Hivi kutongoza ni kosa?

Blaza tatizo kubwa ni timimg.
Kila kitu duniani ni timing tu.

ukisoma alama za nyakati unaweza mpata yeyote umtakaye.

Uhandsome pekee si hoja Shule mmmh!
Pesa, nayo wakati fulani haioni ndani.

Timing ndo kila kitu blaza.

ukitongoza onyesha kwamba umezimika, siyo kwa masafa mafupi bali ya kati.

Eti maneno mawili matatu mara unaonyesha nia na dhamira ya kula uroda.

Wakati mwingine mimacho yako au hata posing yako inaonyesha jinsi unavyotamani.

Mademu wengi cha kwanza wakipendacho ni mahusiano, ni urafiki siyo majambos.

Majambozos ni matokeo tu.

Mimi pamoja na shati langu la kutoboka mabega, enzi zangu nisha wahi tembelea mijiwanja ya nguvu bila nini wala ni.

Blaza timing blaza.

Usisukumwe na hamu ya kutaka uroda, ujenzi wa hoja na mfuatano wa mambo ndiyo jambo la kujenga msukumo.

Usilazimishe mambo hata siku moja.

Ukiwa huku majuu pochi ndo inatongoza.

Huku hapendwi mtu kwanja lake wala sura,inapendwa pochi tu.

Labda hapa mkuu utujuze kama unatafuta demu wa kugonga tu one-time kisha ukimbie au unatafuta mchumba ukaoe???kama ni kugonga tu fasta , sidhani kama unapasa kuweka usanii wote huu, kwa style ya maisha ya sasa!
 
Wana JF nimekuwa nikijiuliza siku nyingi swali hili na sipati jibu sahihi.Utakuta umempenda mtu unaona ni heri umueleze kilicho moyoni mwako tena kwa upendo na upole tu,lakini matokeo yake majibu utakayokutana nayo inakuwa kama vile ni adhabu,utaambiwa huna adabu,kamtongoze mama yako,utapewa misonyo,pengine hata kichapo toka kwa watu,wengine waliwahi hata kusakiziwa mbwa,na mbaya zaidi unawezakuta mtu hakutaki lakini anaamua tu kukukomesha kwa kukupa shida zake zoote na wewe kwa kuwa umependa basi utamtimizia na bado unaambulia patupu.Mengine tunayokutana nayo wakuu mnaweza kuongezea lakini swali langu ni hilo,je kutongoza ni kosa mpaka wanaume tustahili adhabu zote hizi?

Mkuu, hio ndo hali yao, hata kama yuakutaka ndo atafanya hajihisi na wewe kabisa!!!!!, ndio Maumbile yao, Wewe usikate tamaa mpaka mwisho uone kweli hataki.

Nakumbuka nikiwa shulle ya Sekondary, jamaa mmoja sura mbaya(Afadhali REMMY ONGALA), alikuwa atongoza waschana , sisi twamcheka akitupiwa makohozi bwana; baadae wamuona anaongozana na kitoto hicho hicho kilikuwa kikitupa makohozi, tulifikiri ana hirizi lakini kumbe ilikuwa Determination na wadada ndio wapendavyo!!!
 
Kwa taarifa yako
Mwanamke akikaa wiki hajatongozwa hujiona hajakamilika
Kumbuka pia
Hata chui/simba jike huzaa
jamani kimbweka hata kama lololl wiki ndo ujione mkosi si kweli naomba reseach methodology yako na kama is just info from somewhere pleas nipe source yake.si kweli:nono:
 
sifa kubwa mwanamke aliekamilka ni kutongozwa hatakama ni mke wa mtu (kama wewe nimtokaji au unashuguli za hapa na pole ndani siku 7 lazima ukutane hilo hata kama ni utani ,utani mwisho kweli)
 
Hizo geresha tu, wengi wao wanapenda kutongozwa. Ila style yako isiwe kingono zaidi!

Kweli mkuu. Kutongoza wala kutongozwa siyo kosa ila wengi wetu tunakurupuka kwa hiyo tunaonekana wapuuzi zaidi. Hatuna ustahimilivu ambao unahitajika ili kumtunzia heshima huyo mtu tunayetaka kumtongoza. Tunakuwa kama vijana wa mitaani na misemo yao...kumtokea demu. Mwanamke mwenye heshima zake hapendi kitu cha namna hiyo hata kama ana feelings na huyo mwanamume. Vijana inabidi watulize ball waende taratibu..Kama wana tatizo basi waulize..tutawapatia ushauri wa bure.

Rt Maj Gen DC(1947).
 
Kutongoza ni an art ambayo inahitaji talent na convincing power...yaani kwa ufupi kabla hujamtokea msichana/mvulana (nisiwe biased) inabidi uwe at least uwe na ka'talent ka kumsoma mtu, yaani usije tangaza ndoa kwenye msiba!! Na wasichana mara nyingi hawasikilizi maneno unayoongea ila wanadeal zaidi na body language, in short wanakusoma how confident u are ndo maana wengine wanaweza hata kukutukana ili wajue utareact vp ktk situation kama iyo....Kama Madela alivyosema timing is everything na remember confidence is power!!
 
Pole Paka maskini mpaka mawe huo ni unyanyasaji wa jinsia:doh:

Mama sio mimi ila ni jamaa tu, lakini pole yako nitaifikisha kwa mhusika.Unaona jinsi mnavyotunyanyasa kijinsia tungekuwa sisi tunawafanyia hivyo malalamiko yangeshafika TAMWA siku nyingi ,sijui lini kitaanzishwa chama cha kutetea haki za wanaume?
 
Hutongozi tu kila mtu bara barani soma kwanza alama za nyakati. Mpe muda naye wa kukufahamu sio wewe kwa kuwa umemuona na unajua nyendo zake basi ukadhani naye anakujua. Hata ingekuwa wewe utamkubalia mtu ambaye hujawahi muona?

Sawa mkuu kwa yote usemayo lakini hebu jiulize unapokuwa umekutana na mtu na ikatokea love at first site,na hujui kama usipomsemesha na kumuomba contacts zake utamuona wapi tena utafanyaje?
 
Sawa mkuu kwa yote usemayo lakini hebu jiulize unapokuwa umekutana na mtu na ikatokea love at first site,na hujui kama usipomsemesha na kumuomba contacts zake utamuona wapi tena utafanyaje?

Unafanya homework zaidi...na kutumia talent na ustaarabu pia badala ya kuingia ki-bongo flava!
 
Unafanya homework zaidi...na kutumia talent na ustaarabu pia badala ya kuingia ki-bongo flava!

Sawa mkuu kwa uyasemayo lakini wakati wewe unafanya homework yako mtu anaendelea na safari zake na hujui utamuona lini tena ufanyeje kuepuka adhabu zitokanazo na kosa la kutungoza?
 
Sawa mkuu kwa uyasemayo lakini wakati wewe unafanya homework yako mtu anaendelea na safari zake na hujui utamuona lini tena ufanyeje kuepuka adhabu zitokanazo na kosa la kutungoza?

Kwani kufanya homework inahitaji sekunde ngapi? Kama wewe siyo troubleshooter basi unakula kwa macho na kuondoka. Kwani ni lazima kila chakula kizuri ukile?
 
Wana JF nimekuwa nikijiuliza siku nyingi swali hili na sipati jibu sahihi.Utakuta umempenda mtu unaona ni heri umueleze kilicho moyoni mwako tena kwa upendo na upole tu,lakini matokeo yake majibu utakayokutana nayo inakuwa kama vile ni adhabu,utaambiwa huna adabu,kamtongoze mama yako,utapewa misonyo,pengine hata kichapo toka kwa watu,wengine waliwahi hata kusakiziwa mbwa,na mbaya zaidi unawezakuta mtu hakutaki lakini anaamua tu kukukomesha kwa kukupa shida zake zoote na wewe kwa kuwa umependa basi utamtimizia na bado unaambulia patupu.Mengine tunayokutana nayo wakuu mnaweza kuongezea lakini swali langu ni hilo,je kutongoza ni kosa mpaka wanaume tustahili adhabu zote hizi?

Halafu mimi kinachonishangaza kwa hawa wenzetu wa kike akikuta yeye ukamkataa ebwana ee, utakoma, utazushiwa mbovu wewe na mtaani hapo atahakikisha hupati yeyote, atakudharau mwanzo mwisho...hayo yamenikuta mwenzenu cjui kwa wengine
 
Mkuu usihangaike na mambo ya nature,

Just learn how to learn people and you will be safe.
 
Adhabu kubwa niliyowahi kupewa ni kuwa yule demu niliyemtokea alimwadithia sista wangu, sasa sista naye akanishikia bango kuwa atawaambia wazee.. Nilipata shida kweli kipindi kile yaani hata maji ya kuoga nilikuwa naenda kumletea sista ili tu atunze siri. Nilijuta kutongoza, yaani mpaka leo huwa sitongozi mademu ambao wana connection na watu wangu wa karibu kwa kuhofia demu kunidhalilisha. Wengine ukiwapigia simu kama wako na rafiki zao wanakuwekea loud speaker halafu wanakuchora wakiwa na marafiki zao ukiandika meseji ndo mbaya zaidi maana inaachaga ushahidi:A S angry::A S angry::A S angry:

Ndo maana siamini kabisa kwamba mapenzi ya kweli yapo siku hizi, huwa natamani tu. Ukimpata demu kula kisha Ondoka zako, haya mambo ya kujifanya kuweka kambi ndo matokeo yake hayo:
Kugeuzwa ATM.......... life goes on....
 
Hiyo unayoongelea ni michezo ya ma-teen. Hebu pata busara za watu wazima na utayaona ya kawaida?

Kama uko under 18 au ndo umevuka basi unahitaji kusaidiwa. Let us know how we can help u. Kutongoza hata rafiki wa sister wako ni kawaida tu na hutakiwi kupata mateso. Suala ni jinsi unavyofanya kitu hicho. U need to be very strategic vinginevyo unaaibika kama ilivyokutokea! The bottom line ni kuwa hujafanya kosa lolote hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom