Luali
Senior Member
- Jan 1, 2013
- 101
- 11
Habari ya leo waungwana,
Tafadhali ningependa kujua hivi ni kwa nini serikali kama serikali isiwe na vituo maalum ambavyo vingesambazwa mpaka vijijini,vitongojini,mijini na hata baadhi ya mitaa ili wananchi wawe na nafasi kubwa ya kutoa malalamiko yao kisheria na hata hivyo italeta hamasa ya kuzuia vitendo vya unyanyasaji juu ya wananchi dhidi ya sheria na haki zao kwa maana tathmini zinaonyesha fika kwamba asilimia kubwa ya wananchi ni waoga kwa kuwa hawafahamu sheria ama haki zao kama wananchi hivyo kudhulumiwa ama kuburutwa kwa kutofahamu haki zao. Na pia, kwa kuwa wananchi wengi hawawezi kumlipa wakili ama kuwa na wakili maalum hasa katika familia za hali ya chini ama watu wenye kipato cha hali ya chini - vitendo vingi vya haki za binadamu vinafanyika ila wananchi hawajui waanzie wapi mfano wanajeshi,polisi wanapochukua sheria mkononi au kiongozi wa serikali kuishi kwenye mtaa ama eneo akitaka kuishi tofauti na misingi ya sheria ama katiba inavyomruhusu aishi kama raia mwengine wa kawaida, na asijipe madaraka pasina na katiba ama sheria zilizopangwa