Hivi madaktari bingwa wote ni wachaga?

hi hapo kweli ila upo uhusiano kuwa walaji wa ndizi na samak wana akili sana hasa mtoto anapokuwa mdogo ndizi zina asili ya kuimarisha ubongo uliza wataamu

mkuu umenena siri ya wahaya, wachagga na wanyakusa kuwa mbele kielimu ni shauri ya kula ndizi kwa wingi hilo halina ubishi.
 
Nimepata kuchangia hapa jamvini nikapendekeza kwamba JF wanazungumzia mno Wachagga. Tujikite ktk topics za kuimarisha taifa letu.
Licha ya kwamba ni vizuri kujua mila na tamaduni zetu, ni vizuri kuzungumzia mambo yanayoimarisha umoja wa kitaifa.

Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa (makabila ya pembezoni mwa Tanzania) walipata elimu mapema, na kwa hiyo utakuta mabingwa wengi wa kitaaluma za kisasa wanatokea kwao. Wachagga kutokana na ardhi kwao kuwa finyu, pia wamehamia mijini na wanafanya biashara ktk kona zote za Tanzania.

Ni jambo la kuridhisha kwamba hata ktk biashara kubwa kubwa Tz sasa, wamejitokeza Wachagga pia. Reginald Mengi wa IPP na Mike Shirima wa Precision Air ni baadhi ya mabingwa pia ktk sekta zao. Uongozi wa Kichagga ulikuwa unasisitiza kwamba tusibague watu kwa makabila yao na kwamba ni lazima tuwe ni watu wa kujituma.

Nilifurahia sana kuona ktk TV, ukumbi wa Diamond Jubilee wiki iliyopita jinsi Mengi alivyowafanyia sherehe ya ukarimu watu wenye ulemavu kutoka Tanzania kote. Huo ndio uzalendo wa kweli na ilidhihirika kwamba hakuna ubaguzi.
 
Back
Top Bottom