Hivi JK hili amepatia?

mamanalia

JF-Expert Member
Nov 7, 2009
667
146
Hivi karibuni tumeshuhudia The elephants wakija kufanya friend matches zao hapa TZ.
Rais wetu amevutiwa sana na hawa players kama drogba na kuacha majukumu makubwa yanayomkabili na kwenda kuandaa chakula na hawa wachezaji. Nauliza ni kweli sababu za kikwete alizozitoa pale kwenye tafrija zinatosha kumpa muda wa kukutana na wachezaji hawa na kuacha ofisi? au ndo mawaziri wa michezo na wasaidizi wake hawakuwa na wazo hilo!!!!

Mie naona sasa JK aweze kuchagua vitu gani vya kuvipa kipaumbele. Siamini kama alivyosema kuwa drogba aliongea na sky news ndo kunaitangaza TZ, inamaana tumeshindwa kuitangaza TZ hadi tusubiri drogba aje? wadau niambieni kama ninafikiri vibaya au la, mie ninaona aibu kwa rais wetu kuacha ofisi na kwenda kumfagilia drogba.
 
sandy_mwenguo_06.jpg
 
Kuitangaza nchi ni jambo jema zaidi katika biashara ya kimataifa. Hata hivyo namna ya kutangaza tangazo lolote lazima kuzingatia vitu kadhaa muhimu.
1. Gharama za matangazo zisizidi matokeo ya matangazo husika;
2. Wigo wa kufikia wadau (coverage);
3. Kuzingatia muda (timing), je ni muda mwafaka kufanya tangazo hilo?

Aidha, suala la Rais kujitokeza na kuongelea majukumu ya kuitangaza nchi yaweza kuwa na kuingilia majukumu ya wasaidizi wake (mawaziri hasa - michezo, utalii na biashara). Hiyo ni sawa na baba katika familia kuwapa majukumu watoto wake, halafu inatokea sasa anaamua kufanya kazi ya mmoja wa timu ya vijana wake. Hiyo inaonyesha aidha, kijana kashindwa kazi, (i.e. hawezi uendana na kasi inayotakiwa) ama hajua cha kufanya.

Tumekuwa tukiongelea humu jamvini (JF) habari za uimara wa serikali yetu iliyopo madarakani tangu 2005. Tatizo kubwa ni kukosa dira na mwelekeo kitaifa. Masuala yanafanywa tu kama vile ilikuwa ndoto ya usiku huo, mtu akaamua kuwaambia wanakundi kwamba inabidi leo tufanye hivi. Nasema hivyo, kwa sababu masuala haya ya nchi kujitangaza yanatakiwa yawepo kwenye mikakati ya nyaraka za serikali katika sekta husika. Siyo tu inapotokea mazingira ya kuchezwa kwa mechi kama ya juzi ndipo eti tunaona huo ni mwanya wa kufanya hivyo. Hatuna dira kama nchi.

Mimi huwa natazama televisheni za kimataifa, mara nyingi nawaona kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki, Kenya tu ndiyo wana matangazo kuhusu nchi yao na rasilimali zao. Wanaonyesha vitu walivyojitahidi kuviendeleza na ni vivutio kwa wengine (mataifa) kwenda kuviona na hata kuvitumia. Mfano mzuri ni shirika la Ndege la Kenya (KQ).

Kama nchi pengine kwa vile hatuna dira na mwelekeo, hata hayo masuala ya kuyatangaza pengine hayajulikani kwa mujibu wa Serikali. Ndiyo maana sasa wanabaki kimya na kuvizia kutumia shilingi bilioni 7 kuunda kamati ya FIFA 2010. Hizo ni fedha nyingi sana kuweza kutumiwa ndani ya muda wa miezi mitano tu eti zikawa zimeisha. Tujiulize na kujisahihisha kabla ya mambo hayajaharibika zaidi.
 
ni sawa kama anaingilia majukumu ya wasaidizi wake lakini rais akizungumzia kitu chochote huwa kina sound great sana maana yeye ni taswira na alama ya nchi na watanzania wote.
 
Kwani ile kampeni yake ya kulitangaza taifa huko nje ya nchi kwa miaka minne iliyopita imefanikiwa vipi na iliisha lini?
 
Ukweli unabaki palepale kuwa kwa maamuzi yetu tuliyofanya miaka minne iliyopita matokeo yake ni MAUMIVU.
 
ni sawa kama anaingilia majukumu ya wasaidizi wake lakini rais akizungumzia kitu chochote huwa kina sound great sana maana yeye ni taswira na alama ya nchi na watanzania wote.


Ndio maana akaweka wasaidizi wake! Kama wameshindwa tujue ili wawekwe wengine!
 
Ni muhimu kutangaza kitega uchumi muhimu kama uwanja mpya na hasa wakati tunakaribia WORLD CUP 2010.
 
amemtangazia nani hasa; kanuni moja ya marketing is know your 'target'.. .. can somebody help me out kampeni yao ya kutangaza uwanja wetu mpya wanamlenga nani?
 
Namkumbuka marehemu Kolimba "CCM haina dira wala mwelekeo" Serikali yetu ya CCM na inaongozwa na CCM. Dira au mwelekeo ni bidhaa adimu
 
Nadhani JK hana makosa jamani,mnajua uwepo wa Drogba na wenzake hapa nchini umefanya vyombo vya habari vya nchi nyingine viwe attentive kutaka kujua kinachoendelea hapa tanzania, kilichiniudhi ni kumpa jamaa "ubalozi" hiyo inaashiria kuwa tumeshindwa kuitangaza nchi hadi tusaidiwe, jamani hajafanya vibaya sana though inaleta hisia kuwa president anapenda sana attention ya vyombo vya habari.
 
Nadhani JK hana makosa jamani,mnajua uwepo wa Drogba na wenzake hapa nchini umefanya vyombo vya habari vya nchi nyingine viwe attentive kutaka kujua kinachoendelea hapa tanzania, kilichiniudhi ni kumpa jamaa "ubalozi" hiyo inaashiria kuwa tumeshindwa kuitangaza nchi hadi tusaidiwe, jamani hajafanya vibaya sana though inaleta hisia kuwa president anapenda sana attention ya vyombo vya habari.

mbongotz.. hili ni kweli na sidhani kama kuna mtu anabisha kuwa uwepo Drogba kumefanya watu wengine wafuatilie.. lakini kinachonisumbua mimi ni kuwa beside Soccer.. ni kwa namna gani Tanzania inanufaika?
 
Sidhani kuwa kuna tatizo kwa JK kuwaalika wageni wake kwa lunch au dinner wakati wowote ambao anaweza kufanya hivyo. Vile vile, sidhani kama ingewezekana Waziri aandae chakula hicho wakati Rais alishaamua kufanya hivyo. Labda kama muda ungekuwa unaruhusu kwa Timu hiyo ya Cote D'voire kuhudhuria chakula cha Rais na Waziri katika vipindi tofauti. Kitu ambacho pia sioni mantiki yake.

Hii ni desturi ya ukarimu ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi.

Naamini pia kuwepo kwa timu ya nje na hasa wachezaji wa kimataifa, kulivuta kamera nyingi. Ila sina uhakika kama mechi ilipata international coverage au wapiga picha hao walifanya hivyo kwa kumbukumbu zao tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom