Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 176
Mkuu next level hauko serious juu ya kuweka akiba; unaonekana wewe ni mtu ambaye unatumia kadili unavyopata, which to me is not good kama kweli una malengo ya kufanya kitu fulani baadae!
Nina rafiki yangu mmoja anaishi DSM, wakati akipokea mshahara wa laki sita take home alikuwa anasema mshahara anaolipwa unamtosha tu kuishi basi. Alipoongzewa mshahara mpaka kufikia take home ya milioni moja na laki mbili akabadili life style kwa kuhama Tandika alikokuwa anaishi na kuhamia Sinza, pia akanunua na gari GX100. Mwaka huu mwanzoni kapata kazi nyingine kampuni moja ya nje analipwa take home ya 3.5 milioni. Tayari hivi majuzi kahama Sinza na kuhamia Mikocheni, kachukua mkopo wa gari nyingine aina ya Toyota Harrier huku akimwachia mke wake atumie ile GX100.
Next level nimetoa mfano huo mrefu kidogo kutaka kukueleza namna ambavyo waafrika walio wengi wanavyoshindwa ku manage pesa zao vipato vinapoongezeka. Wengi wakipata kipato zaidi wanabadilisha bar wanazokunywa pombe, mademu wa matawi ya juu, na magari. Hii yote ni ulimbukeni kama ongezeko la kipato hali justify kihivyo ongezeko la matumizi ya anasa!!
Mi nashauri jamaa aende kwa banker wake kwa ajiri ya kusolicit mkopo ili ajengee nyumba kwa sababu kuweka tu akiba kidogo kidogo kuna hatari ya kuja kuitumia kwenye dharula kama vile misiba, kuuguza mgonjwa n.k.
....Brother kutumia kadiri upatavyo ni hulka ya binadamu yeyote yule.....na ofcourse ipo hiyo hata kwenye msingi ya uchumi! Mambo ya propensity to save /consume etc....na matheory kibao ya DD/SS!
Ngoja niache hii mambo ya economics.....! kuna mambo binafsi ninayofanya sikuyasema hapo juu.......! Pointi yangu ilikuwa kusave cash kila mwezi kutoka kwenye mshahara ni ngumu mno mno......ndo maana hata kwenye business, ukishauza bidhaa...hela unachukulia mzigo mwingine etc etc! Sasa kwa ss tunaokinga madirishani kila mwezi, kama nilivosema ni ngumu kuweka hela eti kila mwezi, ila unachoweza kufanya...kama unamshahara mdogo, ni kuchukua mkopo bank then unanyia kitu cha muhimu mara moja........! kama unapata mshahara mkubwa unapaswa uwe na ongoing projects....such that inavoingia pesa, tayari inakuwa allocated kwenye projects bila kuchelewa!
Hao wanabadilisha life styles kwa kuwa na kipato kikubwa, hawana projects zozote, they don't plan for the future....what if huo mshahara wako unapata kesho ukakatika kwa kufutwa kazi, ulemavu etc? so the only way to save money ni kuinvest in any way......!