Hivi JK anapokelewaje airport za Marekani na nchi zote za G 8?

mshikachuma,
obama hajawahi kumpokea jk airport hata siku moja. marais wote wanaotembelea usa km wana appointment ya kukutana na obm huwa ni kwenda ikulu ambapo kama ni mgeni rasmi wa obm ndo huwa anapokelewa rasmi pale. sio uwanja wa ndege.
Nimekuelewa Mkuu, Je hao watu wanaotumwa kwenda kumpokea JK aiport huwa wanasindikiza kwa mapikipiki,magari na
mizinga hadi ikulu kama wanavyofanyiwa pindi wawasilipo hapa kwetu?
 
Huyu hapa:

IMG_0018.jpg

Hapa mkuu sio airport wala camp David panaonekana kama shopping mall vile maana kwa mbali namuona binti wa kithungu na mfuko wake kuonyesha katoka kupata mahitaji kwenye hiyo Mall
 
Kuna ujio wa Urais wa aina nyingi, binafsi, ziara ya Kitaifa, ziara ya kikazi, ziara ya kuhudhuria mkutano? ndio maana utaona zingine zina mizinga zingine hazina. Hutegemea na safari yenyewe.
Sawa...lakini hizo ziara zote ulizoziorodhesha hapo juu JK keshazifanya nchini Marekani.
Sasa swali langu ni lilelile...amewahi kupokelewa ki V-I-P hata siku moja? Kuanzia security,media coverage na mapikipiki?
 
mkuu, kama kuna marais mbau(20) wanaotembelea usa per day basi obama angekuwa hana muda wa kufanya kazi nyingine zaidi ya kuwa busy kuwapokea hao marais. mi kwa muono wangu nadhani pale state department kuna kitengo maalum cha kuwapokea marais and etal hivyo obama halazimiki kwenda viwanja vya ndege kusubiri kuwapokea.

Mkuu,
Si marais wote wanaokwenda Marekani humwona Obama...wengine wanaenda kutibiwa..... wengine kwenye biashara zao binafsi..... wengine window shopping....NYC ni kitu ingine kabisa si kama Dar es Salaam tunapangwa barabarani kumpokea Mugabe!
 
Mapokezi ya rais kutoka katika nchi zinazoendelea kama Tanzania huwa wanamapokezi ya aina mbili:

  1. Kama amealikwa na kiongozi mkuu wa nchi hiyo, airport hupokewa wa gavana wa jiji atakapofikia wakiongozwa na msafara wa mapikipiki kama kawaida na mwenyeji wake humsubiri ikulu ambako hupata heshima za mkuu wa nchi na kupigiwa mizinga 21.
  2. Kama amekwenda kwa ziara binafsi au katika mikutano ya mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa hupokewa na viongozi wa mashirika husika na huweza kupangiwa ratiba ya kwenda kumsalimu kiongozi mkuu (Courtesy call) wa nchi aliyoitembelea kama atakuwepo nchini kwake
Nimekupata mkuu, lakini hapo kwenye Bold...kweli imewahitokea JK akapata escort ya mapikipiki 8 au 6 kama tufa
nyavyo hapa Bongo? Jamani mwenye picha ya mapokezi ya JK kuanzia airport za marekani hadi ikulu atuwekee hapa tuone.
 
Sawa Mkuu... lakini je huwa anapokelewa kwa msafara wa mapikipiki na magari hadi njia zinasimama kwa mda?
Na hapo airport analakiwa na nani? Gavana wa jimbo,meye, au Rais wa nchi? Je imehahi tokea Rais wa Marekani
kwenda airport kumpokea Kikwete?

Hakuna gari linalosimama au barabara kufungwa, watu au wananchi wanendelea na shughuliza zao kama kawaida na hata Kwenye traffic light huwa gari lake linasimama mpaka taa zitakapo ruhusu. Huku sio Kama Tanganyika tuseme Kikwete anapita na msafara wake basi barabara zifungwe kwa kuwa Fisadi fulani anapita. Huku hakuna hizo hata wakati mwengine Obama mwenyewe gari lake linasimama kwenye Traffic light.

Na kuhusu Mshafara wake kupokelewa huwa wakati mwengine anapokelea na Gavana wa sehemu hiyo au msaidizi wa Gavana, Meya na baadhi ya watu wa Usalama, Kwa ufupi kupokelewa Kikwete ni sawa na ndoa ya mkeka, shekhe na Mashaidi kwisha kazi, hakuna sherehe zozote zaidi ya kukaribishwa.
 
Hapa mkuu sio airport wala camp David panaonekana kama shopping mall vile maana kwa mbali namuona binti wa kithungu na mfuko wake kuonyesha katoka kupata mahitaji kwenye hiyo Mall

Ofisi nyingi za Serikali nchini Marekani zipo ktk mitaa ya kawaida tu. Chukulia mfano maeneo zilipo Wizara zetu. Hakuna kitu kipya hapa.
 
Nimekupata mkuu, lakini hapo kwenye Bold...kweli imewahitokea JK akapata escort ya mapikipiki 8 au 6 kama tufa
nyavyo hapa Bongo? Jamani mwenye picha ya mapokezi ya JK kuanzia airport za marekani hadi ikulu atuwekee hapa tuone.

JK hujipeleka US na hakaribishwi....akikaribishwa basi ni katika kundi la viongozi...ukikaribishwa huwa ni STATE visit na ndio hupigiwa mizinga
 
Mkuu,hapo kwenye bold jibu ni simple tu....kwanza nilitaka tu kujuwa hawa viongozi wa nchi za Africa wanapokelewa vipi
waendapo kwenye hizo nchi tajiri duniani,pili huwa ninajiuliza why Raisi wetu anakwenda USA mara kwa mara? So nikafiki
ria labda kinachompeleka huko ni mapokezi ya ki VIP kama kufungwa barabara,mapikipiki,magwaride,mizinga na misafara
ya magari hadi ikulu ya white house. Lakini kupitia uzi huu kunakitu naanza kujifunza...tuendelee mkuu

Kwa kuwa lengo lako ni kuelimishwa kupitia Jamvi hili, itakuwa vizuri zaidi kama utatufahamisha unachotaka kujua ili tuchangie hicho badala ya kuacha kila mmoja ahisi kile unachotaka kujua.
 
Mkuu,
Si marais wote wanaokwenda Marekani humwona Obama...wengine wanaenda kutibiwa..... wengine kwenye biashara zao binafsi..... wengine window shopping....NYC ni kitu ingine kabisa si kama Dar es Salaam tunapangwa barabarani kumpokea Mugabe!
Hapo kwenye bold ndipo paliposababisha mimi kuanzisha thread hii.
 
Umeona hao jamaa waliovaa suti na miwani myeusi...:hat:

Kwa kupitia picha hii inaonyesha kuwa Rais wetu alipokelewa na kupelekwa sehemu husika kwa msafara maana nitakuwa mjinga sana kama nitataka kuamini kuwa alipanda ktk magari yote tunayoyaona pichani
 
Kwa wingi wa trip za huyu jamaa nadhan kuna wakati ata izo protocol huwa hazifuatwi maana frequence ni kubwa as mnaweza acha mambo yenu ya msingi bure.
Nadhani kuna kipindi huwa anatelekezwa tuu la ndo ivyo anakomaa tuu
 
Jk yumo hum aje bas atupe infoya ukwel

Kwani kipi cha UONGO ktk mjadala huu hata umualike JK aje? Kwanza kabisa yeye huwa hapangi itifaki hiyo, yeye huwa anapangiwa na maofisa wa mambo ya nje wa Tanzania kwa kushirikiana na maofisa wa mambo ya nje wa nchi husika
 
Kwa kupitia picha hii inaonyesha kuwa Rais wetu alipokelewa na kupelekwa sehemu husika kwa msafara maana nitakuwa mjinga sana kama nitataka kuamini kuwa alipanda ktk magari yote tunayoyaona pichani

Umewahi kuuona msafara wa OBAMA? Gari nne tu na hakuna amabulance

George+Clooney+Images+Presidential+motorcade+bek6muIpdiHl.jpg
 
Back
Top Bottom