Hivi mkutano huu umetugharimu kiasi gani?

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Nimesoma magazeti ya leo asubuhi SPIKA 6 anatoa statements za kudai kuwa hatuna gharama tuliyoingia kwenye mkutano huu

Jambo hili sitaki kuliamini kwa sababu SPIKA 6 si mwadilifu yapotokea madili kama haya na hasa anapokwepo huyo bwana KASHILILAH
IMG_2075.jpg


Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola na Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Mh. Samwel Sitta (kulia) akipozi na Spika wa Bunge la India Mh. Meira Kumar (kati) na Balozi wa India nchini wakati wa hafla aliyowaandalia wabunge 800 toka mataifa 53 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika hoteli ya Kibo Palace usiku wa kuamkia leo ikiwa ni sherehe ya kuwakaribisha wah. hao wanaohudhuria mkutano wa 55 wa chama hicho. mwakani mkutano huo unatarajiwa kufanyika Kenya

IMG_1554.jpg


Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Dk William Shija (shoto mbele) akipozi na kamati ya wabunge wanawake wa chama katika hoteli ya Arusha Corridor

IMG_2122.jpg

Wah. wakiserebuka katika hafla ya kuwakaribisha iliyoandaliwa hoteli ya Kibo Palace usiku kuamkia leo

IMG_1921.jpg

kikundi cha ngoma toka Endulen kikitumbuiza wageni

IMG_1626.jpg

wafanyakazi wa ofisi za bunge wakiandaa vocha za msosi kwa wageni

IMG_1574.jpg

baadhi ya wafanyakazi wanaofanikisha mkutano huo

IMG_1942.jpg

MC Angela Bondo (shoto) akipata maelekezo toka kwa maafisa wa bunge wakati wa hafla ya usiku kuamkia leo hoteli ya Kibo Palace

IMG_1902.jpg

wanafunzi wa shule ya St. Jude wakifanya rihezo chini ya usimamizi wa Mh. Samwel Sitta na wabunge wa Tanzania wa CPA

IMG_1807.jpg

katibu wa bunge Dr. Thomas Kashillilah akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa ofisi za Chama cha Mabunge ya Jumiya ya madola

IMG_1685.jpg


IMG_2443.jpg

Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola Samwel Sitta

SANY4378.jpg

Hoteli ya Arusha Corridor kunakofanyika baadhi ya vikao vya CPA

IMG_2537.jpg


IMG_2500.jpg

Kamati ya utendaji ya CPA katika picha ya pamoja (juu) na wakati wa kikao chao (chini)

blog.jpg


Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola Samwel Sitta akiwapokea wajumbe toka Bermuda

IMG_2393.jpg

Wah. Wabunge wa Tanzania wanaotuwakilisha CPA katika ufunguzi wa mkutano

IMG_2400.jpg


Chumba cha mkutano

IMG_2267.jpg


Mh. Hubert Kim E. Swan ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani katika bunge la Bermuda ni kivutio cha aina yake kwa jinsi anavyopiga pamba katika mkutano huu

IMG_2514.jpg

 
Ina maana huu ukumbi walipewa wa BURE? Hata hayo maji ya kunywa WALIPATA BURE? Labda aseme gharama ndogo...

IMG_1902.jpg


Naona Dr. Slaa na yeye alikuwepo na mezani alikuwa na MTAMBO wa maana sana. Sijui na yeye alinunuliwa na Mwakalinga? Ila inafurahisha kuwa Mzee wetu yuko kwenye Mtandao muda wote.......
IMG_2393.jpg
 
Wakuu hii ni danganya toto tu kwa wale werevu tumesha ling'amua hamjui uchaguzi mwakani?
 
Alafu liukumbi lote hilo watu kiduchu viti tupu si bora wange alika watu waje wahudhurie
 
Hivi na nyie mbona kama mnaongea bila kuelewa,mara nyingi host country wa mikutano au events kubwa kama hizi anapata faida ndio maana watu wanashindana kuandaa vitu kama hivi,unachotakiwa ni kuweka security na kuhakikisha facility za kuwaweka wageni kuanzia usafiri,convention center,usafi etc zinakuwa katika standard inayotakiwa...hivi wakija wajumbe,waandishi,watalii etc kwa ajiri ya huo mkutano kama 5000 mnafikiri hizo pesa watakazotumia kuanzia chakula,hotel,shoping,usafiri,vyangudoa zinaenda wapi?hiki ndio kipindi watu wanakuwa mamilionea hapo na serikali nayo inapata kodi yake,hii ni faida kubwa sana na hiyo gharama ni ndogo sana na kwanza inasaidia utalii wetu maana katika hao waliokuja lazima wengine wataingia kwenye mbuga zetu na wanaweza kurudi baadaye tena,hii kitu ia win win kwa watu wa Arusha na Tanzania kwa ujumla!
 
hivi wakija wajumbe,waandishi,watalii etc kwa ajiri ya huo mkutano kama 5000 mnafikiri hizo pesa watakazotumia kuanzia chakula,hotel,shoping,usafiri,vyangudoa zinaenda wapi?hiki ndio kipindi watu wanakuwa mamilionea hapo na serikali nayo inapata kodi yake,

Koba,

Kikawaida inatakiwa kuwa hivyo. Ila kwa Tanzania unaweza kukuta imeandikwa kuwa gharama zote ni sisi tumewalipia na bili zake hizo. Ila kwa wachache sana ukweli utakuwa kwamba jamaa wamejilipia wenyewe na hivyo hiyo pesa yote imeFISADIWA. Unakuwa kama huishi Tanzania?

Hukusikia Mawaziri/Wabunge wanapata POSHO na kwenda sehemu kikazi. Wakifika hapo wanadai wapatiwe mahali pa kulala na kula wakati wamechukua posho zao tayari kutoka kwa Pinda/Sitta. Haya mambo usishangae watu kama GT kuyaleta hapa kwa mshangao maana GT anasema kutokana na UZOEFU kuwa "haamini!!".
 
Gt lazima awe na wasiwasi kuwa hapo jamaa wamekula kwasababu anajua jinsi wafadhili wake wanavyotuibia!! Ingekuwa mkutano huu umeandaliwa na Lowassa, NSSF au Manji wala asingeuliza umeghalimu kiasi gani?
 
nji hii ina makuu sana
Mbaya zaidi wanadhani wanaongoze watoto wa
Kindergarten
 
Wakulu mkutano wote unagharimiwa na sekretariet ya CPA sio hela yetu. Hapa sisi tunamake tuu. Kama ni kutumia fedha vibaya, ni kwenye Sullivan. Wako watu walia, wa kucheka walicheka, wa kuliwa waliliwa na wa kula, walikula. Huu wa CPA ni kula tuu, hakuna hakuna kuliwa wala vilio ni vicheko tuu.
 
Gharama halisi siwezi jua ila nahisi kiwango kikubwa kimechangiwa na wahusika. Au GT analo lingine maana huwa anaingia katika namna ngumu kuitabiri
 
Back
Top Bottom