Hivi kuna ulazima wa kuoa/kuolewa??

Sio lazima kuoa au kuolewa.ila kuna andiko ktk biblia linasema ni heri kuoa au kuolewa kuliko kukaa mwili ukawaka tamaa.maana yake ni kuwa tamaa ni dhambi, na kama ujuavyo tamaa huanza mengineyo kama kupenda,kutongoza, mwisho mnaivuja ile amri ya sita isemayo usizini. Hivyo acha kuoa/kuolewa ukiwa na uhakika unaweza kuvumilia na kuishi maisha yasiyokuwa na matamanio hasa ya kimwili usije ukatenda dhambi.
 
tamaa haiwezi kuwa dhambi kila mtu aliekamili anahisia lazma atamani.
Hata hivo sifagili ndoa NG'O
 
wengi wanaotaka kuoa/kuolewa wanasema sababu ni aidha umri kusogea sana ama kupiga hatua kiuchumi(kumiliki mali)

1. umri; nasikia ukiwa mzee utakosa msaidizi na life litakuwa gumu ndomana watu husema usipooa uzeeni ni shida
2. uchumi; wengi tunaamini wanawake wanajua kutunza fedha na pia mtu akioa anatulia/matured na anakuwa mtafutaji ili kulisha familia.
ndoa ndoano baba
 
Hata hivyo ili kuzaa sio lazima uoe au kuolewa. Ni woga wa binadamu dhidi ya maneno ya wanajmii ndio unaopelekea watu kulazmisha kuoa au kuolewa. Nawafagilia sana wadada wanaoendesha maisha yao bila kuwa na mtindio wa kutaka kuolewa

Unawafagilia? wapigie deki kabisa, adha wanayopata unaijua au wasema tu kwa sababu hujui? Kawaulize kabla ya kuwafagilia watakwambia.
 
waseme waliopo kwenye ndoa faida wanazopata

Faida gani kubwa wanazozipata?!, wakati kila siku wanalia humu kwenye JF., Mi naona watu wengi wanaoa au kuolewa kutokana na pressure tu wanayoipata kutoka kwenye jamii leo hii, kama hujaoa au kuolewa, kutwa nzima watu wanakuzungumza wewe, embu check zile ndoa zilizovunjika baada ya muda mfupi, ambazo nyingi ni za miaka hii, waliokuwemo humo wanajuta na hawana hamu ya ndoa tena, hivi unajua wengine mfano wanaolewa tu ili ijulikane alishawahi kuolewa hata kama hiyo ndoa anajua kabisa si ya kudumu, yaani itavunjika baada ya muda mfupi, but ilimradi ajulikane alishawahi kuolewa, tuache kumchezea Mungu hivyo, si lazima kuoa au kuolewa, waafrika tulifute hili pia, unaweza kuwa na watoto kama familia ya mzazi mmoja au unaweza kuishi kwa kulea watoto yatima kwenye nyumba yako, kama watoto wako wa kuwazaa na kuacha kutumia pesa zako kwa uhuni.
 
1. umri; nasikia ukiwa mzee utakosa msaidizi na life litakuwa gumu ndomana watu husema usipooa uzeeni ni shida
2. uchumi; wengi tunaamini wanawake wanajua kutunza fedha na pia mtu akioa anatulia/matured na anakuwa mtafutaji ili kulisha familia.
ndoa ndoano baba

Chukua hata watoto yatima, wako kwenye vituo mbalimbali, wanatamani sana wazazi na kukaa nyumbani, sio kwenye vituo hivyo, wanatamani sana kuita Baba,Mama, Dada, Kaka, Shangazi n.k, mbona kuna watu wanafanya hivyo, hasa Ulaya, walee kama sehemu ya familia yako kabisa, uwatambulishe kwa ndugu zako, upiganie, uhakikishe, watoto hao na ndugu zako, wanapendana, kujaliana, kuheshimiana na kuthaminiana vizuri, wasomeshe vizuri, wape pia sehemu ya mali yako itakayowafaa maishani, watakutunza mno, we wasomeshe na kuwalea vizuri, hutapata shida uzeeni, watakutunza, usiwe na shaka, wapo watu waliotunzwa na familia za watu wengine, wanazijali sana hizo familia na kuwasomesha watoto au wajukuu wa hizo familia na wanaishi kama ndugu wa damu kabisa, kiasi mtu asiyewajua hataweza kujua kama si ndugu, mpaka mbea amwambie, undugu kufaana, sio kufanana, na akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli, mfaaye, mjali na yeye atakufaa na kukujali uzeeni kama mzazi wake wa kumzaa, Mungu atakuongoza.
 
tayari ninawatoto wawili nilizaa nikiwa chuo....sasa najitegemea na wamekuwa na ninawasomesha wakiwa kwa mama zao ila mama zao ni kitambo sana na wanaendelea na life lao na mmoja anaolewa, sirudi nyuma mimi, naweza nisioe au nikaoa kigoli kipya.
 
Natalie, kuoa au kuolewa kuna sura mbili Yaani ya kwanza kama sehemu ya maisha na pili ni njia pekee iliyokubalika na Imani za dini kukidhi matamanio ya kimwili.

Jibu la swali Lako linategemea unataka tuwe upande gani. Ukisema Upande Wa dini nadhani kiongozi wako Wa Imani atakupa jibu. Ukitaka tujibu Kama jamii bila kuzingatia vitabu vya dini na utaratibu wetu Wa kiafrika basi kuolewa si lazima.
 
sio lazima,hata yesu alikufa bila kuwa na mke wala mtoto,ni maamuzi yako tu
Mh! Nilikua napita tuu ila umenigusa Yesu hakuja kwajili yakuoa alikuja kwajili ya ukombozi wetu, halafu hivi ni kwanini mtu usioe au kuolewa? Inamaana utakua abnomo na unataka uishi vipi kwenye hii dunia au kuzaa na watu mbalimbali mh kwa mtazamo wangu kuoa/kuolewa ni lazima ili uwe nomo na ukubalike kwenye jamii ya dunia hii
 
Ni lazima kwa maana kama uko normal sidhani kama unaweza kujizui kuwaka tamaa. Tafakari halafu chukuwa hatua.....
 
tayari ninawatoto wawili nilizaa nikiwa chuo....sasa najitegemea na wamekuwa na ninawasomesha wakiwa kwa mama zao ila mama zao ni kitambo sana na wanaendelea na life lao na mmoja anaolewa, sirudi nyuma mimi, naweza nisioe au nikaoa kigoli kipya.
nimeshakujua, hahahaha, kumbe wewe ndo yule sio? ukitaka niPM
 
Ni lazima kwa maana kama uko normal sidhani kama unaweza kujizui kuwaka tamaa. Tafakari halafu chukuwa hatua.....

Kama suala ni kujiepusha na tamaa, mbona watu waliopo kwenye ndoa (si wote) hawaishi kurukaruka hovyo??
 
Back
Top Bottom