Hivi michango ya mawazo ya mafisadi inaonekanaje katika jamii?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Mara nyingi nimeona watuhumiwa wa ufisadi na uozo mwingine katika jamii wakichangia mawazo iwe kwenye mikutano au hata Bungeni.Huwa haingii akilini mwangu.Kilichonifanya niandike thread hii hata hivyo ni kumuona Andrew Chenge akichangia hoja Bungeni katika kikao kinachoendelea hivi sasa.Niseme kweli, nilisikia mwili unasisimka.Akilini mwangu nikawa ninajiuliza,huyu vijisenti leo amejua anatufundisha.Mbona hakujua kwamba kutuibia wananchi ni dhambi,tena sio kwa wanadamu tu, hata mbele za Mungu?Na inakuwaje hawa wengine wanakubali kukaa nao hawa akina Chenge na Mramba nk.?Nikajiuliza hivi wamesahau ule msemo wa kiingereza usemao 'first impression matters",ambao unatumika sana hasa katika udahili. Je,wamesahau kwamba urafiki mbaya unaharibu tabia njema?Je wamesahau kwamba kwa tuhuma zile, jamii haiwaamini tena na yote wanayosema kwao hayana maana na ni upuuzi mtupu?Je hawa hawajui kwamba kuendelea kuwaona hawa ni kama kutonesha vidonda vyetu?Watawala hawa wana maana gani hasa?Hatimaye nikapata jibu.Kwamba wao na akina Mramba na akina Chenge ni kitu kimoja,kwa vile kama wasingekubaliana na waliyoyatenda wasingekubali kuchukuliana nao.Dhambi yao kwa wanachi ni moja!Ninachosema ni kwamba kama watawala wetu wanataka tuwaone kwamba hawana hatia, wawaondoe akina Chenge,Mramba na wengine wa aina hiyo miongoni mwao,vinginevyo they are also guilty!
 
Back
Top Bottom