Hivi Kuna sababu za kupeana Talaka!!!Elewa biblia kuhusu Talaka!!!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakajikuta swali lao limekosewa! Ni kweli zogo (controversy) au hekaheka kubwa inayowagawa watu katika makundi mawili kuhusu talaka inapatikana katika injili ya Mathayo 5:32 na 19:9
Kumbuka Injili ya Luka na Marko pia imeripoti tukio la Mathayo 19:9 Yesu alipotegwa swali na Mafarisayo isipokuwa ni Mathayo peke yake ameandika kuhusu exception ya kutoa talaka ambayo ni kosa la uasherati (tutaangalia baadae kwa nini ni mathayo peke yake ameripoti hivyo).

Kabla ya kufika huko ni Muhimu sana kufahamu mazingira (geography) iliyopelekea Yesu kuulizwa swali na Mafarisayo.
Tukumbuke kwamba Yesu alikuwa Galilaya na alikuwa amemaliza huduma yake na sasa alikuwa anasafiri kupitia eneo la Perea ili kurudi Yerusalemu kwa ajili ya pasaka (yaani kifo chake).

Mafarisayo waligundua kiwamba Yesu atapita hilo eneo ambalo kwa wakati huo lilikuwa chini ya himaya ya Herodi.
Hivyo mafarisayo walijua ni wakati muafaka wa kumuuliza swali (trick question) ili ajichanganye na wapate sababu ya kumuua.
(kumbuka mafarisayo walikuwa wanamfafuta sana Yesu wamuue ila walikosa sababu au shitaka Mathayo 12:14, Marko 3:6)
Kwa hiyo mafarisayo walimuuliza Yesu swali ambalo lengo ni kumtega yeye (test) na si kutaka kujua.

Kumbuka miaka 2 iliyopita Yohana mbatizaji ambaye alimtangulia Yesu alikuwa amefungwa Jela kwa sababu aliongelea suala la talaka ya Herode Antipas ambaye alioa mke wa mdogo wake Filipo ambaye mke wake alitoa talaka kwa mume wake Filipo na kwenda kuolewa na Herodi Antipas (kaka mtu) Soma Mathayo 14:1-12.

Yohana mbatizaji hakubabaika au kujisikia vibaya kumkemea Herodi na dhambi yake hata kama ni ikulu (Math 14:4) matokeo yake akawa arrested na kutupwa jela na baadae kukatwa kichwa.

Kwa kuwa Yesu alikuwa anapita maeneo ambayo ni himaya ya herodi Antipas, mafarisayo walijua fika kwamba Yesu atajichanganya tu na jibu la swali watakaloulizwa na atajimaliza kwa kumtaja Herode na dhambi yake ya kuoa mke wa mdogo wake na kama Yohana mbatizaji kwa kutamka tu aliuawa Yesu Je ambaye anapita kwenye himaya yake?

Swali aliloulizwa Yesu lilikuwa:
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’

Kumbuka wakati Yesu yupo duniani talaka ilikuwa inakubalika kutokana na Musa alivyoamuru hata hivyo kulikuwa na gumzo na utata wa sababu ipi hasa mume anaweza kutoa talaka kwa mke au sababu ipi hasa inaweza kupelekea mume kutoa talaka kwa mke wake na kumbuka pia wayahudi walikuwa hawaruhusu mwanamke kutoa talaka bali mwanaume tu.

Ndipo kukawa na makundi matatu yanayopingana

KUNDI LA KWANZA – SHAMMAI
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ilikuwa ni uzinzi (adultery)

KUNDI LA PILI – HILLEL
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ni pale mke akipika chakula kisichoiiva au kibaya au ovyo.

KUNDI LA TATU – RABBI
Wao walikubalkiana kwamba hata mume akikutana na mwanamke mzuri zaidi ya Yule anaye nyumbani basi anaweza kutoa talaka

Sasa swali kwa Yesu lilikuwa wewe upo upande gani?
SHAMMAI, HILLEL AU RABBI?

Yesu alifahamu fika mioyo ya mafarisayo inawaza kitu gani na akawajibu kwa swali (counter attack) kwa kuwauliza tangu mwanzo Mungu alifanya kitu gani kwa ajili ya mke na mume.

Mafarisayo wakajikuta swali lao limekosewa na kwamba wamekosa point kwani wao walitaka ajibu Kumbukumbu la Torati 24:1-4) na Yeye akajibu Mwanzo 2:24.

Ikabidi wamrukie kwa swali kuhusu Musa kuruhusu talaka ndipo wakajibiwa kwamba Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kukataa kwao design ya ndoa tangu mwanzo na ndipo Yesu akazusha mambo 4 muhimu kabisa

JAMBO LA KWANZA
Hapo mwanzo Mungu aliumuumba mwanaume mmoja kwa ajili ya mwanamke mmoja, kama angetaka Adamu awe na wanawake wengi basi angewaumba akina Sandra, Joan, Jane, Linda wakutosha na si Eva peke yake.
(mwanzo 1:27, 5:2, Marko 10:16)

JAMBO LA PILI
Yesu anatia mkazo kwamba ndoa ndicho kifungo (strongest bond) duniani hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa ni muhimu sana anayehusika kufahamu kwamba anaingia kwenye kitu ambacho huwezi kutoka labda kifo kitokee kati ya wawili.
(Mwanzo 2:24, Marko 10:7)

JAMBO LA TATU
Katika ndoa wawili huwa mtu mmoja, mwili mmoja (one flesh)
(Mwanzo 2:24, Marko 10:8)

JAMBO LA NNE
Yesu alithibitisha kwamba Mungu ndiye huwaunganisha wawili wanaooana na kwamba kile Mungu amekitenganisha binadamu asikitenganishe.

Hivyo swali la mafarisayo
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
Jibu la Yesu ni HAPANA KUBWA
Na kwamba Yesu hakuwa kwenye kundi lolote iwe SHAMMAI AU HILLEL AU RABBI.

Yesu alielezea kudumu (permanency) na kutovunjika (inviolability) ya ndoa hadi wanafunzi wakaendelea kumuuliza jioni yake huku wakipendeleza kwamba kama masuala ya ndoa ni hivyo basi ni busara sana mwanaume asioe kabisa.
 
Hii nadharia tu Kiongozi,

Haya mambo waumini wamefundishwa sana - Kuna kitabu pale Msimbazi Centre kimeongelea sana haya mambo ya Talaka - in details::: Lakini usishangae kitakwimu nusu ya ndoa za Kikristu wameshatalikiana tena kwa viapo!

Old rules of the game (!) are no longer relevant (!)
 
Hii ipo kinadharia na kiimani zaidi kwenye vitendo kuna ugumu kutekelezeka!
 
Back
Top Bottom