Hivi kwa nini Wanaume wengi wanapenda kusaidia 'UKWENI'

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF,
Nimefanya utafiti kidogo kwenye hili jambo, kupitia kwa jamaa zangu na marafiki zangu na jamii kwa ujumla nimeona, ni kwa nini Wanaume wengi wanapenda kusaidia sehemu walipokwenda kuoa 'UKWENI'
Mwenye sababu achangie...
 
unaongeza point mamsap akukubali zaidi hasa miaka ya mwanzo ya NDOA. Wanaume tu wadhaifu kwa wanawake, mwanamke akiwa mrembo chochote akikitaka kikiwa ndani ya uwezo wa mwanaume sometimes hata kwa kuiba mwanaume atatafuta tu alete. naupenda ule wimbo wa O'TEN akitakacho binti mwanaume lazima atanunua. mifano iko kibao tuu. usishangae unamjengea demu tena nyumba ndogo kigorofacmbezi beach wakati wife wako anakamata daladala kwenda kazini. wanaume huwa tunapataana saaana lkn inapofika suala la mwanamke mtatoana roho. so mkuu wala usishangae
 
Kwenu si wanakufahamu toka ukiwa mtoto na umekuwa ukiwasaidia kabla ya kuoa na hivyo umejenga jina kwao. sasa unajenga jina upande wa pili.
 
Haya mambo kumbe ni universal...nilisoma article moja yahoo walikuwa wanazungumzia suala kama hili;

Wanasema mwanamke akiwa na tabia ya kujikomba na kujiweka karibu na in-laws wake basi ndoa yake inakuwa na migogoro mingi hata kuvunjika...tofauti na wanaume...eti wanaume wanaojali wakwe zao ndoa zao uwa na amani na ni more likely kudumu....walitoa maelezo zaidi ya kitaalamu lakini siyakumbuki ila niliondoka na somo la ku stay away from my in laws..
 
Yani hata ujikombe vipi wengi wao ni mwiba. ila kuna familia ambao ni wakwe wazuri.

mara nyingi hii negative attitude kutoka kwa wakwe,inasababisha upande wa mwanamke ndo uonekane mzuri.

Haya mambo kumbe ni universal...nilisoma article moja yahoo walikuwa wanazungumzia suala kama hili;

Wanasema mwanamke akiwa na tabia ya kujikomba na kujiweka karibu na in-laws wake basi ndoa yake inakuwa na migogoro mingi hata kuvunjika...tofauti na wanaume...eti wanaume wanaojali wakwe zao ndoa zao uwa na amani na ni more likely kudumu....walitoa maelezo zaidi ya kitaalamu lakini siyakumbuki ila niliondoka na somo la ku stay away from my in laws..
 
Wana JF,
Nimefanya utafiti kidogo kwenye hili jambo, kupitia kwa jamaa zangu na marafiki zangu na jamii kwa ujumla nimeona, ni kwa nini Wanaume wengi wanapenda kusaidia sehemu walipokwenda kuoa 'UKWENI'
Mwenye sababu achangie...
mwanaume sifa ukweni bana,unaenda kusalimia full mazaga,unagawa mpunga kwa familia ya mkeo.unawajengea bonge la mjengo,afu kwenu nyumba la udogo hahaha.DUH
 
unyanyasaji wa kijinsia, kwa nini waume wapelekeshwe, haki za jinsia wafuatilie hili.
 
Mbona wanawake wanapofanyiwa ukatili na wanaume,wanapocheatiwa na wanaume,mnaotetea hizo haki hamuonekani?ila ikiwa mwanamke kafanyiwa jema basi haki za mwanaume zimekuwa violated!

Inamaana wazazi wa mwanaume wakizawadiwa na huyo mwanaume ndo haki zake hazijawa violated?mmh!
 
Back
Top Bottom