Makame
JF-Expert Member
- Jan 3, 2008
- 512
- 60
Nauliza hili kwa sababu zifuatazo:-
1. Baada ya Uchaguzi wa 2010, Mheshimiwa Rais alichukua muda mrefu kabla hajatangaza Baraza la Mawaziri; katika kipindi ambacho tulikuwa hatuna mawaziri, Nchi ilizama? Ilididimia? Iliganda? Mawaziri wanakula tu.
2. Kwa Mawaziri wanaotuhumiwa, walishawahi kukutana na kamati za bunge husika; wakaambiwa na hawakuchukua hatua kurekebisha dosari husika. Sasa kama Mawaziri wanaelezewa dosari kinaga ubaga, na hawajachukua hatua; kuna haja kweli ya kuwa nao????
3. Taarifa ya CAG kabla haijawasilishwa Bungeni ina mikondo yake inayopitia; na kama CAG amekuwa akiripoti kila mwaka; na Mawaziri wanayawacha mulemule ndani ya mjengo kama vile CAG alikwenda kuwatumbuiza; Mawaziri hawawajibiki, mpaka kelele zipigwe na wabunge; kweli kuna haja ya kuwa nao?
Wana JF, hizo ni fikra ; leteni mawazo yenu