Hivi kwanini Vijiji vya Ujamaa havikufika Kilimanjaro na Bukoba?

Maeneo yaliyolengwa sana sana ni yale yaliyokuwa sparsely populated; mikoa ya kilimanjaro, Bukoba ilikuwa densely populated; lengo la vijiji vya ujamaa ilikuwa kuwakusanya watu waliokuwa wanakaa mbali mbali na kwa uchache uchache waje kwenye eneo moja ili iwe rahisi kuwapelekea huduma za kijamii na pia iwe rahisi kuendeleza vijiji ili vije kuwa miji baadae iwapo mapinduzi ya kilimo yangefanikiwa na kupelekea uanzishwaji wa viwanda n.k;


Excellent explanation!!!!!

Ni sababu hiyo hiyo iliyofanya kusiwe na vijiji vya ujamaa Unyakyusani, yaani wilaya za Rungwe na Kyela!!
 
Maeneo yaliyolengwa sana sana ni yale yaliyokuwa sparsely populated; mikoa ya kilimanjaro, Bukoba ilikuwa densely populated; lengo la vijiji vya ujamaa ilikuwa kuwakusanya watu waliokuwa wanakaa mbali mbali na kwa uchache uchache waje kwenye eneo moja ili iwe rahisi kuwapelekea huduma za kijamii na pia iwe rahisi kuendeleza vijiji ili vije kuwa miji baadae iwapo mapinduzi ya kilimo yangefanikiwa na kupelekea uanzishwaji wa viwanda n.k;

Nakubaliana na wewe 4that reason
 
Pengine wengi wenu hapa ni vijana ambao mlikuta ama kusikia tu habari ya vijiji vya Ujamaa, hivyo maswali haya yanatokana na kutofahamu umuhimu uliokuwepo ktk kuanzisha vijiji vya Ujamaa. Nadhani kwanza ni tuelewe kwa nini vilianzishwa, hizi habari za kushindwa hazina maana yoyote ikiwa lengo lilikuwa bora kwa mendeleo ya nchi yetu.

Waswahili wanasema unaweza kumpleke pumba mtoni kunywa maji lakini huwezi kulazimisha kuyanywa... Hapa wazo la kumpeleka Punda mtyoni ni zuri na kwa faida yake lakini akikataa kunywa maji haina maana yalikuwa ni mawazo mabaya ndio maana Punda amekataa kunywa maji.

Zipo sababu mbili muhimu sana ktk uanzishaji wa vijiji vya Ujamaa, Kwanza kabisa nataka muelewe ya kwamba baada ya Uhuru wetu asilimia 90 ya wananchi walikuwa wanaishi vijijini na asilimia 80 ya pato la Taifa lilitokana na kilimo, lakini asilimia kubwa ya matumizi ya maendeleo ya nchi yetu yalikuwa mijini na sii vijijini. Hivyo, kwa kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya kilimo, na watu wengi wakiwa wanaishi katika vijiji vya asili, alibainisha kwamba ingekuwa njia nzuri ya kupeleka maendeleo vijijini kwa kupitia mfumo wa ujamaa (Lengo).

Pili, Kama alivyosema Mchambuzi, jamani siku zote vision ndio huzaa ideas na muhimu sana kutazama WATU na MAZINGIRA kabla hujaweka Azimio na kutunga strategies zinazohitajika kulingana na vigezo hivyo. Katika kutazama wingi wa vijiji hivyo ilikuwa sii rahisi kusambaza maendeleo kwa kila kijiji nchini ikiwa vijiji vingi vilikuwa vimesambaa hovyo nchi nzima. Hivyo, ikatazamwa mikoa ambayo vijiji vyake viko sehemu ambazo azma hii mpya itakuwa kazi kufikisha huduma ya maendeleo, vijiji hivyo vivunjwe na kujenga vijiji vipya karibu na maeneo ya uzalishaji na ama sehemu zilizokusudiwa kujengwa barabara kuwezesha ujenzi wa vijiji vipya ambavyo leo hii vingekuwa miji..

Kwa hiyo wakuu zangu lengo lilikuwa kupeleka maendeleo vijijini na huwezi kuanzisha vijiji tu bila mipango miji..Wenzetu Ulaya miji yao yote imepimwa, maeneo yote yamewekwa ktk hesabu za maendeleo ya nchi zao na hata sehemu zilizowazi tayari zimewekwa hivyo kwa makusudio ama kuna mipango itafuatwa miaka ijayo..Kwa hiyo mpango wa mwalimu kuanza kujenga vijiji vipya ambavcyo leo hii vingekuwa miji mipya yenye maendeleo tulishindwa kuafiki mpango ule kama Punda aliyepelekwa kunywa maji mtoni.

Hadi leo hii baada ya miaka 50 ya Uhuru, kuna vijiji ambavyo havina kabisa huduma za maji, maduka, shule zahanati, viwanda wala na wala magari hayawezi kufika. Naweza kusema Tanzania nzima leo hii haina ramani.. watu wanjijengea tu wanavyotaka, wanakotaka na kuvamia maeneo maadam yako wazi. Wengine hata hudai urithi wa ardhi ambayo haikuwahi kuwa yao wala ya wazee wao ili mradi awepo shahidi tu wakubainisha uongo huo..

Tunaijenga Tanzania siyokuwa na ramani, tazama hadi mijini nenda ukajionee Kariakoo maghogora yaliyojengwa hayana hata elevator, hakuna maji wala nafasi baina ya nyumba na nyumba..Kaitazame Sinza mji mpya ulivyokjjengwa inasikisha kwa sababu watanzania hatuna Utamaduni wa kujenga kwa ramani..

Sasa utakuta ya kwamba zipo sehemu nyingi sana Tanzania vijiji vya Ujamaa havikufika. Sio Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya tu bali mikoa mingi sana ambayo vijiji vyake vilikuwa ktk maeneo mazuri na yenye kufikiwa kirahisi hawakuwa na vijiji vya Ujamaa. Tazama Mwanza, Musoma, Mbeya, Tanga na Tabora, mikoa ambayo ilikuwa ya uzalsihaji mkubwa wa kilimo nchini wakati wa mkoloni...vijiji vyao vimekuwepo ktk maeneo mazuri na wakazi waliishi ktk maeneo ambayo tayari huduma zilikuwa zinawafikia..Vijiji vingi ktk maeneo hayo vilijengwa na wakoloni kutokana na kwamba walikusanya mazao kutoka mikoa hiyo ya uzalishaji hivyo hapakuwa na sababu ya kuunda vijiji vipya wakati wananchi waliishi tayari ktk vijiji ambavyo huduma zilikuwa zinawafikia.

Katika mipango miji, serikali ni lazima ichore ramani ya miji yetu. Nasikia ukienda ofisi ya Ardhi utakuta ramani ya mji wa Dar kama ulivyokusudiwa na Mjarumani - Utalia kilio cha kughafirika kwa sababu mji huo unaonekana mzuri ulopangwa vizuri lakini leo hii Dar Es Salaam ni mji tofauti kabisa na ule ulokusudiwa, kisha tunalalamika usafiri mbaya, hakuna maji, umeme shida, mvua zikinyesha mji wote mafuriko na kadhalka.. Hii yote ni kwa sababu tumeujenga mji wetu pasipo kufuata ramani bali kipenda roho..Zile zile tabia tulokuwa nazo kabla ya Ujamaa na kujitegemea - Watu kuvamia maeneo, kujenga hovyo hatutaki kupangiwa sheria ya kuishi... Halafu tunajiuliza sheria iko wapi viongozi wanapokiuka sheria. Nani kweli anafuata sheria nchini kwetu? Utamaduni huo tumeupata wapi ikiwa sheria kwetu ni utumwa wa kutawaliwa...

Lakini ikitokea serikali kutaka kuwahamisha wanalalamika kuhamishwa maeneo yao kwa sababu inatakiwa kujengwa barabara, viiwanda, mji mpya na kwa kutumia dhana hiyo serikali imeweza kuwahamisha watu pasipo hiari yao na kuwapeleka ktk maeneo mapya. Majuzi tu Machinga huko Mbeya wamekiwasha hawa wana tofauti gani na wananchi waliokataa kuhamia vijiji vya Ujamaa!... Na kweli serikali imeshindwa kuwaondoa machinga mijini, wameshindwa kuondoa vibanda vilivyojengwa mbele ya nyumba kujenga maduka ambayo yamechukua hadi sehemu za barabara. Residential areas zimekuwa ndio sehemu za biashara, maduka, viwanda na kadhalika..

Je, kutokana na kiburi hiki cha Wadanganyika, kutokuwa na ustaarabu unaweza kuita ndio kushindwa kwa serikali iliyopo madarakani!
 
eeeh kwa hiyo umakini wangu unautilia shaka kwa kuwa sijasema uchagani badala yake nimesema kilimanjaro kwenye heading!acha uvivu wa kusoma jenga tabia ya kusoma post yote sio kukurupuka na heading tu basi....
We ni mjinga,heading yako inasemaje na ndani ni uharo mtupu,acha ujinga wewe,unashindania upuuzi,we nawe great thinker?

Nimekwambia kuna vijiji vya wachagga vilivyokuwa na mashamba ya kijiji,maduka nk,vyote vya kijiji,na hayo ni mojawapo ya hizo characteristics za vijiji vya ujamaa,inaelekea kichwa yako nazi wewe,tena koroma!

Usintapishe na huu upupu!

Hunijui we **** na sikujui...Judge on upupu unaobandika na kujitetea kama uko kwenye mashindano,heading iseme Kilimnjaro halafu utake majibu ya uchaggani peke yake,as if Kilimanjaro iko occupied only na wachagga,hopeless wewe,usinpotezee muda.
 
Niliwahi kuomba kiwepo pia kitufe cha kubovyo mtu anapokerwa na post ya mwenzake kama ambavyo kipo kitufe cha Like unapofurahishwa na hoja ya mwenzako.
 
Labda "kujenga nchi" maana tuliimbishwa sana tanu(ccm)yajenga nchi enzi zile lakini mimi nilikua najiuliza hivi inatakiwa kujenga nchi au maisha yetu wananchi??
Hata waliosimika mataifa makubwa kama Marekani wangekuwa na mawazo ya kujenga maisha yao tu, mataifa hayo yangekuwa ya hovyohovyo kama Tanzania. Nyerere did his best, waliokuja kumpokea ndio wamekuja kuuza uhuru wa nchi, and we have to fight again for independence.
 
Sijui kwa Bukoba lakini Kilimanjaro walienda - au tuseme walijaribu

Nakumbuka wakati huo Mkuu wa mkoa alikuwa Peter Kisumo
Simulizi zinasema Alijaribu kuyapeleka hayo na kilichompata hatasahau.

Kuna historia ya sehemu moja huko moshi vijijini panaitwa Mtemboni - palikuwa pawe Tahrir - akabwaga manyanga na hawakurudia tena kuongelea hilo jambo

Tatizo la kukariri ndiyo lilileta shida
 
Nachoelewa mie ni kwamba villagisation ililenga kuharmonise maendeleo ili watu waje pamoja na kushiriki ktk kazi za kimaendeleo kwa pamoja,hii ni kati ya falsafa 4 za Nyerere ikiwemo,UNITY,LOVE.WORK na VOCATION..Kitu ambacho tayari hayo maeneo walishaweza kutokana na mifumo ya ukabaila ya Nyarubanja na Kiyanja

Lakini pili isingewezekana sana ktk maeneo hayo kutokana na wenyeji kuwa wanamiliki kubwa za mali katika maeneo yao k.v mashamba makubwa,mazao,nyumba za kudumu na uwepo wa vituo vya huduma mahala pao tokea enzi za wakoloni kwa vile walikuwa feudals.

Hii ilikuwa ni tofauti kwa maeneo mengine ukizingati wengine hata leo bado vijiji havieleweki,kijiji jina lakini nyumba na wanakijiji ni wa kuhesabu,nihishie hapa lakini ukitaka kuelewa zaidi 'ROMANTIC' tafadhari tembelea maeneo hayo naamini u will learn alot,

Bado naamini Nyerere alitumia akili na si ujinga wala ujuaji
.
 
Sijui kwa Bukoba lakini Kilimanjaro walienda - au tuseme walijaribu

Nakumbuka wakati huo Mkuu wa mkoa alikuwa Peter Kisumo
Simulizi zinasema Alijaribu kuyapeleka hayo na kilichompata hatasahau.

Kuna historia ya sehemu moja huko moshi vijijini panaitwa Mtemboni - palikuwa pawe Tahrir - akabwaga manyanga na hawakurudia tena kuongelea hilo jambo

Tatizo la kukariri ndiyo lilileta shida
Sawa kabisa kwamba Vijiji vya Ujamaa vilipata upinzani mkubwa kutoka kwa watu ambao hawakutaka maendeleo na hakika hadi leo hii hakuna maendeleo..Ni sawa na vita ya Machinga, leo japokuwa hawa hawakutayarishiwa makazi mapya lakini Nyerere alijitahidi sana kuanzasha vijiji vipya kwa lengo la kupeleka Maendeleo vijijini, bahati mbaya ile sababu ya pili ya punda kutotaka kunywa maji ndio kulipelekea azimio hilo lishindikane.

Kilimanjaro, Mbeya na Bukoba kote mashambani walijaribu kuwasogeza walokuwa nje ya huduma muhimu wakakataa kwa sababu Wadanganyika hatukuwa na Utamaduni wa ujenzi wa miji au vijiji isipokuwa kuvamia ardhi na kuyafanya makao mapya. Maendeleo yoyote hutanguliwa na kupatikana kwa huduma muhimu jambo ambalo sii utamaduni wetu, tunapenda au tulizoea kusafiri maili 10 kutafuta maji, shule na hospital na ndio maana leo ni asilimi 15 tu ya wananchi wanapata Umeme na maji safi..

Mwisho wa yote haya vijiji vyetu letu havina huduma muhimu na wala hakuna maendeleo vijijini, na kuna maeneo hadi leo yana watu bado kabisa wanatembea uchi, kuna NGOs zinazofanya biashara kututangaza ktk TV kuonyesha umaskini wa Watanzania - hao Punda walokataa kunywa maji..
 
Kama alivyoeleza mchangiaji aliyetangualia, zoezi la vijiji vya ujamaa lilikuwa practical zaidi ktk maeneo ambayo yalikuwa sparsely populated.

Kilimanjaro ardhi siyo kubwa kiasi hicho na wananchi tayari walikuwa karibu karibu. Kuna vihamba vya kahawa lakini navyo siyo vikubwa kulazimisha wananchi wakusanywe kuanzisha vijiji vya ujamaa.

Suala la LAND OWNERSHIP, na the fact kwamba KAHAWA ni zao la kudumu, naamini vilikuwa kikwazo cha kuanzisha vijiji vya ujamaa Kilimanjaro.
 
Eeeeh!mi nimeuliza na wewe unaniuliza mimi tena!!kweli sisi ni wabongo asilia....

Kuna watu huwa wanasubiria matatizo ya wengine ili wapate suluhu ya shida zao, ndo maisha na akili za wabongo, shusha tu munkari utazoea.
 
Sungurampole said:
Nakumbuka wakati huo Mkuu wa mkoa alikuwa Peter Kisumo
Simulizi zinasema Alijaribu kuyapeleka hayo na kilichompata hatasahau.


JokaKuu said:
..kama alivyoeleza mchangiaji aliyetangualia, zoezi la vijiji vya ujamaa lilikuwa practical zaidi ktk maeneo ambayo yalikuwa sparsely populated.

..Kilimanjaro ardhi siyo kubwa kiasi hicho na wananchi tayari walikuwa karibu karibu. Kuna vihamba vya kahawa lakini navyo siyo vikubwa kulazimisha wananchi wakusanywe kuanzisha vijiji vya ujamaa.

Endapo kijiji flani kinaitwa kuwa ni cha ujamaa,ni kwasababu kilianzishwa na kikaitwa "Kijiji cha ujamaa" ama ni kwasababu ya characteristics zake ndizo zinazofanya kijiji kiitwe cha ujamaa?

Hapa kijiji cha ujamaa kiko determined on population?
 
jmushi1,

For the purpose of this discussion nadhani ni kijiji kilichoanzishwa na kuitwa "kijiji cha ujamaa.

Pia kuanzishwa kwake kuwe muitikio na utekelezaji wa zoezi zima la "operesheni vijiji.
 
Last edited by a moderator:
Natumaini muuliza swali aliposema Bukoba na hapo hapo akasema Kilimanjaro alikuwa anataka kusema Kagera badala ya Bukoba!

Na pia kwamba kwa kusema Bukoba labda aliataka kusema, kule kwa Wahaya peke yake(Wilaya za Bukoba mjini, Bukoba Vijijini na Muleba tu).

Sasa, ikiwa ni Kagera au kwa wahaya, jibu ni kwamba katika Mkoa wa Kagera kulianzishwa vijiji vya ujamaa sawa na sehemu zingine. Mfano ninaoufahamu kwa uhakiki ni Kijiji cha Ujamaa cha Rushwa.

Hiki kiko wilayani Muleba. Pia mfano mwingine ni katika wilaya ya Biharamulo. Vijiji vingi tu vya ujamaa. Kama walivyosema waliotangulia, watu waliokuwa wakikaa mbalimbali ndio waliokuwa wanatakiwa wakae pamoja ili imwe rahisi kuwahudumia.
 
jmushi1

Alaaa kwa hiyo unataka tutoleane lugha za kifedhuli si ndio?! Bahati mbaya sana hiyo siyo style yangu kaka,japo lugha hiyo naiongea pia!

Tatizo We inaonekana u decide not to understand sasa mimi bahati mbaya sana sina muda wa kukulazimisha unielewe brother,walionielewa wanaendelea kutiririka na mimi na take notes,so lengo langu la kujifunza na kuelewa hii kitu linaonekana kufanikiwa!na hii ndio raha ya kuwa na great thinkers wengi,ili wengine wakichagua kutoelewa kwa makusudi au vinginevyo,wengine wengi wanaendelea kumwaga "shule"
 
Last edited by a moderator:
Alaaa kwa hiyo unataka tutoleane lugha za kifedhuli si ndio?! Bahati mbaya sana hiyo siyo style yangu kaka,japo lugha hiyo naiongea pia!Tatizo We inaonekana u decide not to understand sasa mimi bahati mbaya sana sina muda wa kukulazimisha unielewe brother,walionielewa wanaendelea kutiririka na mimi na take notes,so lengo langu la kujifunza na kuelewa hii kitu linaonekana kufanikiwa!na hii ndio raha ya kuwa na great thinkers wengi,ili wengine wakichagua kutoelewa kwa makusudi au vinginevyo,wengine wengi wanaendelea kumwaga "shule"
Mkuu kuchangia thread yako ni respect tosha ulitakiwa ujuwe hilo.
However samahani,lets move on.
 
Back
Top Bottom