Hivi Kuna Ulazima Gani wa Kuoa?

Kuna watu hawakuoa, lakini wameuguzwa vizuri tu kwa sababu wameishi vizuri na watu, au wana fedha za kulipia huduma nzuri, au wanajaliwa na ndugu zao.

Kuna wengine walioa, mke/ mume alipojua tu kwamba mwenzake anaumwa na talaka ikaanzia hapo hapo.

Kwa hiyo habari ya kuuguzana si ya msingi katika kuamua kuoa.

Hao watu ni wamatumbi?
 
Kwahiyo hapa unatuaminisha kwamba zamani wote walikuwa ni wacha mungu? mbona magereza yote na mahakama vilijengwa zamani hizo? sikubaliani na wewe hapa unaleta urongo.

Unawaza pua na mdomo ww mmh
 
Sio lazima, ndo maana wengine ni watawa na wanaishi. Hata mtume Paulo alisema mkiishi kama mimi bila kuoa ni vyema zaidi.
 
Kuoa nani?binadamu mwenzako au?maana siku hizi ni jambo la kawaida binadamu kuolewa au kuoa mbwa,paka nifahamishe kidogo
 
mara nyingi ULAZIMA wa kitu huja kutokana na dhana ya WAJIBU, na option huja kama hicho kitu ni HAKI... hivyo kwa maana zote ninazojua mimi (kisheria, kidini, kiserikali, kijamii nk) kuoa si lazima...ni hiari yako LAKINI isiwe sababu ya wewe kwenda kinyume na hali uliyoichagua...mfano kuwa na wapenzi wengi, kuwachezea watoto wa watu, kutembea na wake za watu, kuwaona waliooa ni wajinga..nk... (kwa tathmini inaonesha kuwa vijana wa siku hizi huchelewa kuoa, na wachache hufa bila ya kuoa kutokana na sababu mbalimbali katika changamoto za maisha bila ya wao wenyewe kuzijua na kuchukua hatua kuzifanyia kazi: mfano- uchumi, hali ya kifedha, majukumu ya kazi na masomo nk)
 
Sio lazima, ndo maana wengine ni watawa na wanaishi. Hata mtume Paulo alisema mkiishi kama mimi bila kuoa ni vyema zaidi.
Mkuu kwa Biblia ninayoifahamu mimi aliyesema maneno hayo ni mtume Paulo, maana hata yeye hakuwahi kuoa mwanamke, ndio alisema mkiweza muwe kama mimi, lakini maneno haya nasema mimi, na asemi bwana.

Angalizo: kwa mujibu wa Biblia ukipunguza neno katika maandiko ya Biblia basi na wewe utapunguzia neema zako kwenye mti wa uzima, na ukizidisha neno katika Biblia basi na wewe utazidishiwa mapigo katika siku ya mwisho.
 
mara nyingi ULAZIMA wa kitu huja kutokana na dhana ya WAJIBU, na option huja kama hicho kitu ni HAKI... hivyo kwa maana zote ninazojua mimi (kisheria, kidini, kiserikali, kijamii nk) kuoa si lazima...ni hiari yako LAKINI isiwe sababu ya wewe kwenda kinyume na hali uliyoichagua...mfano kuwa na wapenzi wengi, kuwachezea watoto wa watu, kutembea na wake za watu, kuwaona waliooa ni wajinga..nk... (kwa tathmini inaonesha kuwa vijana wa siku hizi huchelewa kuoa, na wachache hufa bila ya kuoa kutokana na sababu mbalimbali katika changamoto za maisha bila ya wao wenyewe kuzijua na kuchukua hatua kuzifanyia kazi: mfano- uchumi, hali ya kifedha, majukumu ya kazi na masomo nk)

jf never boring
 
Back
Top Bottom