Hivi Kikwete anaweza nini?

Hawezi kitu. Angeweza si angemwondoa Mary Chatanda kule Arusha maana yeye ni Mwenyekiti. Angeweza pia angeongeza mishahara baada ya inflation kubwa, angeajili walimu, angekiweka UDOM kwenye mazingira mazuri ya kiutendaji, lakini UDOM ni agenda waliyoidandia, ilikuwa ya CHADEMA, haiko kwenye ilani yao na wala hawatakiweza, angeweza angewaondoa viongozi wavurundaji kama Hosea, Mwema, Sofia Simba, Makongoro Mahanga. Kwa hakika hawezi. Tuombe tumalize miaka mitano yake iliyobaki salama. Kigoda cha Mwalimu Nyerere kililiona hili mapema wakasema asiteuliwe tena, lakini wapenda kula wa CCM wakasema anaweza, ona sasa!
 
Ni Swali zuri amabalo linahitaji mjadala mpana sana,

Kwanza mimi ninaweza kujibu hilo kwa kuangali pande mbili yaani Chanya na Hasi.

Chanya
Siyo kwamba Kikwete hakuna kitu amabacho hawezi, kuna mengi kama akiamua kuwa na uthubutu wa kukemea na kuyasimamia,anaweza kufanya maajabu makubwa katika kulilitea hili taifa maendeleo maaan kila kitu kipo kuanzia Mbuga za wanyama, maziwa makuu, madini na rasimali watu,mfano mzuri ni ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma.

Hasi

Huyu bwana kitu amabcho kinammaliza ni kuwapa watu kazi amabzo hawana uwezo wa kuzifanya,ama wana uwezo mdogo wa kufanya maamuzi na kusimamia vitengo/idara husika au wanaongozwa na tamaa za kujitajilisha wao na familia zao kwanza, wengi ni mafisadi wakubwa wasiokuwa na hata chembe ya huruma kwa kufuja rasilimali za taifa.
Hii imesababisha idara nyingi sana kufanya vibaya na lawama kwenda moja kwa moja kwa rais maana ndo aliyewateua.

Ushauri.
Rais kikwete anatakiwa kufanya yafuatayo ili akiondoka madarakani apatwe kukumbukwa na hata na vizazi vijavyo
Sekta ya madini.Tanzania mpaka kufikia mwaka jana tulikuwa na deposit ya dhahabu kiacha ~100Moz, hiki ni kiasi kikubwa sana kwa nchi kama Tanzania, kinachotakia ni usimamizi makini wa hii sekta ili tanzania ipate kunufaika na siyo vingivyo.
Hii ni moja kati ya sekta muhimu sana katika kutoa ajira kwa watanzania, lakini nenda huko, ni aibu tupu, unakuta expart mzungu hata jianlake kuandika ni shida

Sekta ya Utalii.Hii ni sekta muhimu sana ambayo ikutumia vizuri na kuondoa uozo/ufisadi uliyoko huko, unaweza kumsaidia sana kupata pesa za kufanyia mambo mengine ya muhimu kama kuwalipa watumish mishahara mizuri ili wawe ni wenye tija kwenye kazi zao.

Kilimo-Hii sekata ianachekesha sana, maana kumekuwa na kauli mbiu nying sana mara kilimo ni uti wa mgongo, mara mapinduzi ya kijani mara Kilimo kwanza, lakini ukichunguza kwa makini watendaji wake wengi hqawana dhamira ya dhati kukikomboa kilimo cha hapa Tz, sikiliza kuna watu wananyimwa ruzuku za pembejeo kisa ni wapizani, kwa mtaji huu hiki kilimo ktaendelea kuwa uti wa mbavu mpaka hapo baadaye, cha msingi hii wizara inatakiwa apewe mtu anayejali maslahi ya taifa mbele,mwenye vision and mission lazima awe ni mtu wa objectives.Tanzania ni kubwa sana na aslimia 80% ya watu wanategemea kilimo, atumie sera ya majimbo katika hili, hakika atafanikiwa sana.

Namalizia kwa kusema wasaidizi wa rais sasa ni wakati mwafaka wa kuona aibu na kuchapa kazi, wengi mtakumbukwa kwa matendo yenu na dhamira zenu za kulitumika hili taifa.
 
...kwa mimi niliyewahi kuishi dodoma nimeshajua huyu NewDawnTz anamaana gani,kweli kabisa mkubwa,hapo umenena!!:A S thumbs_up:
 
Nga nge ngi ngo, na ne ni no!!! na majungu na uchonganishi
 
hivi ni kitu gani serikali ya kikwete inaweza? Maana hata kulipa watu mishahara kwa wakati muhafaka ni tatizo! Na ukiangalia vizuri unakuta zile wizara na taasisi zilizopewa hawa ndugu zetu... Mtandao cum vibarakashia cum wakwe ndo zinavurunda shoto kulia! Hii sio siri ila kama kuweka usawa wajameni kati ya hawa ndg zetu kuna wale wenye uwezo yaani wanaoweza kupewa uongozi wa wizara au taasisi au jeshi on merits na waka-deliver na sio jinsi hali ilivyo sasa! Hii inakera mbona wakina shivji hawapewi hizo taasisi nyeti wakaziendesha au ndo kujipaka matope kwenyewe kwa kupitia mgongo wa udini kwamba hatuwezi! Tuwe wakweli jamani kwenye uvundo na kuvurundwa kwa serikali ya sasa kuna vijielementi vya watu kupewa vyeo without merits kuanzia chama, kuja serikali, jeshi mpaka taasisi! Tuondelee tu kuangalia cinema!

Nb: Simchukii mtu miye ni muislam safi niliyeelimika mweye uchungu na nchi yangu!

watu waliotuletea hizi dini ndio wametuharibu....na ndilo lilikuwa lengo lao......kutugawa.....usitaarabu wa babu zetu wa zamani na tunguli zao ulilipa na unalipa....relatively.....
 
Muda tumeshampa wa kutosha hakuna alilolifanya la maana na wala hatafanya zaidi ya kuzidi kutuudhi na kututia katika mazingira hatarishi.Oh sijui watendaji wabovu kitu gani,wanao wakiwa hawana adabu manake ni mapungufu yako umeshindwa kulea watoto.Hana kisingizio chochote it simply hawezi uwezo wa nafasi hiyo hana,tukumbuke maneno ya Kambarage kwamba hakuwa amekomaa kushika urais,pale alimaanisha kwamba hafai sema tu alitumia maneno ya kistaarabu zaidi.
 
Jamani mwacheni rahisi ,anaweza mengi
anaweza kuendelea kutawala kisanii hali ya wananchi ikiwa mbaya
anaweza kuwarubuni wadanganyika kwa kiwango kisichoelezeka
kuwaruhusu wezi warudishe fedha walioiba !
Kuwapa wala rushwa muda wakujirekebisha.
Ameweza kuvumilia kuitwa mwizi /fisadi bila kujibu!
Kwa ujumla ana sifa za uongozi za kipekee hapa dunian..
.....kama angekua nchi nyingine za wajinga angekua ameshajiudhuru siku nyingi sana
rais ambaye watendaji wake wanaonekana wanafanya vibaya yeye ni mzuri !!!!!!!!!!!!!!??
Hii haipo ktk nadharia zote za uongozi
anastahili sifa!
 
Back
Top Bottom