Hivi JOTI anawarekebisha au anawaumbua wasanii?

Sep 4, 2012
15
0
Jana mtu mzima AY katokelezea kwenye segment ya copy and paste kwenye kipind cha orijino commedy -TBC 1,shukrani zimwendee joti kwa kuwafichua vilaza wote wanaojiita wanamziki,
 
Anawaweka attention kuwa wawe wabunifu na vitu vipya sio vile tulivyovizoea na tukavichoka...
 
bwahaha AY kakopi wapi tena? wenyewe ukiwauliza wanakuambia eti ni sampling na sio copy na paste
 
kina Joti hawana jipya watafute kazi nyingine ya kufanya kuchekesha wameshashindwa.....ivi iyo copy n paste nayo ni kichekesho??......yani wamekuwa kama marehemu anaetaka kuondoka na wake.
 
Joti ana chambua makosa ya maproducer na kudhani ni mkosa ya wasanii!
 
kina Joti hawana jipya watafute kazi nyingine ya kufanya kuchekesha wameshashindwa.....ivi iyo copy n paste nayo ni kichekesho??......yani wamekuwa kama marehemu anaetaka kuondoka na wake.

Mkuu karibu hongera kumaliza ban,ila kina joti hawana kipya,ile ni kundi la kucopy
 
pia nao hawana jipya bora hata mwanxo wakiwa eatv, bt now bureee kabisaaaaaa
 
bwahaha AY kakopi wapi tena? wenyewe ukiwauliza wanakuambia eti ni sampling na sio copy na paste

sampling ndo coping hiyo hiyo chalii yangu,wanaipaka rangi tu!F.A akajifanya Fredro Star wa ONYX kipidi kile na ngoma yake ya ingekuwa vipi,Mike T akajifanya Fifty Cents na ngoma yake ya Je Utanipenda akikopi 21 questions ya mtu mzima thumni and the list goes on!mi nawatazamaga waavyojishebedua halafu nikitaka muziki wa kweli nawatafuta Parapanda Arts naona kitu cha moja kwa moja jukwaani roho inasuuzika..........wote wezi tu!!
 
Joti ana chambua makosa ya maproducer na kudhani ni mkosa ya wasanii!

siamini kama wasanii wanakuwa hawajui,wanajua na wanaafiki..some of them nimewasikia wakitoa maelekezo ya 'nataka beat kama ya fulani' nikiwa studio,sidhani kama msanii makini anaweza fanya hivyo.varieties zinatakikana sokoni ila Joh Makini kujifanya Hover,Godzila kujifanya Fifty,Ngwea kuwa na swaga za Wizy,Pina kukausha koo kwa kujifanya Dmx nadhani haikai poa wazee,what happened to creativity and uniqueness?wapi ngoma kama ANHA! au USHANTA au NINI DHAMBI za X-PLASTAZ?kina joti wanakosea kwenye ya kwao(mi sijali sana huko)ila kwa hili wanaambia wanamuziki wetu ukweli!!
 
sampling ni illegal na unatakiwa upate ruksa ya mwenye nyimbo kwanza sio unaamka asubuhi hapo bungoni unachuka beat ya mtu nzima nzima unsema una sample huo ni ufala. tatizo lilipo ni la kijamii hii nchi kimsingi haina vichwa kwa maana ya creativity na originality, lishe tunayopata udogoni ni duni pia tunanyonya sana maziwa ya ng'ombe udogoni mama zetu wanata matitia yabaki wima, maziwa ya ngombe yanadumaza akili.
 
Back
Top Bottom