelekeo kutoka kaskazini mwa Equator na kuteremka chini. Hivi sasa jua linapita maeneo ya mipakani kusini mwa Tanzania na nchi jirani za kusini. Baada ya siku 2 au 3 jua litakuwa limeshahama usawa na Tanzania na baadae baada wiki 2 hivi hali itakuwa na uafadhali sio kama ilivyo sasa.

sipati picha waliopo Sudan pakoje.....ki ukweli jua ni kali sana na huku Yaeda kulivyo dry ukituona utadhani vima tulivyopauka....tunahitaji sala kwa wingi ili mvua inyesha
 
@Preta.. Huko Sudan sasa ndio wanapumuwa kidogo baada kuwa na joto kali kwa kipindi cha takribani miezi mitano iliyopita. Njia ya muelekeo wa jua imebadilika na kwa sasa halipitii juu ya anga ya Sudan hadi mwakani tena jua litakapopanda juu ya usawa wa equator hadi kaskazini mwa Sudan na Misri. Katika kipindi cha kisiozidi siku 60 baadhi ya maeneo ya Sudan kaskazini kutakuwa na baridi kali.
 
Naamini kuna wana JF ambao ni wataalamu wa Hali ya Hewa Jamani.Juzi nilikuwa Shinyanga yaani Joto ni Kali kuliko Maelezo na Sasa Nipo Mtwara natamani Kuhamia Baharini.
Nini Kinaendelea na Je Nchi nyingine na Mikoa Mingine hali ni hivyohivyo?

ni kweli lakini naona joto la uchaguzi limezidi zaidi nchi nzima na hasa baada ya kubakia siku chache, huku yule jamaa shekhe yahya akisisitiza kuwa hamna uchaguzi mwaka huu
 
@Preta.. Huko Sudan sasa ndio wanapumuwa kidogo baada kuwa na joto kali kwa kipindi cha takribani miezi mitano iliyopita. Njia ya muelekeo wa jua imebadilika na kwa sasa halipitii juu ya anga ya Sudan hadi mwakani tena jua litakapopanda juu ya usawa wa equator hadi kaskazini mwa Sudan na Misri. Katika kipindi cha kisiozidi siku 60 baadhi ya maeneo ya Sudan kaskazini kutakuwa na baridi kali.
mmh uko dip kaka ndo fild yako nin?
ivi kumbe jua nalo linatembeaga ennh?
mi nilijua likitoka mashariki na kuzama magharibi ndo basi kumbe linamove eennh?thax for the class kp t up
 
Ni wapi Huko Matarese Ili angalau nije Kwa Wiki Moja...Joto Limezidi Bongo.Natamani kuloweka Godoro katika Maji.Na usiombe Umeme ukatike na Feni Isimame...Nyumba Jehanamu
 
Back
Top Bottom