Hivi kujiita Mtanganyika ni kosa?

Haki ya MUNGU Watanganyika lazima tubadilike na kuitukuza Tanganyika yetu. Wazanibar wametupiga bao wanajitambulisha kwa uzanibari na upemba. Mi mzanzibar mi mpemba .Sisi watanzania mpaka ukakasi mi MTANGANYIKA. TAFAKARI BADILIKA CHUKUA HATUA .Jivunie Utanganyika wako

Nimekusoma mwana... My Tanganyika!
 
Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?
......ole wao wanaojiita watanzania, maana mimi nikiangalia mbele siioni Tanzania zaidi ya Tanganyika na Zanzibar, akah! mi mtanganyika yakhe!
 
Kuna yale maonyesho ambayo hufanyika Zanzibar kila mwaka, waandaaji kwa kukosa fedha za kuendeshea wakaamua wayahamishie huku "Tanzania bara". Nikamsikia Maalim Seif Sharrif Hamad (Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar) akikataa na hapa namnukuu "Mimi siafiki maonyesho haya kupelekwa Tanganyika". Kwa kiongozi mkubwa hivyo kusema hayo, basi hata wao wanaijua. Ndo maana mimi sipendi siasa ni KIGEUGEU.
 
Samahani na pole kwa kum- overestimate maalim. Ulivyomdhania sivyo alivyo kabisaaaa... Kifupi yule ni mchumia tumbo!
 
Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?

LOL. Wewe dogo haujatulia:)

Ningekuwa nakulipia mimi school fees ningeku-ground, hahaha!

Anyway, alimradi ulitaka kuburudisha kidogo, mbona haukutumia jina la kwanza kabisa la hii nchi, yaani German East Africa! Au Deutsch-Ostafrika.

I hope unajua kuwa hii nchi iliundwa na waJerumani na baadaye kupewa jina la Tanganyika na waIngereza walipowashinda waJerumani katika vita ya kwanza ya dunia. Infwakti baba wa taifa wa kikwelii ni Karl Peters na siyo Kambarage!
 
duh! Umenifumbua macho, ila katika Deustche Ostafrika watu hawakuwa huru kama ilivyo sasa. Ni vigumu kutaja kama nchi yetu. Karl Peters hawezi kuwa baba wa taifa kwa kuwa alikuwa akisimamia matakwa ya Udachi na Wadachi, Nyerere anastahili kwa kuwa alikuwa pale kwa maslahi ya nchi na wananchi.
 
Dawa ni ndogo tu, raia wote tunaotatizwa na kiinimacho cha muungano tukomae kuiita nchi yetu kwa jina la Tanganyika, asiyetaka litumike akaue kwanza lile la Zanzibar (kitu ambacho hakiwezekani) kusubiri watawala wezi walitumie jina hilo ni ndoto za mchana. Angalia post zangu humu mara nyingi naiita nchi hii Tanganyika na raia wake watanganyika... Inaonyesha wengine wanasubiri hisani ya watu wa Marekani ndo waanze kulitumia!
 
mbona wazanzibar hawajiiti watanzania visiwani? wanajiita wazanzibar, wana kila kitu mpaka bendera ya zanzibar, benki na vinginevyo mbona hawaviiti jina la tanzania visiwani? mi pia ni mtanaganyika pureeee
 
duh! Umenifumbua macho, ila katika Deustche Ostafrika watu hawakuwa huru kama ilivyo sasa. Ni vigumu kutaja kama nchi yetu. Karl Peters hawezi kuwa baba wa taifa kwa kuwa alikuwa akisimamia matakwa ya Udachi na Wadachi, Nyerere anastahili kwa kuwa alikuwa pale kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Kabla ya Karl Peters kulikuwa hakuna nchi inaitwa Tanganyika, Tanzania wala Deutsche Ostafrika. Yale mikataba hewa aliyoingia nayo Karl Peters na wale machifu ndiyo yalijenga hili taifa.

Kabla ya hapo kulikuwa kuna vijikabila vilvyokuwa vinatawaliwa kitemi na machifu. Nchi ilikuwa inarindima na vita vya kikabila kwa ajili ya kukamata watumwa. Akina Mirambo, kwa mfano, walikuwa ni majambazi makatili yaliyotesa sana makabila ya kanda ya Ziwa. Wamasai walitesa sana Kaskazini. Wahehe nao walipiga bakora makabila yaliyowazunguka.

Kwa ujumla, ilikuwa ni vurugu mechi. Maisha yalikuwa na thamani ndogo sana wakati huo. Mtu anaweza akatolewa kafara hivi hivi live mnamuona.

Vile vile, usifikiri tulikuwa tumeendelea saaaana kabla ya hawa Wakoloni kuja. Kulikuwa hamna hospitali, barabara wala shule za kata. Hata gurudumu tulikuwa hatujagundua.

Ni vizuri tukajua tulipotoka ili tuweze kujua tuendako.
 
[h=1][/h]Written by Hassan10 // 25/11/2011 // Habari // 3 Comments

Mphamvu(Mtanganyika)

Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?
jamiiforums newspape

[h=4]Related Posts[/h][h=3]BARUA YA WAZI KWA WALA UROJOBARUA YA WAZI KWA WAZANZIBAR KUTAKA KUTAMBULIWA KWA DISEMBA 10-12.1963 KUWA NI SIKU RASMI YA UHURU WA ZANZIBAR[/h]
[h=3]Mh Aboubakar (Waziri wa sheria Z’bar) asema wananchi itumieni fursa hii muliopata ili kutowa dukuduku zenu na maoni yenu.[/h]
[h=3]SMZ yaitupia Serikali ya Muungano gharama za Katiba Mpya[/h]

[h=3]mapinduzi zanzibar 1964[/h]
[h=3]Maalim Seif aikabidhi leseni Star Times aitaka kuandaa vipindi vizuri[/h]

[h=3]3 Comments on "Hivi kujiita Mtanganyika ni kosa?"[/h]

  1. makame silima 25/11/2011 kwa 11:02 mu · Ingia kujibu
    Kujita Mtanganyika kwa vile sio Mzanzibar basi sio kosa niuzalendo mkubwa wa kuto kuzarau asili ya nchi yako na historia yako, Na kujita Mtanzania ndio kosa kwa sababa Tanzania is come from no where(Dodoma ), na Tanzania haina historia yoyote ispokuwa imeundwa Dodoma tu kwa matakwa ya chama tawala ccm .
    Ndio mimi huwashangaza sana kuacha asili ya nchi yenu na historia yake na kukumbatia jina lisilo na Baba wala Mama, kwa hio Ndugu yangu (Mphamvu) jaribuni kuhamasishana ili mudai katiba ya Tanganyika na sio ya Tanzania.
    Mukidai katiba ya Tanzania kama Chadema speed yao basi itafika hadi mutajichanganya kuto kujuwa ni Watanganyika au Watanzania? maana sisi wazanzibar Sherehe zetu za Uhuru hazibadiliki zinakuwa zilezile za uhuru wa Zanzibar lakini nyiyi munajichanganya eti 9Dec1961 kutimia miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ovyoo?.
    Sikwamba umezaliwa kijijini na Unaishi Dar ndio ukazarau kijiji chaka na watu wake, Watanganyika wake up .

  2. Ashakh (Kiongozi) 25/11/2011 kwa 12:17 um · Ingia kujibu
    wasia huo
    Unahitaji kusimamiwa na kuendelezwa. Shime ndugu zetu wa Tanganyika, daini nchi yetu mujivunie historia yenu.
    Angalia wenzetu wa Zaire, asili yao ilikuwa ikiitwa Congo Kinshasa. Akaja mgalatia asiyejuwa thamani ya historia akaibadilisha ili kukidhi maslah yake. Baada ya kuondoka vijana ma-conservative wanaopenda na kujali historia yao wamelirudisha lilelile jina la asli – Congo.
    Nanyi musione tabu kwenda kinyume na mgalatia baba yenu hata ikiwa yeye alifanya makosa kupoteza asli yenu kwa kuificha nchi yenu Tanganyika. Hakuiuwa bali aliifich tu ili munufaike kwa kupitia mgongo wa Zanzibar. Sasa ni wakati wenu kuifichua, leo hii mukitaka Tanganyika itonekana.

  3. Nassor20 25/11/2011 kwa 2:25 um · Ingia kujibu
    Haha
    Nimefurahi sana leo kuona mzalendo wa kitanganyika kujita yeye mtanganyika,vijana wengi wa sasa wanasema kuwa wao wamezaliwa hakuna tngnyka. Na ukimwita hivyo ni sawa na kumtusi.
    Ni ufahari mkubwa kujita mtanganyika kwa sababu ndio nchi yako ilikupatia uhuru 1961.

Mbona waZanzibari mnarukia yasiyowahusu? Lini Zanzibar imesherehekea tarehe ya Uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza (10.12.1963)? Msituzuge, kila mwaka mnasherehekea mapinduzi ambayo ndiyo ulikuwa uhuru wa kweli kwa Wazanzibari wengi. Huo wa 1963 ulikuwa kwa waArabu na Wamangakoko wao. Tanganyika inachofaidi kwa 'mgongo wa Zanzibar' ni nini? Zanzibar ndiyo mzigo kwetu kuanzia umeme wa bure, kutegemea bara kibiashara, kukimbilia bara kuishi kwa uhuru zaidi na baadaye kurudi kwenye kifungo chenu huko kwenye visiwa vyenu kama mapumziko, mgawo wa mapato msiyochangia kitu, ....................................
 
Nina rafiki yangu ni Mtanganyika,tuko benet sana mshakaji huyu yeye ananita mimi mpemba,lakini nilimwita yeye mtanganyika anakasirika kiasi ambacho tunashindwa kuelewana tena,lakini mi katu siachi kumwita asili yake.

Sasa nauliza kujita mtanganyika ni kosa hali yakuwa ni mtanganyika ? Kwa nini sisi wazanzibari tuko na ufahari kujita wazanzibari,british ukikumbana nae popote ukimuuliza wewe nani atakuwa matatu,yeye m scotish,au irish ambao ni wa north ireland,au english ...

Kuna kosa gani mimi kumuita mtanganyika mtu wa mainland tanzania ?
 
Kuna wengine ukiwaita Wapemba, Wamasai, Wamachinga, nk wanakasirika mpaka hamwelewani! Mwingine unamwita "mwanamke" anakasirika huku ikionesha kuwa ni kweli yeye ni mwanamke! Hapa suluhu ni kumwita mtu anachotaka kuitwa! As simple as that!
 
Sio kosa ila ni Upumbavu. Tumeshaelimishwa sana kuhusu athari za kujitofautisha katika misingi ya Utanganyika na Uzanzibari. Hakuna mantiki iliyo dhahiri ya wewe kumwita mpemba (wich is inappropriate) badala ya Mtanzania (wich is logical and appropriate).
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom