Hivi kituko gani unakikumbuka ulikifanya wakati mdogo

Hahaha nimecheka sana na vituko vya utotoni, nakumbuka zamani sisi baba yetu alikuwa ni mtumishi wa serikali hivyo tulikuwa tunahamahama mikoa na hivyo tunahamishwa sana mashule

Mara nyingi mimi na ndugu zangu tukiitwa wageni maana shule moja humalizi hata mwaka, sasa bwana mimi mpenda vitabu nikiwa darasa la 3 Gangilonga Iringa, nikaazima kitabu kinaitwa 'dogodogo wanitesaaaa'

Kurudi home ilinichukua kama siku 3 kukisoma nikiwa nakificha na mto, salale baba akachungulia chumbani na kufunua mto na kunikuta ndio ninakimaliziamalizia...jamani nilichapwa! Mtoto wa miaka 8 unasoma dogodogo wanitesa....!! Mdingi akakichana kile kitabu

Kwenda shule nikawa nadaiwa mpaka ikabidi niache kwenda shule (nadaiwa na mtoto wa drs la 7 ), mama kugundua siendi shule ndio akanipeleka kwa mkuu wa shule na kulipia gharama za kitabu shs 40...

Kilichofuatia mkuu wa shule kwa ufisadi mzito hiyo hela hakumpa mdada anayenidai, akala kichapo na kuchimbwa biti juu kuwa asinidai tena!

Kwakweli mpaka leo kwa wiki nanunua wastani wa 2 storybooks, tht habit isn't easy to shake off..(Currently reading all 8 books of Alfu lela ulela )

Mhandisi
 
Aah mie nakumbuka nilikuwa naficha daftar la hesabu nnje juu ya bati mzee akiuliza namwambia nimekusanya mana lilikuwa na mikosa kibao. Kuna siku nikaliweka tena mzee akafunga milango usiku mvua ikapiga.
 
Nakumbuka nilipewa Hela ya UPE, basi siku moja nikaila kama Tsh 230 hivi,, nikawa naona noma kumuambia mdingi. siku akanibananisha kama nimelipa nikamwambia niliibiwa hela, mfukoni nikakuta tsh 770. Nilizichezea haswa
 
Si unajua zile za kulala mchana? Basi siku moja nililala mchana nikachelewa sana kuamka, mpaka saa moja na nusu sijaamka. Nakumbuka kabisa niliota naenda toilet kukojoa. Kumbe niliamka kitandani na kutembea(nikiwa nimelala/sina ufahamu) na badala ya kukunja kona ya kwenda toilet, nikakunja ya sebuleni na kukojoa. Nilivyomaliza nikaflush(kwenye ndoto kabisa naona). He! Nilishtuka naitwa, unafanya nini?? Nikawa kama bubu sielewi, kuangalia chini mkojo. Duh nilidekishwa! Mpaka leo najiuliza what happened mpaka nikakojoa sebuleni
 
Jamani nakumbuka mambo ya kombolela nilikuwa nachezea kichapo mbaya kwa maza du,
 
Nilikua natamani sana kujua jinsi mkojo unavyotoka...nikaenda nyuma ya nyumba, nikambana jamaa, nikamgeuzia juu, nikashusha kichwa ili niuone vizuri unavyotoka halafu nikaachia...mkojo ukapiga usoni, yaani nilikunywa mkojo kidogo ila nikajifunza kuwa kumbe ni kweli mkojo una chumvi! sisahau tena
 
Nakumbuka dingi alikua anafanya biashara ya ndizi sasa huruhusiwi kuchukua ndizi mana ni za biashara niliiba 2 nikaenda kula chooni mara nikakutana na mama wacha nile tifu la hatari darasa la 6 hiyo
 
Nakumbuka nyumba ya jirani kulikua na watoto watatu baba yao alikua na uwezo kifedha wilayani kwetu lakini pia alikua mkoloni sana. Kwao hawa watoto kukutwa na pesa lilikua ni kosa la jinai linaloadhibiwa kwa bakora lukuki.

Siku moja hawa jamaa zangu wakawa wameiba pesa ndani kwao hivo wakawa wamejaa pesa mfukoni. Jioni ilipofika wakaenda kununua samaki waliokaangwa kwa mama mmoja aliyeitwa mama khalidi. Huyu mama alikua ni jirani yao. Bahati mbaya huyu mama hawakumkuta kwani alikuwa amekwisha ondoka kuwapeleka samaki eneo la biashara ambapo ni mbali kidogo na nyumbani kwake.

Basi jamaa zangu kwa kuhofia kuchelewa nyumbani na kufika kabla ya baba yao hajawasili kutoka kazini wakarejea nyumbani mikono mitupu bila samaki. Mida ya saa mbili usiku baba yao akawa amekwisharejea nyumbani. Huku nyuma mama muuza samaki nae akawa amerejea kwake na akawa amebakiza samaki nadhani biashara haikuwa nzuri. Wanae wakamwambia kina flani walikuja nunua samaki hawakukukuta. Mama wa watu akajua dili hili siliachii. Si akabeba sinia la samaki hadi kwao na jamaa zangu. Kufika akabisha hodi, mmoja wa jamaa zangu akaenda kufungua mlango. Kugundua aliyepo mlangoni ni mama wa samaki akafunga mlango haraka haraka akijua mama kawaletea noma. Baba yake akauliza kwa nini kafunga mlango ilihali aliyebisha hodi hajaonana na wakubwa (yaani baba ama mama yao jamaa zangu). Akamuliwa afungue mlango mgeni aingie. Mlango ukafunguliwa mama wa samaki na sinia lake kaingia ndani.

Mama wa samaki akaeleza shida yake kuwa kapata taarifa samaki walihitajika wakati yeye akiwa biasharani. baba wa jamaa zangu akaitikia kinafiki ati ni kweli na akawahimiza wanae wanunue wale samaki kwa bashasha na unafiki mkubwa.

Baada ya biashara mama wa samaki huyooo akaondoka zake. Huku nyuma baba wa jamaa zangu akaenda kukata bakora akawahimiza wanae wawatafune wale samaki huku akitaka maelezo pesa ya kununua samaki ilitoka wapi. Jamaa zangu wakawa wazito kula wale samaki. Basi mzee akaanza kuwatembezea bakora kwanza za kuwahimiza kula wale samaki. Jamaa zangu wakawa wanakula wale samaki huku wakilia na wakati huo huo yule baba yao akiwa nje anaanda mzigo wa bakora huku akifoka "leo mtanitambua si nilishawakataza kuwa na pesa leo mtanitambua".

Jamaa zangu huku wakilia wakatafuna wale samaki lakini wakati huo huo mvua za bakora zikiwanyeshea kuwahimiza waongeze kasi ya kula wale samaki.

Aisee baada ya zoezi la kula wale samaki lilipokwisha baba yao aliwashushia bakora za kutosha sana kama adhabu ya kukiuka amri yake ya kutokukutwa na pesa mfukoni.

Ni kituko kilichofanywa na jamaa zangu lakini hunichekesha sana kila nikikikumbuka ama tukumbushanapo pindi nionanapo na mmoja wa hawa jamaa zangu.
 
Nilikua natamani sana kujua jinsi mkojo unavyotoka...nikaenda nyuma ya nyumba, nikambana jamaa, nikamgeuzia juu, nikashusha kichwa ili niuone vizuri unavyotoka halafu nikaachia...mkojo ukapiga usoni, yaani nilikunywa mkojo kidogo ila nikajifunza kuwa kumbe ni kweli mkojo una chumvi! sisahau tena
He he he heeeh!! Utoto bana...
 
ama kweli utoto noma, kuna watoto wageni wa kike walikuja hom, tukakubaliana 9t tutalala pamoja ili tuchezeane lkn kwa bahati mbaya tukalazwa bed tofauti, usiku wa manane nilizinduka toka usingizini na kuanza kunyemelea wageni ili kukamilisha ahadi, aiseee sababu ya giza sioni nilitumbukia kwenye bonge la sufuria limejazwa maji ya mvua, duh nilipiga mayowe na kusingizia eti nilikuwa natafuta sehemu ya kukojoa. chekechea hiyo
 
Hahahaha sio mchezo duh
 
Basi bwana kwetu tulikuwa tunapikia kuni, mama alipomaliza alikuwa na tekinolojia ya kuweka moto ili ukae asisumbuke kununua viberiti. Mie nikaenda nikakojolea ule moto nikiwa uchi. Nilikuwa nimeambiwa kuwa itaharakisha kuotesha manywele ya kule chini ili nionekane mkubwa. Majivu yakatanda mwili mzima mpaka nikaonekana kama mawingu. Mama akanipa adhabu ya kuchota maji mpaka nijaze drum.
 
Mimi toka mdogo sikuwa napendwa suala la kuonewa, wakati nipo darasa la 6, kuna siku nilichelewa shule, baada ya kufika eneo la shule nilikuta viranja wakizuia wanafunzi waliokuwa wamechelewa. Niliposimamishwa na Kiranja nilikaidi na kwenda mojakwamoja kwenye eneo ambalo wanafunzi wengine waliowahi walikuwa wamejipanga ambapo muda wa kukimbia mchakamchaka ulikuwa umewadia. bila kujua kumbe wakati nakaidi kuzuiwa ,mwalimu mmoja mnoko alikuwa ameniona na kunisikia nikigoma kuzuiwa, ghafla wakati niko mstarini nilisikia nikiitwa ili kuadhibiwa, haikuwa rahisi kwani nilihoji sababu za kuadhibiwa na mwalimu, bila kutegemea mwalimu alirusha kofi ambalo pamoja na kujitahidi kulikwepa lakini lilinipata kiaina, jambo hilo lilinighadhibisha sana hivyo nikachukuwa hatua za kutoa tusi lililokuwa linamlenga mama yake mwalimu huyo, baada ya kuona vita ni kali nilitimua mbio ambapo mwalimu aliamuru wanafunzi wanifukuze hadi wanikamate kitendo hicho cha kukimbizwa niliona ni cha kunivunjia heshima hivyo baada ya kukimbia kama mita 100 nikasimama huku kundi la wanafunzi wakinifuata, nilipata ujasiri wa ajabu wa kuokota jiwe na kuanza kuwafuata wanafunzi waliokuwa wananikimbiza, kwa mafanikio makubwa niliwarudisha wanafunzi wote mpaka eneo walilokuwa wamesimama na mimi sikasimama juu kidogo nakuwaeleza kuwa mtu aje anikamate wakati narudisha kikosi hicho nilifanikiwa kumpora panga kijana mmoja aliyekuwa anakwenda shamba hivyo nikawa na silaha ambayo iliwaogopesha wanafuzi wote. Picha niliyocheza ilikuwa ni ajabu kwani kwa muda kama wa masaa 2 wanafuzi na walimu walishidwa kufanya chochote hadi ndugu yangu mmoja alipoitwa na kunisihi niachane na vita hiyo. baada ya hapo nilisimamishwa shule kwa miezi miwili na kutakiwa kuwaomba radhi walimu kwa kile nilichokifanya. Mtihani wa mwisho wa darasa la saba niliweza kufaulu mimi peke yangu pamoja na ukomandoo wote.
 
Nilipokua mdogo nilikua nasumbuliwa sana na kifua. Sasa cku moja nikamsikia bro akisema dawa ya kifua ni pombe kali. Nakumbuka cku moja ya xmas kifua kilikua kinakwaruza, mi nikaingia room kwa dingi kulikua na chupa ya whisky nikaanza kuinywa! Muda huo ndugu zangu walikua wako huko nje wanapiga stori. Basi ili nisikamatwe nikafunga mlango wa nje kwa ndani nikaendelea kujimiminia kilaji. Si nikalewa nikaishia usingizini! Unaambiwa cku hiyo watu wote walilala nje! Gonga mlango.. Wapi! Duh..

Umenikumbusha mambo ya kilevi ngoja niunganishe hapa. Basi wakati nipo darasa la 4 siku moja nikakuta brother anakunywa Pombe moja hivi ambayo nafikiri ilikuwa dengerua, nilitamani ila hakuonyesha dalili ya kunionjesha, kwa bahati akaitwa na mgeni nje jambo lililomfanya atoke. Ile ilikuwa nafasi kwangu kwani nilipiga kama litamoja na nusu halafu nikatimka kurudi home, wakati niko njiani ndiyo nikaanza kuyumba huku nikiimba na kutamka maneno ya kilevi, kimsingi njia nzima nilikuwa nashangiliwa na watu hasa vijana niliokutana nao kwani nilikuwa nayumba vibaya sana. Kufika maeneo ya home nilikutana na mother anamsuka mwenzake ambapo sikuwa na uwezo hata wa kumsalimia zaidi ya kutoa tabasamu la kilevi na kunyoosha mkono kama ishara ya kumsalimia huku nikijitahidi kujikaza ili nisiyumbe bila mafanikio, mama alishikwa na butwaa kubwa kwani katika maisha yake sidhani kama alishawahi kuona mtoto aliyelewa pombe, nilipotinga sebuleni tu nilishamgaa nikitapika na kufanya sebule yote ienee matapishi na kwa bahati mbaya siku ile nilikuwa nimepiga ugali wa mhogo na maharage kitu kilichosababisha hali ya hewa na mazingira eneo lile riharibike. Baada ya kuzimika kwa muda kadhaa nilizinduka na kuomba radhi kwa kile kilichotokea!
 
Mimi nikiwa darasa la sita nilipendana msichana mmoja lakini hatukuwahi kufanya chochote maana sikujua namna ya kuanza. Siku moja nikiwa na huyo msichana tulikutana na baba yangu ambaye alikuwa hataki watoto tutembee mbali na nyumbani bila sababu. Alinipiga kofi kali sana mbele ya msichana wangu, niliumia, lakini kilichoniliza ni kupigwa mbele ya yule msichana...kesho yake tulipoonana, aliponiona tu alilia sana...du machozi yananilenga...naishia hapa!

Pole sana nakuona jinsi ulivyoaibika mbele ya demu wako, mimi bwana nilikuwa najua mchezo unapofanyika ila wakati nimeshavua kaptula yangu na kuiweka pembeni huku mtu wangu naye akiwa amenyanyua sketi yake juu, wakati naendelea kufaiti (wakati huo tupo kichakani) kwa bahati mbaya kumbe baba yake demu wangu kumbe alikuwa anatulia timing, kucheki pembeni nikamuona dingi wake kachuchumaa alipogundua kuwa tumemshitukia na mimi nikijitahidi kuokota kaptula yangu nilisikia akinitia moyo kuwa nisikimbie nimalize hata hivyo nilitimka ile mbaya na kila nikimuona ilikuwa nalala mbele.
 
Mimi toka mdogo sikuwa napendwa suala la kuonewa, wakati nipo darasa la 6, kuna siku nilichelewa shule, baada ya kufika eneo la shule nilikuta viranja wakizuia wanafunzi waliokuwa wamechelewa. Niliposimamishwa na Kiranja nilikaidi na kwenda mojakwamoja kwenye eneo ambalo wanafunzi wengine waliowahi walikuwa wamejipanga ambapo muda wa kukimbia mchakamchaka ulikuwa umewadia. bila kujua kumbe wakati nakaidi kuzuiwa ,mwalimu mmoja mnoko alikuwa ameniona na kunisikia nikigoma kuzuiwa, ghafla wakati niko mstarini nilisikia nikiitwa ili kuadhibiwa, haikuwa rahisi kwani nilihoji sababu za kuadhibiwa na mwalimu, bila kutegemea mwalimu alirusha kofi ambalo pamoja na kujitahidi kulikwepa lakini lilinipata kiaina, jambo hilo lilinighadhibisha sana hivyo nikachukuwa hatua za kutoa tusi lililokuwa linamlenga mama yake mwalimu huyo, baada ya kuona vita ni kali nilitimua mbio ambapo mwalimu aliamuru wanafunzi wanifukuze hadi wanikamate kitendo hicho cha kukimbizwa niliona ni cha kunivunjia heshima hivyo baada ya kukimbia kama mita 100 nikasimama huku kundi la wanafunzi wakinifuata, nilipata ujasiri wa ajabu wa kuokota jiwe na kuanza kuwafuata wanafunzi waliokuwa wananikimbiza, kwa mafanikio makubwa niliwarudisha wanafunzi wote mpaka eneo walilokuwa wamesimama na mimi sikasimama juu kidogo nakuwaeleza kuwa mtu aje anikamate wakati narudisha kikosi hicho nilifanikiwa kumpora panga kijana mmoja aliyekuwa anakwenda shamba hivyo nikawa na silaha ambayo iliwaogopesha wanafuzi wote. Picha niliyocheza ilikuwa ni ajabu kwani kwa muda kama wa masaa 2 wanafuzi na walimu walishidwa kufanya chochote hadi ndugu yangu mmoja alipoitwa na kunisihi niachane na vita hiyo. baada ya hapo nilisimamishwa shule kwa miezi miwili na kutakiwa kuwaomba radhi walimu kwa kile nilichokifanya. Mtihani wa mwisho wa darasa la saba niliweza kufaulu mimi peke yangu pamoja na ukomandoo wote.
Anold hapo kwenye blue nakufananisha na Starring wa cinema za kihindi, kwa jinsi ulinyofanya hiyo action
 
Nakumbuka nikiwa std 1, kuna rafk yangu anaitwa ben, aliomba nimfutie kwenye daftar lake, na bahat mbaya likachanika kidogo, kilichofuatia naye akachana kdogo langu, nami nikachana, ikawa chana nichane, 2kamaliza madaftari yote mawili. Nilirud nyumban nalia, mama alinipoza na kunipa hela ya kununua jingne, cjui ilikuwa sh. Ngap kpnd hcho, 95
 
Haaa,haaaa,mi nakumbuka nilipokuwa boarding form two,hiyo siku ilikuwa zamu yetu kufanya usafi wa bwalo la chakula,wakati tunafanya usafi(kudeki)nakumbuka mwalimu wa zamu siku hiyo alikuwa Mr.Saruji(jina la utani),ghafla aliingia bwaloni,akakuta jamaa yetu mmoja anapiga stori na vicheko vingi,kwahasira teacher akawa anamwita kwa hasira mkononi kashika fimbo huku anamfuata,karibu anamkaribia tukashtukia teacher kadondoka chini kwa kishindo,tulicheka sana tulikimbia tukijua akinyanyuka ni mbogo,kumbe pale chini kulikuwa na ganda la ndizi mbivu ndo alilolikanyaga,siisahau hiyo siku tulipandishwa assembly tukachezea mbakora kuliko maelezo!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom