MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
- Thread starter
- #21
Kigeu geu....hukitaki ukiwa nacho ila ukiona kwamba mwingine anaweza kitaka/kitamani na kukichukua unataka urudishiwe.
Ubinafsi....wakati anakusema hufai anafanya vile kujifurahisha kwa kukufanya wewe ujione duni na sio kweli anavyokuona.Ndio maana anapoona mtu mwingine anafaidi anarudi mbio kulia "nimekosa...nimekosa."
Uroho....sikutaki pia nakutaka.Hawa ndo wale wanataka raha ya kuangalia chakula na kukila pia...kitu ambacho huwezi kuwa navyo viwili moja kwa moja....na kuchagua kimoja hawawezi.
Unyanyasaji....furaha yake inatokana na kuwafanya watu wengine waamini/wajione wao sio kitu.Anakuondolea/punguza kujiamini kwako ili uwe "Mwindwaji" mzuri.Unakua sehemu ya mchezo aupendao...akitaka kufurahi anakutapika...siku akiona vipi anakuweka mdomoni na sio anakumeza.Hapa kazi inabaki weka mdomoni...tema...weka..tema ikiwa utakubali kufanywa hivyo.
Kusema ukweli binadamu wengi kama sio wote tumeumbwa na roho ya wivu bila kuacha kigeu geu.Leo hii kuna mtu anaweza kutupa ndoo asioipenda sana kwasababu imepasuka ila kesho akimuona nayo jirani yake anavyoifurahia vaada ya kuichomea karoho kanamuuma na kutamani kwenda kudai ‘ndoo yake‘. Hivyo hivyo kwa wapenzi wakati mwingine mmoja anaweza kumuona mwenzake sio ‘hadhi yake‘...‘mchovu‘...‘mshamba‘...‘amefulia‘ n.k akamwacha kwa sababu hizo ila ikitokea yule mpenzi akakutana na mtu mwingine ambaye yeye ataenda mbali na kujaribu kumuinua na akabadilisha hayo/hicho kilichofanya aaachwe mwanzo lazima yule aliyeacha atamtamani huyu ex-mpenzi alikua upgraded na kuumwa roho kwamba "uzuri wote ule anafaidi/atafaidi mwenzangu?!SITAKI KABISA" Na ndio hapo usumbufu unapoanza maana all of the sudden unaonekana u-bora na sio choka mbaya anymore.
Lizzy umesema sawa kabisa yaani binadamu kweli tuna makuu
..................huwa tunajisahau kuwa tunapokiona cha nini huku twakunja uso na kuziba pua, kuna wengine wanajiuliza watakipata lini kishaufu kile chenye kunukia kama vikuba vya asmini!!