hivi mliangalia ule mdahalo wa jana tbc-tabora mjini?

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,025
sijajua kwanini chadema haikushiriki ule mdahalo, au ndio tuseme hawana mgombea aliyesimama kwenye lile jimbo?(ingawa walisema kuna wagombea 3 hawakushiriki-kwani walikuwa 7).kuna mzee mmoja nadhani ni wa UPDP, dah huyu mzee alikuwa ananifurahisha sana kwa comments zake..mfano alikuwa akisema "huyu shabani kissu namshangaa sana, yeye anatoa dakika 3 kuelezea sera zilizojaa kwenye kitabu''..huku akionyesha mikaratasi ya sera mkononi mwake...akasisitiza kwamba hamna cha sera wala nini,sera za vyama zote ni nzuri''.....huyu mzee comments zake ni outstanding mno.....la mwisho lililoniacha kinywa wazi, wagombea wote 7 walikuwa waislamu, na wote walikuwa wanamnadii mgombea wa urais wa CUF-PROF IBRAHIM LIPUMBA...kwenye mdahalo ule sikusikia jina la KIKWETE(iwe kwa jema au kwa uongozi mbaya)...walau yule mzee alimtaja DK SLAA kuwa ni mpambanaji....:director:
 
hata mie nilisikia na nilibaki kinywa wazi almost muda wote wa mdahalo. bongo kuna mambo!
 
Niliufuatilia ule mdahalo,Chadema wamesimamisha mgombea ubunge anaitwa, kwikima nafikiri kutokana na matatizo ya kibinadamu, hakuweza kuudhuria mdahalo huo.Tabora ni mkoa wenye waislamu wengi,hivyo kuwa na wagombea wengi au wote waislamu si jambo la kushangaza, kwani wakristu ni wachache sana.Lakini imewahi kuwa na wabunge wengi wakristu.Wabunge wa zamani ambao ni wakristu ni Kisanji,Misigalo,mama Busongo na prof Mgombelo wengine kama Abubakar mgumia(deceased),[Chief Fundikira(deceased)]Kaboyonga hawa ni waislamu.Usishangae kuona listi ya wabunge wa zamani wa Tabora mjini ni wengi sana hii inatokana na historia ya Tabora mjini katika miaka ya hivi karibuni ambapo Mbunge hawezi kukaa zaidi ya kipindi kimoja,kwa mfano (Misigalo 1990-1995),(Mama busongo1995-2000),(Prof Mgombelo 2000-2005),(Kaboyonga 2005-2010),(Rage 2010-2015,awezi kuvuka hapo huo ndio utaratibu wa Tabora Mjini)
 
hii midahalo kwakweli ni mizuri japo wahusika hawajajiandaa au tusime hawajui kujielezza kabisa yani kuna wakati utacheka mbavu ziume
 
kwa kweli tangu nianze kuangalia kipindi hiki cha mchakato majimboni, hakuna siku ambayo nilicheka sana kama jana.
Ukweli nim kwamba hiyo ndio demokrasia na haki ya kuchagua na kuchaguliwa inavyotumiwa na watanzania. wenye haki ya kupigiwa kura wamejitokeza sasa ni zamu ya wenye haki ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi tarehe 31 October.
 
Hasa yule aliyesema kwamba atatumia shilling milioni 10 kati ya millioni 11 atakazokuwa anapata kwenye maendeleo ya jimbo lake aliniacha hoi
 
Niliwasikia wawili kwa mbali wakidai kuwa, iwapo watachaguliwa kuwa wabunge, hao wenzao waliokuwa nao kwenye mdahalo (kutoka vyama vingine) hawatawaacha nyuma, watakuwa kwenye jopo lao la washauri!
 
AH!!! mimi mpaka nikabadili channel, maana iliboa sana! at least wa cuf afadhali
 
Vilaza akina nani sasa ebu acheni masihara watu madr alafu unasema vilaza?
 
sijajua kwanini chadema haikushiriki ule mdahalo, au ndio tuseme hawana mgombea aliyesimama kwenye lile jimbo?(ingawa walisema kuna wagombea 3 hawakushiriki-kwani walikuwa 7).kuna mzee mmoja nadhani ni wa UPDP, dah huyu mzee alikuwa ananifurahisha sana kwa comments zake..mfano alikuwa akisema "huyu shabani kissu namshangaa sana, yeye anatoa dakika 3 kuelezea sera zilizojaa kwenye kitabu''..huku akionyesha mikaratasi ya sera mkononi mwake...akasisitiza kwamba hamna cha sera wala nini,sera za vyama zote ni nzuri''.....huyu mzee comments zake ni outstanding mno.....la mwisho lililoniacha kinywa wazi, wagombea wote 7 walikuwa waislamu, na wote walikuwa wanamnadii mgombea wa urais wa CUF-PROF IBRAHIM LIPUMBA...kwenye mdahalo ule sikusikia jina la KIKWETE(iwe kwa jema au kwa uongozi mbaya)...walau yule mzee alimtaja DK SLAA kuwa ni mpambanaji....:director:

Hivi na CCM hawakuweka mgombea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom