Hivi Loliondo iliyouzwa na Mwinyi kwa waarabu isharejeshwa?

Kwa wanaokumbuka kashfa iliyotikisa nchi wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi ya Loliondo watakuwa na mengi ya kusema. Je yule mwarabu Brigedia Ali wa falme za kiarabu ndiye huyu huyu aliyesafirisha twiga hivi karibuni? Je serikali ilisharejesha mbuga yetu au wamekuwa wakirithishana ulaji hasa baada ya kusikia kuwa viwanja vingi vya uwindaji vinamilikiwa na makampuni ya vigogo ukiachia mbali watu kama Pius Msekwa kuwa na maslahi binafsi kwenye dili hili?
Unanikumbusha mmoja wa wapiganaji wa enzi hizo ambaye kwa hizi siku unaweza kidogo ukamlinganisha na Saed Kubenea, the late Stanslaus Katabalo.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi na awape muda zaidi wa kuishi wauaji wake ili washuhudie uzandiki wao katika maisha yao

 
Mzee Ruksa aliuza kwa waarabu! mzee Ruksa pia anausika kumkolimba mwandishi wa habari Stanley Katabaro aliyechunguza na kuandika habari ya LOLIONDO GATE.

R.I.P Stanley Katabaro.....shujaa wetu,mzalendo wa kweli
nawapenda sana wanaosema ukweli unaoumiza, cha muhimu ni ukweli
 
nyamazia hapo hapo wala usiongeze neno ukanitibua nyongo bure,amiliki kisheria ni uarabuni hapa? Hii ni Tanzania na ardhi yk ni mali ya Watanzania.
Ukodishwaji wa vitalu ni kwa mujibu wa sheria na taratibu ilizojiwekea serikali kwa wenye sifa na vigezo kukodishwa,sasa kama wewe huna sifa usilete chuki endelea kukazana ili na wewe upate.

 
Hivi wazungu wakristo wanaomiliki migodi hawakutibui nyongo au wao ni Watanzania ???

Sio ndiyo kila kukicha tunawatufuta wawekezaji? Wawekezaji nao wana hiari kuchagua wanapopataka.
jerumani Karl Peters aliwekeana mikataba na Machifu ambao hawakujua kusoma. Je, leo viongozi wanataka wawe na kisomo kiasi gani katika kutambua athari za uwekezaji? Heri kina Abushiri na Kinjekitile.
 
nyamazia hapo hapo wala usiongeze neno ukanitibua nyongo bure,amiliki kisheria ni uarabuni hapa? Hii ni Tanzania na ardhi yk ni mali ya Watanzania.

Kwenye listi niliyoweka juu, kampuni ya Waarabu ina kitalu kimoja, jee hivyo vingine vya kina nani?
 
Yule MZUNGU WA SINGITA ANAYE MILIKI KIPANDE CHA HIFADHI KULE SERENGETI anamiliki kwa miaka 99 na Kile si kitaru cha UWINDAJI, yeye hawindi bali anahifadhi yake YENYE ZAIDI YA HEKARI 1000. hiyo ya miaka MITANO MITANO NI DANGANYA TOTO, KWANI TANGIA MWARABU AMILIKISHWE IMEISHA MIAKA MINGAP? Na kama ni miaka 5 mbona Kajenga na majumba ya kudumu?
 
Mada iliyopo ni Loliondo siyo migodi

suali kutoka kwa mtoa hoja ni
By Angel Msoffe

nyamazia hapo hapo wala usiongeze neno ukanitibua nyongo bure,amiliki kisheria ni uarabuni hapa? Hii ni Tanzania na ardhi yk ni mali ya Watanzania.

suali kwako findu fiki

kwani migodi ipo mbinguni ???
 
hii labda labda hii ndiyo inayonifanya nisihelewe hii M4C ya CDM kwa nini sisi tufikirie wenyewe labda watafanya hiki badala ya wenyewe kueleza umma unaotaka mageuzi ya kweli kua watafanya hivi...cdm iko vugu vugu kwenye mageuzi ya kweli

kuna vitu huwezi sema vyote hadharani.Kwani hata adui huweweseka akihisi unaenda pata power na bado hajui msimamo wako kwa maslahi yake.Hawa waarabu ukiwashtua watafanya sana uharibifu+ kutumia mamluki wa tZ ku terrorize Nchi.
 
Hunting Blocks hazitolewi zaidi ya miaka 5. Msidanganye watu.

ALLOCATION OF HUNTING BLOCKS WILL NOT BE REPEATED
The Ministry of Natural Resources and Tourism would like to inform the general public that the process for block allocation for the hunting tern of 2013 – 2018 was concluded in September, 2011.
The results were published through mass media in September, 2011. It was reported that, 60 companies were allocated with hunting blocks. Out of those a total of 51 companies were local (85%) and 9 were foreign (15%). The current allocation was done in conformity with the requirements of section 39 (3) (b) of Wildlife Conservation Act No. 5 of 2009.

Soma zaidi: ALLOCATION OF HUNTING BLOCKS IN TANZANIA

Zomba Grumeti Reserve na Loliondo si hunting Block km unavyodhani ingawa pia wanafanya hunting.Hawa jamaa wana mamlaka yao ambayo hata askari wetu wa wanayama pori wala watembeza watalii hawaingii.Kwa ujumla ni ubalozi fulani.Sasa ukisema balozi anakaa miaka 5 au 4 , halafu ukataka tuamini kuwa na Jengo la ubalozi linamilikiwa miaka hiyo, utapata shida elezea ni kwanini Ubalozi wa marekali umejengwa wa kudumu vile.

Kwa ujumla hao jamaa wana kila kitu chao, wana mpaka airstrips zao, wana askari wa wanyapori wao na watalii wao wanaoingia ktk maeneo yao na mengine ila wa wengine hawapiti maeneo yao.

Watu wa dar hamuujui utalii kama ilivyo kwa dhaifu na wengine ila kwa kujidai wajuaji n akuharibu mipango ya nchi mpo juu.Hao wanokodi vitalu kamuulize dr.leak yule mcahmbuzi wa mpira ndio kazi zake hizo.
 
Tanzania inabidi tugombanie uhuru wetu kwa sasa.

ila swali naomba mwenye OFFICIAL information tu ajibu, siasa pembeni kwanza
- je vitalu vya uwindaji vilivyotolewa kwa miaka 99 vimewahi kuwa vingapi hadi sasa? je kati yao kuna ambavyo vimerudishwa kwa sababau yoyote? yani kurevoke leseni au kibali/ hati au ruhusa?
- je kuna vitalu vya mbuga/mapori ya hifadhi kwa muda mwingine licha ya miaka 99 ni vipi?
- je sheria za kumilikisha zimepokelewa na wanaofahamu haya mambo au bado kuna zogo kama zilivyo sheria zingine za rasilimali zetu?
 
Tuangalie piea katika WMAs nani ananufaika? Serikali ama wakazi wa eneo husika? We have a long way to go for independence.
 
Back
Top Bottom