Hivi kuna sababu gani za kupost/kuweka picha za watoto wetu mitandaoni?

Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

Watu kujinafasi na watoto wao ruksa.

Hata mtu akisema mwanawe ana akiki sana wakati ni wazi mtoto ni tutusa ni ruksa.

Ukimind unaweza kuwa mchawi.
 
Mambo ya Ngoswe, muachie Ngiswe mwenyewe.

Watu kujinafasi na watoto wao ruksa.

Hata mtu akisema mwanawe ana akiki sana wakati ni wazi mtoto ni tutusa ni ruksa.

Ukimind unaweza kuwa mchawi.

huo ni ushamba mkubwa! tena ushamba wa kisukuma
 
Ushamba ni upi?

Ushamba wa Kisukuma ninaoujua mimi anao Magufuli.

Anawaambia polisi waibe matairi ya magari ya raia halafu wakiulizwa gari limefikaje polisi wajibu gari limekuja bila matairi.
 
sirjohn wamekuelewa ni ujinga mtupu muache mtoto akue afu yeye ndo ataamua kufungua ac na yeye auze uze kdogo, ndo mana nachukia fb mimi ndo yale yale mtu anapiga picha miguu yake afu like 700 ,
 
Hii ni mada njema kwa wazazi wa dotcom. Ukiachilia mbali suala la faragha ya mtoto, ambayo ni haki yake mwenyewe kuamua na sio kuamuliwa na wazazi, pia kuna suala la usalama wa mtoto. Kwa kuweka picha ya mtoto kwenye mtandao, watu wanaweza kujua hali yako ya kipato na pia na hata kumtamani mtoto. Matokeo yake kuna kutapeliwa kwasababu ya taarifa ya mtoto wako mtandaoni, kutekwa kwa mtoto na kutakiwa kutoa pesa.

Lakini baya zaidi ambalo lipo njiani (kama bado halijaanza) ni dhuluma za kingono kwa watoto (pedophilia). Mabadhadhi wanaweza kumtaman mtoto wako kutokana na picha uliyoweka na hatimae kumtafuta na kumfanyia dhuluma. Kwa nchi zilizoendelea kwa TEHAMA kama India ambazo wazazi wanamudu kuwanunulia watoto wao kompyuta zilizounganishwa kwenye mtandao, mambo haya hutokea sana. Kwa taarifa tu, India inaongoza kwa utumwa wa kimapenzi na usafirishaji wa watoto wadogo. Mwanao atatafutwa facebook na jitu linalojifanya nalo ni toto, na bila wasiwasi wowote, mtoto atatoa taarifa za kazi na ratiba na mama na baba ni hivyo kufahamika wakat gani haupo nyumban. Sasa hapo linabaki suala la mtoto kuambiwa njoo hapa barabarani nikununulie icecream au baga. Huo waweza kuwa mwisho wa mtoto kumuona. Pia South Afrika kuna tatizo kubwa sana la watoto kupotea-tehama ni moja ya sababu.

Pia kuna wazazi wanawapiga watoto picha uchi na kutumia ndugu au mume/mke whatsup. Uchi ni uchi tu hata uwe wa mtoto. Sidhani mzazi unapenda mtoto wako aje awe bullied shuleni sababu ya maumbile yake ya siri. Kwa taarifa tu, mara nyingi smartphone yako huhifadhi kwenye mtandao picha zote unazopiga au kutumiwa (mfano huhifadhiwa kwenye mtandao wa photos), hivyo hata ukifuta kwenye simu, hujafuta sehemu nyingine kwenye mtandao. Hackers wanaweza kufanya lolote, wakati wowote na picha zako zilizoko kwenye mtandao wa photo. Jihadhari, umeonywa.
 
asante kwa shule nzuri! wataelewa tu
 
asante kwa shule nzuri! wataelewa tu
Binafsi napenda sana privacy. Na nina training ya computer security. Kwa hiyo naelewa matatizo yote hayo yaliyotajwa ya security.

Nini picha ya mtoto. Ile kuwa na page FB tu halafu watu wakaja kukupongeza "Happy birthday" ni security risk. Birthday ni PII.

Tuache kusheherekea birthday kwenye social media?

Lakini, kuna watu wanajua yote hayo lakini hisia zao za kibinadamu ni kujivunia wana wao. Na kuna wengi tu wamefanya hivyo kwa muda na hakuna lolote lililotokea.

Bottom line watu wana haki ya kuishi wanavyotaka ili mradi hawavunji sheria.

Mimi binafsi napenda privacy. Kwa sababu hiyo nawapa privacy yao hata wale wasioheshimu privacy.

Kuwafuatilia sana kunaweza kuzua maswali kwa huyo anayefuatilia.

Je, anakuwa paranoid?

Je, ana wivu?

Je, akipotezea tu na kukubali kwamba binadamu wote hatuwezi kupenda vitu vile vile atapoteza nini?

Je, wengine wakisema kwamba yeye anawaficha watoto wake kwa sababu si wazuri atajisikiaje?

Je, watu wengine wakijivika ujuzi wa kujua kuwalea watoto wake kuliko anavyonua yeye ataonaje?
 
mimi naona nibora kuliko mama mwenye watoto kupost picha yake kwenye mitandao ya kijamaa akiwa na chupi au wale wanaocheza chura bira chup mtoto anajifunza nn ni mara mia umpost mtoto
 
juvenile davis huna mtoto wewe unalea watoto wa wenzako una upload picha wenye watoto wao wanatia like tu ,kama huamin angalia waliogonga like wote kama hakuna anaefananana na hao unaosema watoto wako
 
somo zuri sana!!!! utasikia kama kaenda kununua shoes za mtot mliman city ili watu wajue kuwa kanunulia pale utaskia hapohapo anamfotoa akiwa kajaribu anarusha fb, inst, whtp n.K utaskia ma angle agrysh!! si ulimbuken huO jaman mbona hawapigag Na kupost wakiwa wamefilicka???

Wivu ni Maradhi
 
Back
Top Bottom