Hivi inakuwaje hujawahi kupanda ndege?

Nimeshagundua humu ndani kuna watu kibao hawajahi panda ndege wakiongozwa na Kongosho!
Hata vile vindege vya costal??..lol
 
Asante sana mkuu
Yaani utoto full
Unakumbuka enzi unarudi home unamtambia mtoto mwenzako kuwa umepanda gari
Sasa ndo hii amepanda ndege kwa mara ya kwanza anakuja kushangaa watu hapa kuwa hawajawahi kupanda ndege
duh na anategemea watu wajadili na kumsupport
ujue unanishangaza sana,unasema hutaki kuijadili hii post lakini una mchango karibu wa tatu katika thread hii,halafu uwe na tabia ya kujisemea nafsi yako,usipende kutumia neno WATU jizungumzie wewe mwenyewe,mbona watu kibao wamechangia au hao ni ng'ombe? swali liko wazi braza kaka,umeshawahi kupanda ndege?:poa
 
Safari zake zote zinaendeka kwa gari na usafiri mngine. Usiendekeze sana mambo ya ndege, ni carbon footprint mbaya sana.
Tuombe Mungu siku moja tuwe tunaenda hata ulaya kwa TGV!

tunaomba utupe darsa pana hapa ili tuelewe vizuri.
 
Kwa hiyo unaturingishia au unatutishia..Haya basi umepanda,,, kwa hiyo!!??????
 
kweli mkuu. mi mwenyewe hapa sijawahi panda ndege wala treni. hii thread imegusa maisha yangu. safi sana. hivi kweli inakuaje mtu unamaliza masomo ya secondary na chuo bila kupanda ndege? kuna ile kampuni ya ndege inapunguzaga bei kipindi cha valentine ngoja niwavizie. hivi zanzibar kuna kumbi za disco? nataka valentine nipande ndege niende zangu kucheza disco zenji, kesho yake nirudi tena na ndege ili hii thread yako ikose maana kwangu. Mia
fanya fasta sana mkuu,we usijali disco wala nini unaweza kwenda kununua samaki wa kitoweo na kurudi ili mradi tu uweke historia kuwa umemkwea mwewe.Mia
 
Back
Top Bottom