Hivi kuna mvumbuzi au scientist yeyote mweusi?

ogm12000

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
304
86
Hivi kuna mvumbuzi au scientist wa nguvu like elbet eistern, Galileo, Isaac newton, Kekule, Kalman , sharpov, n.k ambaye ni black?

Kama yupo anaitwa nani na alifanya nini?

Kama hakuna ni kwanini ?

NB: Ni swali tu ktk kutaka kujua.
 
yupo........... tena wapo wengi kidogo..........................

mwalimu julius nyerere alivumbua mwenge wa uhuru na falsafa yake.................

Dr jakaya kikwete alivumbua falsafa ya ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya............

nk.nk.
 
kazi kweli kweli...
 
wapo wavumbuzi
mmoja wapo ni mwanasayansi aliyegundua maji ya mto yanawai kuganda kuliko ya baridi.
tena huyo ni mtanzania. tujivunie kwa hilo
 
Pia nami napenda kujua wanasayansi wagunduzi ambao sio wayahudi au wenye damu ya kiyahudi. Leteni hapa ufahamu wenu
 
Kama hakuna mweusi,vile mchina na mhindi.
Lakini kila mtu anajua wazungu walianza na kuchangamka mapema kwa ugangster wao.
Angalia Spanish walivyokwenda america,Wareno walipowasili Brazil na British walivyotufanya.

Lakini kila mzungu anajua Mchina na Mhindi wanakwenda kasi,hawa hawana uvumbuzi mkubwa mpaka sasa.Lakini wameweza kucopy kiasi kikubwa mpaka mzungu anaogopa.
labda sisi tumgeweza kutumia resources zetu vizuri kubuy into status.Angalia waarabu wenye mafua ,UAE hawajangua kitu ,lakini wamejitahidi kutumia resources vizuri.
 
Wait wait wait,

Mchina na Mhindi hawana uvumbuzi mkubwa mpaka sasa? Kabla ya wazungu kusoma vitabu vya wahindi hawakuwa na symbol ya 0, jaribu kuhesabu from 1 to 100 bila kutumia 0 uone kazi.

Unajua nani kaleta the revolutionary concept of 0 in mathematics?

Unajua nani kavumbua the use of gunpowder? Unajua kwa nini visosi vinaitwa "China"? Unajua wakati wazungu wanakula chochote walichokipata wahindi walishajua mambo ya balanced food? Unajua wakati Pythagoras na wenzake wanahangaika kubishana kuhusu philosophy lord Budha alikuwa kashatoa maandiko mengi tu muhimu kabla yao? Unajua vitu vingi vilivyokuwa "vinavumbuliwa" Ulaya wakati wa enzi za renaissance vilikuwa vishasahauliwa huko China/ India? Unajua kwamba wakati Wajerumani wanasherehekea the first printing press (Guttenberg) wahindi walisha invent block printing tangu mwaka 888 na actually ku print "The Diamond Sutra" a buddhist text?

Fanya research kabla ya kuandika mazee.
 
mkuu, katika kipindi hao uliwataja walikuwa wanafanya uvumbuzi, watu weusi kwa ujumla walikuwa na matatizo chungu nzima kama Slavery, Ukoloni, nk. Pia, Africa (sio pwani) kwa miaka mingi haina mawasiliano yeyote na dunia nzima, kwahiyo uvumbuzi wowote ulikuwepo lazima haukuweza kufahamika. Pia tamaduni ya nchi nyingi za africa hazikuwa na maandishi. Kwahiyo, record-keeping yeyote ilikuwa kwa mdomo. Kwahiyo historia yeyote ilikuwa skewed based on the loyalty of the communicator.

Kwahiyo hatuwezi fahamu kwa uhakika ni uvumbuzi gani ulifanywa na "wanasayansi" wetu. Uvumbuzi wowote ambao ungefanywa na watu weusi ni ili kukabiliana na maisha katika civilization zao. Binafsi ninadhani kuna teknolojia kadhaa tulizokuwa nazo kule kijijini kwetu ambazo kwa mantiki ya maisha na mazingira ya kule, ilikuwa ni uvumbuzi safi tu. mfano, mtu akigongwa na nyoka huwa walikuwa wanakupa aina fulani ya jiwe ambalo linanyonya sumu katika kidonda. (soma zaidi http://en.wikipedia.org/wiki/Snake-stones). Hii imekuwa ikitumika kijijini kwa miaka nenda rudi, na ninadhani ilivumbuliwa independently from other world civilisations. Teknolojia nyingine nyingi zilikuwa labelled as "uchawi" by the so called missionaries.

Kwa haraka haraka, majina mashuhuri ya wanasayansi na wavumbuzi wanaofahamika na ni weusi ni kama:
http://en.wikipedia.org/wiki/Arthur_Lewis_(economist)
[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Ronald_Mallett[/ame]
[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Vivien_Thomas[/ame]
[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Ben_Carson[/ame]
 
Hivi kuna mvumbuzi au scientist wa nguvu like elbet eistern, Galileo, Isaac newton, Kekule, Kalman , sharpov, n.k ambaye ni black?

Kama yupo anaitwa nani na alifanya nini?

Kama hakuna ni kwanini ?

NB: Ni swali tu ktk kutaka kujua.

Ameuliza scientist sio mwanafalsafa, nyani jibu hapa!
 
Tatizo ni kwamba, tushagubikwa katika utamaduni wa kimagharibi so much sasa hivi hata hatujijui.

Hii concept nzima ya mtu mmoja kuchukua credit kwa uvumbuzi ni ya kimagharibi, huku kwetu watu walikuwa wakivumbua kitu kinapelekwa kwa chief, kinatumika, hamna emphasis kwa individual.

Ndiyo maana wagiriki walivyoenda Masr na kukuta kuna ilmu kibao ambayo haijaandikwa wavumbuzi ni kina nani, wakawahi ku publish na kujisema wao ndio wavumbuzi.Zama zile sana sana Masr ukijitia kujitangaza kwamba wewe ni mvumbuzi Farao atakutangaza wewe kama heretic na kukuchinjilia mbali.Hapa ndipo tulipokosea Waafrika, badala ya ku cultivate freedom of thought and invention sisi tuli cultivate tyranny - not that Europe did not do the same, it just happenned that Greece was at the helm of it's philosophical experiments with the ideas of freedom and democracy-

Kwa hiyo hata hao kina Pythagoras wanavyosema wamevumbua Pythagoras theorem, kina Archimedes walivyosema kwamba wamegundua Archimedes principle, na kina Erasthothenes wanavyosema waliweza kupima mzingon wa dunia kwa usahihi, chances are Wamisri walishafanya haya, au worse still, hawa wagiriki walikwenda kuiba hii knowledge hapo Masr kama inavyojadiliwa katika kitabu "The African Origins of Greek Philosophy".
 
Hivi kuna mvumbuzi au scientist wa nguvu like elbet eistern, Galileo, Isaac newton, Kekule, Kalman , sharpov, n.k ambaye ni black?

Kama yupo anaitwa nani na alifanya nini?

Kama hakuna ni kwanini ?

NB: Ni swali tu ktk kutaka kujua.

Chenge alievumbua mambo ya rada
gavana Balali aliekula hela ya EPA...
Mkapa alievumbua uuzazi wa nyumba za serikali na hiyo ni record hakuna ataeivumbua...
ni wengi tuuu mkuuu
 
mkuu, katika kipindi hao uliwataja walikuwa wanafanya uvumbuzi, watu weusi kwa ujumla walikuwa na matatizo chungu nzima kama Slavery, Ukoloni, nk. Pia, Africa (sio pwani) kwa miaka mingi haina mawasiliano yeyote na dunia nzima, kwahiyo uvumbuzi wowote ulikuwepo lazima haukuweza kufahamika. Pia tamaduni ya nchi nyingi za africa hazikuwa na maandishi. Kwahiyo, record-keeping yeyote ilikuwa kwa mdomo. Kwahiyo historia yeyote ilikuwa skewed based on the loyalty of the communicator.

Kwahiyo hatuwezi fahamu kwa uhakika ni uvumbuzi gani ulifanywa na "wanasayansi" wetu. Uvumbuzi wowote ambao ungefanywa na watu weusi ni ili kukabiliana na maisha katika civilization zao. Binafsi ninadhani kuna teknolojia kadhaa tulizokuwa nazo kule kijijini kwetu ambazo kwa mantiki ya maisha na mazingira ya kule, ilikuwa ni uvumbuzi safi tu. mfano, mtu akigongwa na nyoka huwa walikuwa wanakupa aina fulani ya jiwe ambalo linanyonya sumu katika kidonda. (soma zaidi http://en.wikipedia.org/wiki/Snake-stones). Hii imekuwa ikitumika kijijini kwa miaka nenda rudi, na ninadhani ilivumbuliwa independently from other world civilisations. Teknolojia nyingine nyingi zilikuwa labelled as "uchawi" by the so called missionaries.

Kwa haraka haraka, majina mashuhuri ya wanasayansi na wavumbuzi wanaofahamika na ni weusi ni kama:
http://en.wikipedia.org/wiki/Arthur_Lewis_(economist)
http://en.wikipedia.org/wiki/Ronald_Mallett
http://en.wikipedia.org/wiki/Vivien_Thomas
http://en.wikipedia.org/wiki/Ben_Carson

Nimependa hiyo picha yako ya huyo mchumi mkali sana Rweyemamu..

Waafrika, tena weusi, wamegundua vitu vingi sana kuanzia vitu ambavyo bila hivyo, basi dunia ya sasa isingekuwa kama ilivyo.

-Alphabet, tunayoitumia sasa hivi, iligunduliwa Misri ya zamani(Kemet).

-Pythagoras theorem ilivumbuliwa na Wamisri 2000bc kabla hata wagiriki 'kugundua' mnamo 400bc. inasemekana wagiriki walicopy kutoka kwa waafrika hawa weusi.(Na wanakubari hili kwenye maandishi yao).Ukisoma Kahun papyrus inakuonyesha kwa maandishi yao wenyewe pythagors theorem ya wamisri.

-Ni waafrika tena weusi wa misri waliogundua calender , na calendar yao ilikuwa ina siku 365 kama calendar tunayoitumiaa sasa hivi.

Piramidi za Nubia na misri ni precision surveying za kwanza duniani majengo haya yalijengwa kwa ujuzi mkubwa(miaka 4500) iliyopit kiasi cha kwamba mpaka sasa bado yapo.

Hizi ni baadhi ya old inventions za waafrika.
 
Vivien T. Thomas, L.L.D.

Supervisor of
Surgical Research Laboratories
1910 - 1985

Gonga hapa for more info.​
 
Mtanzania anaitwa Mpemba aligundua Mpemba Effect. Unaweza kuisoma kwenye wikipedia.
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=xOVZV6DxaRs[/ame]

Wazimbabwe walijenga nyumba za mawe zamani sana. Na hii ndiyo maana ya Zimbwbwe yaani iZumba Lya Mabwe au jumba la mawe.

Muulize mtu wa Bangladesh atakuambia kuwa ile helcopter ya USA iitwayo Apache, umeshsuhwa na mtu wa kwao aishiye USA.

Wenyeji wa Mali walisherehekea sana chombo cha Pathfinder (kilichopelekwa Mars) kwani mtengenezaji alikuwa Mmali.

Wafipa waligundua Blast furnace za kuyeyushia vyuma. Watu wa West Africa waligundua mashine za kutengeneza vitambaa kwa kutumia nyuzi za pamba.

Mtanzania mwingine huyu hapa hata hafahamiki hadi anajitangaza kwenye Youtube. Pia kumbukeni ugunduzi wa Dr. John Pombe Magufuli. Nyingine angalieni kwenye Youtube.
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=p-FAg2hcuFA[/ame]
 
Nimependa hiyo picha yako ya huyo mchumi mkali sana Rweyemamu..

Waafrika, tena weusi, wamegundua vitu vingi sana kuanzia vitu ambavyo bila hivyo, basi dunia ya sasa isingekuwa kama ilivyo.

-Alphabet, tunayoitumia sasa hivi, iligunduliwa Misri ya zamani(Kemet).

-Pythagoras theorem ilivumbuliwa na Wamisri 2000bc kabla hata wagiriki 'kugundua' mnamo 400bc. inasemekana wagiriki walicopy kutoka kwa waafrika hawa weusi.(Na wanakubari hili kwenye maandishi yao).Ukisoma Kahun papyrus inakuonyesha kwa maandishi yao wenyewe pythagors theorem ya wamisri.

-Ni waafrika tena weusi wa misri waliogundua calender , na calendar yao ilikuwa ina siku 365 kama calendar tunayoitumiaa sasa hivi.

Piramidi za Nubia na misri ni precision surveying za kwanza duniani majengo haya yalijengwa kwa ujuzi mkubwa(miaka 4500) iliyopit kiasi cha kwamba mpaka sasa bado yapo.

Hizi ni baadhi ya old inventions za waafrika.

Mazee umeongezea uzito na specifics kwa post yangu # 12 hapo juu.
 
Dr. Alex Paurine. Mangi huyu hapooo UK.......

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=Lp7mgLZxt_M&feature=related[/ame]
 
Dr. Phillip Emeagwali, Mnigeria ambaye aliwashangaza hadi Wajapan/USA na hizo Super Computer. Anaitwa The father of Internet na hadi sasa tunavyotumia, tunatumia matunda ya jamaa. Haya majaribio ya Super Computer iliyojengwa Europe union, wanatumia ujanja wa jamaa wa kutumia Computers nyingi zikiwa zimeungwa pamoja....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=0M_lwAEgUYU[/ame]

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=JFXBOv5QvVs&feature=related[/ame]
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom