Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

MGAO UNASABABISHWA NA SIASA ZA SEREKALI YETU KWENYE MAMBO YA MSINGI NDIO MAANA LEO HII TANESCO WAMEFILISIKA KWA SABABU YA MZIGO WANAOBEBESHWA NA SEREKALI KAMA KUNUNUA MAFUTA YA UMEME WA DHARURA MPKA UNA KUTA MATUMIZI NI MAKUBWA KULIKO MAPATO.
LEO HII AGRECO WANA WADAI TANESCO MABILION NA WAMEZIMA MITAMBO SASA HATA HAYO MAFUTA MKIWAPELEKEA SIJUI KAMA WATAKUBALI KUWASHA MITAMBO BILA KULIPWA DENI,SYMBIONI VILE VILE WANA DAI MABILIONI KIBAO,SONGAS NAO WANADAI MABILIONI SIJUI MWAKA HUU ITAKUAJE HUU MGAO UTAKUWA WAKUTISHA NA HAUJAWAHI KUTOKE TANZANIA,MUNGU IBARIKI TANZANIA TULETEE MVUA.KIBAYA ZAIDI MVUA IKINYESHA SEREKALI YETU INALALA NA MIPANGO YOTE INASIMAMA.SIJUI ALICHOTUELEZA BUNGENI MWAKA JAN NGELEJE SI JUI Kama kuna lililotekelezwa hata moja zaidi ya ulaji wa kununua mafuta.
 
Nimesoma magazetini; mgao mkali waja.
Ni miaka minne sasa, kila mwaka kuna mgao wa umeme na kila mwaka Serikali imekuwa ikija na mikakati na ahadi za kuondoa kero hiyo. Mwaka juzi Serikali iliahidi Bungeni hakutakuwa na tatizo hilo tena.
Waziri na Katibu Mkuu Wizara wamebadilishwa, tatizo liko pale pale. Kwa serikali makini, ingejiuzulu. Wakati umefika Wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali ya JK, imeshindwa kutimiza ahadi, imeshindwa kuondoa kero moja tu kwa miaka minne,

Inatosha!

Mkuu ni zaidi ya miaka minne nadhani tangu Mr. Ben .
 
Hivi jamani,hivi hatuwezi ku-outsource rais,mawaziri na makatibu wakuu wa wizara?Hawa watanzania wenzetu wanatulet down daily yaani!
 
Mgao wa umeme mkali umekuwa ukiendelea kinyemela katika maeneo mengi jijini Dar es salaam. Tanesco tunaomba mtu wekee bayana kuwa kuna Mgao wa umeme na kutupa ratiba kamili. Kuna thread ilikuwa humu ikielezea kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco aliyotoa baada mkutano wa Bodi pale Makao Makuu Tanesco,alituhakikishia kwamba tutaona cha moto na Mgao utaendelea. Nilifikiri ilikuwa porojo,sasa kauli yake inadhihirika.

Waziri mwenye dhamana Bw. Muhongo uko wapi? Ulitoa kauli Bungeni kwamba hakutakuwa na Mgao tena Tanzania. Wananchi tunaomba mwongozo tafadhali. Au ndio mafisadi wachache wana nguvu na jeuri kushinda UMMA?
Maana kauli na matendo Yao yanadhihirisha hivyo. Tunakoenda TANZANIA sio pazuri.
Nawakilisha kwa uchungu.
 
Hamjanielewa wakuu. Hoja yangu ni kwamba watuwekee wazi kwamba kuna mgao ili kuweza kuokoa gharama za hapa na pale. Kwa mfano : vyakula na vitu kuharibika kwenye jokofu. Kulizima jokofu ili kuepuka uharibifu au kuungua pindi umeme utakaporudi kwa mbwembwe.
Tatizo letu tumeshazoea kuburuzwa mpaka mambo ya msingi tunachukulia kiwepesi wepesi.
 
Hali hii inashangaza, sisi tulio maeneo ya kinondoni tunapata tabu ya umeme kila siku asubuhi kwa masaa kama 4 hivi. toka jana, ikifika saa 3 kasoro robo wanakata na kurudisha kama saa 6 hivi. hiyo imetokea jana na leo tena imetokea,
Je kuna mgao wa kimyakimya? mbona hawatangazi?
 
Huenda ikawa maana hapa Udsm toka wiki jana umeme sio stable hata kidogo, tumekuwa tukikosa umeme takribani kwa saa moja au mbili hivi kati ya siku mbili au tatu za kila wiki.
 
eh !eh hata huku Arusha mtindo ndo huo huo japo wanakata jioni kwenye saa 1.30 hivi juzi na jana wamekata na sijasikia mgao
 
Nafikiri mgao upo,tena ni mkali sana kupita maelezo. Tanesco wamekuwa WasengeNyaji sana kupita maelezo. Wanatusengenyaaa tu utafikiri umeme wenyewe wanatugawia bure.
 
toka saa 3 ndio umeme unarudi sahizi, yaani saa 12 na robo, his is terrible, afazali wangesema tu...kuwa kuna mgawo.
 
Hali hii inashangaza, sisi tulio maeneo ya kinondoni tunapata tabu ya umeme kila siku asubuhi kwa masaa kama 4 hivi. toka jana, ikifika saa 3 kasoro robo wanakata na kurudisha kama saa 6 hivi. hiyo imetokea jana na leo tena imetokea,
Je kuna mgao wa kimyakimya? mbona hawatangazi?

Huku Gongolamboto mgawo kama kawa. Wakati mwingine twalala gizani. Umeme hukatika hadi masaa kumi na mawili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom