Hivi kibonde anafikiria nini wakati mwingine??

Habari za leo wanajamii!!!
Jana jioni nikiwa ndani ya daladala narudi nyumbani kutoka kazini, Radio hewani ilikuwa ni clouds fm jahazi. Sasa ilikuwa ni ile segment ya magazeti ya leo ambapo walikuwa wanazungumzia ushauri aliotoa Dovutwa kwa raisi wa nchi kuwa ni bora angejiuzulu kwa kushindwa kushughulikia tatizo la RUSHWA NDANI YA CHAMA Kufuatia chaguzi zilizopita za ndani ya chama ambapo suala la rushwa lilikuwa nje nje.

Sasa basi huyu KILOPO bwana Kibonde akaanza eti “ooh hawa waandishi wanauza magazeti kwa cheap stories za siasa maana kama ni suala la rushwa wao wanaishia kuripoti tu. Kama wao ni waandishi bora kwanini wasingeingia na kufuatilia kwa undani haya madai kupata ushahidi na vidhibiti na hatimae kuwakamata. Sasa wao wanaishia kufanya kazi za tunasikia… very stupid” Hapo ni mwisho wa kumnukuu.
Sasa basi mimi ninajiuliza maswali yafuatayo;
1. Katika kazi zao waandishi wa habari wanakuwa ni makachero wa rushwa??
2. Na je nini kazi ya makachero wa PCCB ambao wanalipwa vizuri tu kwa pesa za walipa kodi wengi ambao ni masikini na ndio VICTIM wa rushwa??
3. Hivi ni nini hasa kinampa huyu KIBONDE jeuri ya kuwaambia/kuita kazi za wenzie stupid?
4. Waandishi wenzie angalau wanapaza sauti na kalamu zao kuwasilisha hayo matatizo sugu,je yeye kafanya nini zaidi ya kubwabwaja pumba tu ndani ya studio na kupamba hao wala rushwa??
Mjadala upo wazi wanandugu.

kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake. huo ni mtizamo wake juu ya tatizo la rushwa. kama mtu mwingine ana maoni tofauti basi ruksa kuyaweka bayana pasipo kutumia lugha za ukakasi mpaka wengine wanafikia ku-disclose health status za watu pasipo consent zao, si busara. Moreover, kifo hakiji kwa sababu moja tu, kuna watu wanaamka wazima, jioni wanaaga dunia hata bila kuugua. Kwa mtizamo wangu bado naamini tunaweza ku-brainstorm njia nzuri ya kutatua tatizo la rushwa katika nchi yetu bila kutukanana. asante.
 
Habari za leo wanajamii!!!
Jana jioni nikiwa ndani ya daladala narudi nyumbani kutoka kazini, Radio hewani ilikuwa ni clouds fm jahazi. Sasa ilikuwa ni ile segment ya magazeti ya leo ambapo walikuwa wanazungumzia ushauri aliotoa Dovutwa kwa raisi wa nchi kuwa ni bora angejiuzulu kwa kushindwa kushughulikia tatizo la RUSHWA NDANI YA CHAMA Kufuatia chaguzi zilizopita za ndani ya chama ambapo suala la rushwa lilikuwa nje nje.

Sasa basi huyu KILOPO bwana Kibonde akaanza eti “ooh hawa waandishi wanauza magazeti kwa cheap stories za siasa maana kama ni suala la rushwa wao wanaishia kuripoti tu. Kama wao ni waandishi bora kwanini wasingeingia na kufuatilia kwa undani haya madai kupata ushahidi na vidhibiti na hatimae kuwakamata. Sasa wao wanaishia kufanya kazi za tunasikia… very stupid” Hapo ni mwisho wa kumnukuu.
Sasa basi mimi ninajiuliza maswali yafuatayo;
1. Katika kazi zao waandishi wa habari wanakuwa ni makachero wa rushwa??
2. Na je nini kazi ya makachero wa PCCB ambao wanalipwa vizuri tu kwa pesa za walipa kodi wengi ambao ni masikini na ndio VICTIM wa rushwa??
3. Hivi ni nini hasa kinampa huyu KIBONDE jeuri ya kuwaambia/kuita kazi za wenzie stupid?
4. Waandishi wenzie angalau wanapaza sauti na kalamu zao kuwasilisha hayo matatizo sugu,je yeye kafanya nini zaidi ya kubwabwaja pumba tu ndani ya studio na kupamba hao wala rushwa??
Mjadala upo wazi wanandugu.

Wee endelea kumchukulia kirahisi rahisi Kibonde sasa hivi utashtukia tu ni mkuu wa wilaya yako, mimi namkubali sana kibonde ni mpambanaji hivi unategemea yeye hajui kwamba ana sifa za kuwa mkuu wa wilaya? Mjini hapa stuka!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom