Analytical
Senior Member
- Mar 7, 2011
- 149
- 73
Nilikuwa naangalia kwenye Michuzi blog, wakati wa kuzindua Flaviana Matata Foundation, ambayo pamoja na watu wengine ilihudhuliwa na wabunge kama January Makamba na Zitto Kabwe. Mgeni rasmi akiwa mkurugenzi wa Utamaduni katika wizara ya Habari Profesa Mwansoko. Naona ilikuwa Kiingereza tu tokea mwanzo mpaka mwisho. Hii inaashiria nini? Au mantiki ya uzinduzi huo ilikuwa ni kwa ajili ya nani? Je labda Falaviana ndo alikuwa hajui kiswahili? au wageni waalikwa walikuwa hawajui kiswahili? Au ni nini? Sina uhakika kama kulikuwa na yeyote kati ya waliohudhuria hakuwa anajua kiswahili kwa maana ya kutoelewa kinachoendelea. Lakini hata kama ni hivyo mbona nchi zingine wanatumia lugha zao kwenye makongamano yao. Au kiingereza kwetu ni nini? Kama waandaaji wamo humu wanaweza kunifafanulia hii mantiki.