Hivi, kuwaanzishia au kuanzisha makundi ya wanawake kunawasaidia?

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,272
31,393
Kuna haya mambo ambayo yameanzishwa kwa ajili ya wanawake pekee, je kuna manufaa yoyote wanayoyapata kwa kuanzishwa na makundi hayo..????kuna TAMWA, TAWLA, MEWATA, MALKIA AKAUNTI, UWT, WIZARA INAYOWAHUSISHA WANAWAKE, TANZANIA WOMEN BANK (TWB), ....etc.....etc
 
Dah mkuu hivi vikundi ni NGO's za wanao jiita wasomi ili wapate ulaji na wanapata kweli fedha angalia akina mama wenye vikundi hivyo vizuri wanavyo tengeneza pesa bila kuvuja jasho.
Kuna watu wana hitaji misaada kweli akina mama wapo vijijini huko wanataabika kweli kweli wengi wanakosa huduma za msingi kama wanawake lakini vikundi hivyo vimejikita mijini tu huku vijijini hawaendi kama wanaenda wanaenda kwa kuzuga napo mara moja kwa mwaka wanapo andaa report kwa wafadhiri ili wamwagiwe mpunga tena.
Naona havina msaada wowote ni wizi tu.
 
Malkia Acount is better, kwa sababu ni hela yako unaweka mule hawana miujuiza na wewe kama hujaweka hela. Hayo mengine yote yanatupotosha tu wanakula hela eti wanasaidia wanawake. WAMELUBA MJINI HAWAENDI VIJIJINI, KASEMA NANI WANAWAKE WA MJINI TUNA SHIDA???? HE!
 
Big up kwa MEWATA na TAWLA pekee. Wengine naona kama miradi ya kujinufaisha tu!
 
Back
Top Bottom