Hivi kujua lugha ya kiingereza ndiyo usomi Tanzania?

kujua kingereza si kigezo kuonekana msomi. hapa tanzania kuna wasomi waliomaliza vyuo vikuu na bado hawajui kingereza wanaongea lugha mbadala kama kiaarabu kigermany au kifaransa badala ya kingereza
 
Kaka wakati tunaendelea na majadiliano kasome english course ili uwe fit pale british council maana utakosa kazi kweli atiii.
Hatuna kitu, vile tulivyonavyo si vyetu wamepewa wenye lugha zao atakutaka nini tena wewe? kama ni mgodi anao yeye wewe aje kwako kufanya nini mpaka ajue english. inabidi tujifunze ili tuombe vibarua. China na ufaransa na nchi zingine hawamtegemei mtu kwenye uchumi wao.

Umeongea la msingi sana hapo, nilipita ugerumani na ufaransa yaani lugha zao kama hujui utahangaika na wanajivunia kweli.
Uchumi unachangia huoni Zimbabwe wanajifunza kiswahili ili waje kutafuta ajira huku wakichangia na lugha ya kiingereza wanaoijua zaidi
 
mheshimiwa MPOGORO,MZIZI WA MBUYU.....
mimi naomba kuuliza swali,
mtu unasoma kuanzia form 1 hadi university(miaka 9+ ) kwa kutumia kiingereza kwa masomo yote(kasoro ya lugha nyingine) halafu unamaliza chuo kikuu una degree hujui kiingereza katika hali ya kawaida mtamuelewa vipi huyo mtu?
NB:huko china/russia etc hawatumii kiingereza kama sisi wanatumia lugha zao kwenye kila kitu hivyo huwezi kuhoji ukikuta watu wao hawajui kiingereza.

kwa maoni yangu huwezi kutenganisha kiingereza na usomi tanzania hadi tutumie kiswahili kama lugha ya kufundishia hadi chuo kikuu.

ujue mtoto wa miaka saba tena aliye jifunza kiswahili kama lugha mama umpe miaka 9 Kujifunza kingereza kila siku ndani ya masaa8 akirudi nyumbani anazungumza kiswahili au lugha ya kabila lake unadhani itakua rahisi kukijua hiki kingereza??
 
Back
Top Bottom