Hivi Kuna Ulazima Gani wa Kuoa?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Wanajamvi,

Naomba mnijuze kwa wale wenye uzoefu na wale ambao bado hamjafanya maamuzi
 
Hakuna ulazima wa kuoa kama utaishinda zinaa ama kama una mpango wa kijisajili kwenye uasherati baada ya kuoa. Manake kuzini ni dhambi.
 
kama hujui umuhimu wa Makalio, jaribu kukalia kichwa...
Hebu subiri uumwe halafu ndio utajua kwamba kuoa ni muhimu au la!
 
kama hujui umuhimu wa Makalio, jaribu kukalia kichwa...
Hebu subiri uumwe halafu ndio utajua kwamba kuoa ni muhimu au la!
Kwahiyo ukiumwa mke ndio anakulipia matibabu fast track pale Muhimbili? au vipi kama mke ndio atakuwa anaumwa!!?
 
wanaosema hakuna ulazima ni vijana wa leo ambao wemekuta wasichana wako wengi na maadili yamewashuka au hawana kabisa,hivyo kutembea na wasichana tofauti tofauti,inge kuwa enzi hizo hili neno usingelisikia,kipindi hicho umpate mwanamke lazima uwe mcha mungu uwe unaenda msikitini au kanisani,vinginevyo utaula wa chuya
 
Kabla ya kujibu swali, inabidi utuambie kuoa ni nini?

Maana mtu anaweza kujibu swali akiwa na fikra tofauti kabisa ya kuoa na unavyofikiri wewe, mkawa mnakubaliana au kupingana huku hata hamjakubaliana kwamba mnaongelea kitu kimoja au vitu tofauti.

Mathalani, je, unahesabu mwanamme na mwanamke kukaa pamoja bila kushirikisha mipango ya kidini , kimila au kiserikali kwamba ni kuoa? Wengine wanasema huku ni kuoa (common law marriage) wengine wanasema si kuoa.

Na kama unakubali huku ni kuoa, mtu akae na mwenzake kwa muda gani ili wahesabike wako katika ndoa? Nini tofauti ya girlfriend, mchumba na mke wa "common law marriage"

Kuna maswali mengi kama hayo inabidi kujibu kwanza.

Mie naweza kusema kuoa si lazima, kumbe naongelea kuoa kiserikali na kidini, na siongelei common law marriage.

Umenipata hapo?
 
.....Hili swali ni sawa na kuuliza je kuna ulazima wa kufanya mapenzi?
 
Kilakitu kinakuwa na umuhmu pale kinapohtajika, kwahyo binafsi naweza sema ULAZIMA UPO au HAUPO inategemeana na wakati na mazingira alionayo mtt.
 
WaDUvi

Mnaendelea kunigusa, naomba tu muogelee katika maana yoyote, iwe ni kwa statutory interpretation, customary rituals, au under religious norms............hapa pia nieleweke kwamba sijaamanisha kufanya tendo la ndoa nimeuliza kuoa na unaweza nogesha kuolewa ikiwa ni lazima au la!! mkitupa uzoefu (visa mkasa) itasaidia sana
 
wanaosema hakuna ulazima ni vijana wa leo ambao wemekuta wasichana wako wengi na maadili yamewashuka au hawana kabisa,hivyo kutembea na wasichana tofauti tofauti,inge kuwa enzi hizo hili neno usingelisikia,kipindi hicho umpate mwanamke lazima uwe mcha mungu uwe unaenda msikitini au kanisani,vinginevyo utaula wa chuya
Kwahiyo hapa unatuaminisha kwamba zamani wote walikuwa ni wacha mungu? mbona magereza yote na mahakama vilijengwa zamani hizo? sikubaliani na wewe hapa unaleta urongo.
 
WaDUvi

Mnaendelea kunigusa, naomba tu muogelee katika maana yoyote, iwe ni kwa statutory interpretation, customary rituals, au under religious norms............hapa pia nieleweke kwamba sijaamanisha kufanya tendo la ndoa nimeuliza kuoa na unaweza nogesha kuolewa ikiwa ni lazima au la!! mkitupa uzoefu (visa mkasa) itasaidia sana

Kuoa si lazima, kama mtu hutaki kuoa kwa nini kuoa kuwe lazima?
 
kama hujui umuhimu wa Makalio, jaribu kukalia kichwa...
Hebu subiri uumwe halafu ndio utajua kwamba kuoa ni muhimu au la!

Kuna watu hawakuoa, lakini wameuguzwa vizuri tu kwa sababu wameishi vizuri na watu, au wana fedha za kulipia huduma nzuri, au wanajaliwa na ndugu zao.

Kuna wengine walioa, mke/ mume alipojua tu kwamba mwenzake anaumwa na talaka ikaanzia hapo hapo.

Kwa hiyo habari ya kuuguzana si ya msingi katika kuamua kuoa.
 
Back
Top Bottom