Hivi Michuzi anaishi Tanzania?

Huyo ni mpiga picha tu. Halafu nawashangaa watu mnaoingia kwenye blogu yake mkitegemea kukuta habari serious humo!
 
Umeombwa uivisit blog yake? staili yake hiyo ndio imemfanya afahamike na afike hapo alipo!
Kama anakukera wewe potezea tu, yeye mwenyewe anajua anachokipata!
 
huyu jamapamoja nakuwa mwana habari wa sikuyingi lakini naona haitendei haki taaluma yake (katika blog yake) kwani kila siku yeye habari zake nyingi ni zaburudani na starehee tu.utazania yupo kwenye nchi ambayo ina utawara bora, mahitaji muhimu ya wananchi yanapatikana.JE! HUYU NI MTANZANIA KWELI?

Na wewe pamoja na kuwa ni Mtanzania wa siku nyingi, unaidhalilisha lugha ya Taifa.
 
Umeombwa uivisit blog yake? staili yake hiyo ndio imemfanya afahamike na afike hapo alipo!
Kama anakukera wewe potezea tu, yeye mwenyewe anajua anachokipata!

Kweli Anachokifanya Hakifurahishi Kabisa!! Sisi Kama Wasomaji wa Glob ya Jamii Tuna Haki ya Kutoa Ushauri wetu wa Namna ya Kuboresha!! Ila Mtu Kama wewe Unaonekana kila kitu chenye Manufaa kwa Mtu Binafsi, Jamii unakuwa Negative!! Sijui Ukoje?? Ila kwa Mawazo na Uzoefu wa Haraka Huyu Bwana alianza Kubadilika Mwanzoni mwa 2010!! Nadhani alilambishwa Asali ambayo sasa Inaua Taalumu Yake Taratibu!! Magamba?? Hawana Hata Huruma na Taaluma za Watu!! Nawasilisha!!
 
huyu jamapamoja nakuwa mwana habari wa sikuyingi lakini naona haitendei haki taaluma yake (katika blog yake) kwani kila siku yeye habari zake nyingi ni zaburudani na starehee tu.utazania yupo kwenye nchi ambayo ina utawara bora, mahitaji muhimu ya wananchi yanapatikana.JE! HUYU NI MTANZANIA KWELI?
Wewe umekurupuka hii nyanja inaelekea hauijui vizuri,katika uandishi kuna magroup matharani waandishi wa habari za uchumi na siasa,michezo na burudani,sayansi na elimu,uchunguzi etc.ila wewe unataka blog yake ifate matakwa yako!yeye anajali wateja wake wanahitaji nini!sasa wewe unalaumu bila kufanya utafiti!
 
Nisaidie labda mimi sielewi, mpiga picha na mwandishi wa habari wana tofauti gani??
CD!!mwandishi niyule anayekusanya habari na kuziweka kwenye chombo chakuwakilisha ktk jamii,radio,tv.gazeti,etc.Na mpiga picha nimwandishi anayeleta ujumbe kwa picha kwakutumia vyombo,tv,gazeti.
 
Tatizo lake ni pale anapoweka picha za Vyama vya kisiasa; Kwa CCM anapamba sana na kuweka nzuri nzuri tu; kwa Upinzania nzuri ni kidogo sana, zaidi ni zile labda wapinzani wanapata kibano na mbaya mbaya tu etc. nadhani hata kama taarifa zinatoka kwa wahusika sitaki kuaamini kwa upande wa upinzani nyingi zinazomfikia ni zile za kasheshe kasheshe tu
 
Kama uko nje ya nchi na unapenda ujiko ujiko (kama akina mashaka) kwa CCM ili siku moja wakukumbuke Michuzi is the blog to go. Binafsi nilishajipiga ban toka mwaka juzi!!
 
Jamani kila siku napakua michuzi blog lakini sijawahi kukutana na taarifa za mapambano ya kuiokoa nchi yetu. Kila siku yeye na wasanii, kama ni habari za siasa utakuta ni chama cha ccm tu. JE YEYE BLOG YAKE HAITAKI MABADILIKO HAYA TUNAYOYAONA JAMII FORUMS INAYAPIGANIA?

Stahili za mapambano zipo nyingi sana, kuna wapambanaji wengi wa kutukuka hapo Tanzania na nje ya nchi, bahati mbaya wamekuwa wakipuuzwa. Jaribu kuangalia mtu kama Rev Mtikila, pamoja na madhaifu yake ya kibinadamu ni mapambano mangapi amepigana na system na kufanikiwa kuleta mabadiliko? Mbona 'Watanzania wa kweli' sijawasikia wakimsifu hapa zaidi ya kumbeza kwa vijembe visivyo mashiko?
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Kweli Mkuu. Pamoja na mambo yake, lakini jamaa amekuwa anapigania vitu vya maana. Kama the right to independent candidate ni hoja muhimu sana lakini naona kaachiwa mwenyewe. Kaipeleka kesi African court of human rights na akishinda utaona jinsi watu wengi watavyojitokeza kama wagombea binafsi. Kweli sometimes anaudhi, lakini kuna mambo ya msingi huwa anayapigania.
 
Michuzi akitoa habari inayohusu CHADEMA ujue kwamba lazima itakuwa negative tu! CHADEMA wakipingwa mabomu, ama wakikamatwa na kupelekwa kizimbani jamaa huwa mstari wa mbele kuzitoa habari, lakini unapokuja kwenye hoja za nguvu zinazotolewa na wanaharakati kuhusu kulikomboa taifa huwa haziweki, yeye kila siku ni Jk ama Nape ama picha za kitchen party na harusi. Watu wengine Bwana! kuna matatizo mengi ndani ya jamii , hayaoni hayo au ndiyo kishaleweshwa na cCm?
 
Michuzi anaishi Tanzania sema akili zake zimo tumboni. Na blog anayoita yake si yake bali chombo cha mafisadi kuhadaa umma. Angekuwa na shule tungesema anakosea. Kwa kihiyo yoyote apatapo ulaji hata kama ni wa kujiuza huwa haangalii mbele. Poor Michuzi na kazi ya kufua nepi za mafisadi.
 
Hiyo blog ya michuzi ni KITENGO MAALUMU CHA PROPAGANDA kwa ajili ya watanzania wala keki waishio huko ughaibuni,na anapata ruzuku kwa ajili hiyo ili kufanya kazi ya ccm nje ya nchi.ndio maana hakosi mialiko ya minuso(a.k.a dhifa za kitaifa)popote pale nchini .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom