hivi kwanini wanaume huwachoka wake zao?

mi naonaa wababa wengi wanawachokaa wake zao kwa sababu hizi,unakutaa love moto moto iliyokuwaa kipindi cha boy/gal lover inakuwaa imepunguaa kipindi mwanamke ameolewaa hasaa akijifungua upendo alio kuwa anapewaa mwanaume,unaamiaa kwa mtoto,pili wanawake wengi wakishaolewaa ndo ilee full kujiachiaaa,yani yale mashamsham ya sijui kujirembaaa,sijui kutindaa nyusi,usafiii unakuwaa unapungua kwa wengiii,piaa mazoea yana tabu
 
Sababu ni hizi----------- wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno * *ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni Mbaya.

2.* **Hufanya kazi kwa Moyo na Huamka alfajiri na mapemaKuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaribu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haichelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa.

3.* *Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yakeKuna wanawake ambao ni wachafu – usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu, wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti mwanamke awe msafi muda wote. Wanaume wote wanapenda Usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisha “Reception” inakuwa Safi na kuwa katika hali ya kumfanya Mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha mstarehe.

4.* *Jali na timiza Mahitaji ya NDOA kwa mume wakoSulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya Ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

5.**** Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho familia itafurahia.Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Test”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.

6.**** Mwamini Mume wako,*wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza Ndoa kwa Uadilifu na Upendo. *
 
Umesema kweli kabisa Lizzy, wamama wanajisahau sana jamani, ndo sababu mimi huwa nasema nyumba ndogo haziwezi kwisha
kujisahau ni one thing, lakini kuna wamama ambao wapo bomba mno lakini waume zao moto huko nje. ni litabia tu la watu
 
Leo nilikuwa naperuzi email yangu nikakuta mada inayofanana na hiyo hebu cheki hiyo nukuu...inaonyesha wanawake wengi hugeuka kuwa mzigo kwa waume zao. kwa wana jf mliooa hali ikoje?
A man inserted an 'ad' in the classifieds: "Wife wanted". Next day he received a hundred letters. They all said the same thing: "You can have mine."
Brad Pitt
 
kama wewe mwenyewe jibu unalo kwaamba mnaharibika unataka huyo mwanaume atakuona yule tena.Cha muhimu ni nyie wenyewe kujiangalia na hiyo miili yanu
 
Kwasababu wengi ukipita mwaka baada ya kuolewa au wakishazaa wanabweteka. Wanadhani ndio mwisho wa kupendeza, kujiremba, kuongea taratibu, kudeka, kumbembeleza mume n.k
Maisha yanakua kama jeshini. . . amri na malalamiko ndio vinatawala. Ikishakua hivyo hata hamu ya kurudi nyumbani mume anakosa.

Imejitosheleza kabisa,
Mwenye masikio na asikie,
Mwenye kubadilika na abadilike!
 
Kwasababu wengi ukipita mwaka baada ya kuolewa au wakishazaa wanabweteka. Wanadhani ndio mwisho wa kupendeza, kujiremba, kuongea taratibu, kudeka, kumbembeleza mume n.k
Maisha yanakua kama jeshini. . . amri na malalamiko ndio vinatawala. Ikishakua hivyo hata hamu ya kurudi nyumbani mume anakosa.
Sio hamu ya kurudi nyumbani tu inakwisha bali hata zile simu za mahaba huwezi kumpigia tena, maana anageuka kuwa ni sehemu ya kero.
 
kujisahau ni one thing, lakini kuna wamama ambao wapo bomba mno lakini waume zao moto huko nje. ni litabia tu la watu
Unafahamu kinachoendelea ndani ya nyumba zao? au ukiona watu wanapendeza ndio unajuwa wanalala chumba kimoja?
 
Sio hamu ya kurudi nyumbani tu inakwisha bali hata zile simu za mahaba huwezi kumpigia tena, maana anageuka kuwa ni sehemu ya kero.

Mkipigiana simu na text zinakua zile za "Uko wapi?!" "Mbona ile pesa hukuacha?!!""Ntachelewa" "Mtoto anahitaji viatu vipya, ntapitia pesa ofisini". . .Hamna tena "naomba" "ahsante" "samahani" na "pole" za kupendeza masikio.
Wanaume mna kazi kweli sometimes. . .
 
im really curious, kwanini wanaume huwachoka wake zao na kutafuta kazi za nje? kama wanawake tunaweza kuwa waaminifu kwanini nyie mshindwe?
mtu anakuzalisha alafu ukisha haribika mwili, anatafute waschan wadogo, inauma sana. au wanadhani wao hawa haribiki? hata wanaume hupata kitambi na kua na mwili mbaya but wanawake huvumilia na kuendelea kumpenda.
kuna solution ya hili, kumfanya mwenzako asikuchoke?

Kazi za nje zinaongeza kipato kwahiyo zina umuhimu wake, lol!!!
 
im really curious, kwanini wanaume huwachoka wake zao na kutafuta kazi za nje? Kama wanawake tunaweza kuwa waaminifu kwanini nyie mshindwe?
Mtu anakuzalisha alafu ukisha haribika mwili, anatafute wasichana wadogo, inauma sana. Au wanadhani wao hawa haribiki? Hata wanaume hupata kitambi na kua na mwili mbaya but wanawake huvumilia na kuendelea kumpenda.
Kuna solution ya hili, kumfanya mwenzako asikuchoke?


Umegeneralise kupita kiasi.

Mimi mbona sijamchoka mamsapu wangu?

Anyway,inategemeanana vile utakavyojitunza na kujipenda pindi utakapojifungua. Kwani ukijiachia na ukawa unanukanuka maziwa,mara mikojo ya mtoto et al. ni rahisi mwanaume kujitafutia kipozeo,ingawa simaanishi kwamba hivyo ni sahihi.
 
Kumbe mambo ni rahisi sana.


....rahisi sana basi tu sisi wenyewe tunayafanya magumu. Sasa kama mtu akikuchoka ufanyeje? Nawe mchoke, songa na life yako.
Unajua kwa nini huko nchi zilizoendelea divorce nyingi? Mambo kama hayo hakunagana kulazimisha mapenzi, penzi likifa basi kila mtu kivyake.
 
Kaulimbiu ya fitness first inabidi kuchukua mkondo wake ili mimi mwanaume nisiharibike nikamuudhi my future significant other na yeye awe fit.
Halafu sitamzalisha ili na yeye asiharibike tunachanganya mbegu halafu tunatafuta artificial womb ili itubebee mtoto wetu kwa hiyo miezi 9.Mamaa anabaki ki-potabo,stretch marks free as a result nyumba ndogo is automatically out of the picture(ceteris paribus).
Then we live happily ever after.
 
nasema nyumba ndogo haziwezi kwisha

Na wanaharakat tunataka iwekwe hiyo kwenye katiba mpya...kwani katiba si ya kwetu wananchi. Safari hii vitu vyote tunatupia humo kwa katiba ili amani itawale huku mtaani.
 
Back
Top Bottom