Hivi kwanini Mahakimu uitwa Waheshimiwa

doup

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
2,346
2,151
Leo nilikuwa mahakamani , nilishangaa kuona hata hawa wauaji (polisi) na wengineo wakinyenyekea na kila mara kabla ya kuongea uanza na "muheshimiwa"

nikajiuliza je nikimuita ndungu Hakimu kuna Kosa?
 
Leo nilikuwa mahakamani , nilishangaa kuona hata hawa wauaji (polisi) na wengineo wakinyenyekea na kila mara kabla ya kuongea hua nza na "muheshimia"

nikajiuliza je nikimuita ndungu Hakimu kuna Kosa?

Mi nadhani ni mazoea tu ya wabongo kutukuzani Huko kwa wenzete hilo neno hata ni gumu kulipata translation yake. nadhani watanzania tunasumbuliwa na "Inferiority complex syndrom"
 
Leo nilikuwa mahakamani , nilishangaa kuona hata hawa wauaji (polisi) na wengineo wakinyenyekea na kila mara kabla ya kuongea hua nza na "muheshimia"

nikajiuliza je nikimuita ndungu Hakimu kuna Kosa?

Unafiki tu na kujikomba hakuna lolote!
 
Wanaitwa waheshimiwa kwasababu ndio watu wenyetaaluma ya pekee katika kutafsiri sheria za nchi zinazotungwa na bunge linalokaliwa na waheshimiwa wa bunge walio chaguliwa na ninyi wananchi wenye akili timamu.
Angalizo. Si kila mtu ataitwa mheshimiwa, ingekua ni vivyo hata wapishi wangepata kuitwa vivyo.
 
Ole wako usimwite muheshimiwa unaweza maliza kuongea akakuambia hakuoni au ageukie upande wapili wakati unaongea ,hizo ni taratibu za kimahakama. Your Honour
 
Hilo neno "mheshimiwa" huwa linaniudhi sana jinsi watu wengine wanaona ni maalum kwa ajili yao tu.Ninavyojua kila mtu ni mheshimiwa pale alipo.Utajiitaje mheshimiwa wakati na wewe utakufa tu kama mimi?
 
Ole wako usimwite muheshimiwa unaweza maliza kuongea akakuambia hakuoni au ageukie upande wapili wakati unaongea ,hizo ni taratibu za kimahakama. Your Honour

asante, ningejikuta na wajibishwa kwa umbumbu.
 
kwan tatizo ni nin?kama unataka na ww kuwa hakimu uitwe mheshimiwa..vinginevyo yaache mambo kama yalivyo
 
Leo nilikuwa mahakamani , nilishangaa kuona hata hawa wauaji (polisi) na wengineo wakinyenyekea na kila mara kabla ya kuongea uanza na "muheshimiwa"

nikajiuliza je nikimuita ndungu Hakimu kuna Kosa?

mkuu,udugu uliisha enzi za mwalimu sa iz kuna "wanaoheshimiwa" waheshimiwa, na kinyume chake(kinyume cha kuheshimiwa). Wanaheshimiwa kwa kuwa wanauwezo wa kugeuza nyeupe ikawa nyeus na nyeus ikawa nyeupe! Wamagogoni,wamjengoni na hata wa huku katani wote ni "waheshimiwa". Walibaki ni kinyume cha waheshimiwa!(jina naogopa kulitaja, linaudhi!)
 
Ni mazowea tu hayo, maana waheshimiwa wa kweli duniani ni baba na mama, pamoja na babu na bibi- wengine is just ndugu
 
Kwanza hata ukichunguza hao wanaowaita WAHESHIMIWA si kweli kuwa wanamaanisha so mi nadhani ni UWOGA NA UNAFIKI tu ndio unaotusumbua kwani hakuna sehemu ktk Katiba au popote panapotaja kuwaita watu fulani ni waheshimiwa. Pia hakuna adhabu wala faini 4 It.
 
Back
Top Bottom