Hivi inakuwaje gari ya rais inachomoka tairi?

Rais wetu ni chaguo la Mungu ndio maana wachawi wanamloga sana.
Mara aanguke majukwaani, mara apigwe mawe kule Chunya, kila mkosi yeye.
Sisi wananchi tumemchoka, abaki yeye na huyo Mungu wake.
 
hakiyamungu huyu bwana nilishasema siku nyingi ameingiza wahuni ikulu,pale kuna watoto wa kijiweni watamtoa roho.kwanza ratiba hazina mpangilio,hotuba za kubumba,sasa kwenye tairi wakifika kwenye msosi mi sipo.2010 tutafute presdaa mwingine.

Yeah - tusisahau kesha dondoka majukwaani X2 na kulikuwa vigugumizi badala ya explanations za kuridhisha!
 
Ni dalili njema kuwa kuna watu wameshamchoka na hawamtaki kwa namna yoyote. Asome nyakati tu na kujua kuwa hatakiwi kwani akufukuzaye hakwambii toka.
 
Kibajaji changu kikichomoka tairi sio issue sitawasikia mkiongea ,hakuna haja ya tume hapa nadhani ni ajari kama zingine ..tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea
 
Guys don't be shallow!! JAMBO LA KAWAIDA kwa misingi ipi?? Hakuna hata siku moja nimeshawahi kupakia gari na TAIRI KUCHOMOKA na sijawahi pakia gari jipya au lenye sifa za uimara kama hizo vx v8!!
Watanzania lazima tunalaana si bure!!!
Gari ya kwanza aliyopakia raisi gia zilikataa kuingia (the last time I experinced this was in a landrover 109 ya mwaka 78) wakamtoa na kumuingiza kwenye ingine ambayo ikachomoka tairi, and some people think NI JAMBO LA KAWAIDA!!!
Dah and I thought JF ndio atleast kuna mchujo wa wenye akili kidogo from the rest, sasa wadanganyika wengine je!!
 
Guys don't be shallow!! JAMBO LA KAWAIDA kwa misingi ipi?? Hakuna hata siku moja nimeshawahi kupakia gari na TAIRI KUCHOMOKA na sijawahi pakia gari jipya au lenye sifa za uimara kama hizo vx v8!!
Watanzania lazima tunalaana si bure!!!
Gari ya kwanza aliyopakia raisi gia zilikataa kuingia (the last time I experinced this was in a landrover 109 ya mwaka 78) wakamtoa na kumuingiza kwenye ingine ambayo ikachomoka tairi, and some people think NI JAMBO LA KAWAIDA!!!
Dah and I thought JF ndio atleast kuna mchujo wa wenye akili kidogo from the rest, sasa wadanganyika wengine je!!

Nakwambia hatuna watu! wanasapoti mambo ya hovyo hovyo tu na ya kisengesenge -- eti ni kawaida! Ni laana kubwa sana iliyoletwa na CCM!
 
Inanikumbusha kisa cha mtu mwingine kusema gari limechomoka tairi.. hivi ingekuwa rahisi namna hiyo magari yangekuwa yanachomoka matairi kila kukicha.. na sasa linapokuja kuwa ni gari la Rais.. hivi ingekuwaje kama wangekuwa masafa marefu? kweli mngesikia gari limepata ajali na Rais yumo ndani halafu maelezo ni kuwa limechomoka tairi? Really? Gari la Rais ambaye ana ndege la bilioni 50? Hayo matairi yameshikishwa kwa gundi?

Kwa uzembe wa kupenda majibu mepesi mepesi mtakubali mkisikia ati ndege imeruka kufika angani wakagundua hakuna rubani na Rais yumo ndani halafu wakamshusha kwa parachuti iliyopasuka kwa sababu ilikuwa imechakaa!
 
Tanzania Daima ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, alikiri kutokea kwa matukio mawili tofauti yaliyosababisha rais alazimike kuhamishwa kutoka katika magari aliyokuwa amepanda. “Ni kweli matukio hayo yalitokea, katika tukio la kwanza gari alilopanda lilipata hitilafu baada ya gea kugoma kubadilika wakati katika tukio la pili, gari alilopanda lilipata pancha,” alisema Rweyemamu. Alipoulizwa kuhusu taarifa za gari la pili kung’oka gurudumu hata kusababisha kuitwa kwa gari la kubeba magari mabovu, Rweyemamu alikanusha habari hizo na akasema hazikuwa sahihi. “Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyopata rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika Jiji la Dar es Salaam?” alihoji Rweyemamu. Mwandishi wa habari hizi alimweleza Rweyemamu kuwa, gazeti hili liliona umuhimu wa suala hili kwa kuwa lilikuwa likigusa usalama wa kiongozi mkuu wa nchi moja kwa moja. Jibu hilo lilisababisha Rweyemamu amuombe mwandishi afuatilie kuhusu ukweli wa taarifa hizo na ndipo baada ya muda usiozidi dakika 30 alipiga simu chumba cha habari na kulihakikishia Tanzania Daima kuwa hitilifu za magari alizokabiliana nazo Rais Kikwete zilikuwa ni za kawaida.

Kama kuna mtu wa kwanza kufukuzwa kazi pale Ikulu anapaswa kuwa huyu jamaa Salva ambaye kwake yeye anaona gari la Rais wa nchi kupata hitilafu barabarani si jambo muhimu! Hatuombi, lakini iwapo gurudumu lile lingelichomoka wakati Rais akiwa ndani ya gari hilo na iwapo magari ya msafara wa Rais yangelikuwa kwenye mwendo mkali kama ilivyo kawaida nini kingetokea? Hayo yote Salva haoni kwamba ni muhimu.

Salva anachoona muhimu ni ziara ya Rais kwenda kukagua ‘adha ya maji’ ambayo imekuwepo tangu Rais aingie madarakani na katika kipindi cha miaka 4 hao wasaidizi wake hawajamshauri hata mara moja akakague chochote hapa Dar! Tena walipaswa kumshauri akakague adha hiyo alipoingia madarakani maana adha hiyo si ya jana wala juzi. Lakini, wamemshauri aende kukagua sasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi. Bila shaka Salva anayeona ukaguzi huo ni muhimu kuliko usalama wa Rais ndiye aliyemshauri Rais afanye ziara hizo zisizo na tija. Ziara kama hizo katika kipindi kama hiki zinamuumbua Rais aonekane kama anataka kuwadanganya wananchi kuwa anarekebisha mambo kumbe sivyo. Wananchi wanabaki kushangaa na kukejeli.

Salva, you should do better than that! After all REDET na Sheikh Yahya wamewahakikishieni ushindi wa kishindo - Why worry?
 
Inanikumbusha kisa cha mtu mwingine kusema gari limechomoka tairi.. hivi ingekuwa rahisi namna hiyo magari yangekuwa yanachomoka matairi kila kukicha.. na sasa linapokuja kuwa ni gari la Rais.. hivi ingekuwaje kama wangekuwa masafa marefu? kweli mngesikia gari limepata ajali na Rais yumo ndani halafu maelezo ni kuwa limechomoka tairi? Really? Gari la Rais ambaye ana ndege la bilioni 50? Hayo matairi yameshikishwa kwa gundi?

Kwa uzembe wa kupenda majibu mepesi mepesi mtakubali mkisikia ati ndege imeruka kufika angani wakagundua hakuna rubani na Rais yumo ndani halafu wakamshusha kwa parachuti iliyopasuka kwa sababu ilikuwa imechakaa!

Maelezo yako yameniacha natabasamu .
 
Kikwete chupuchupu

na Juma Kasesa (Tanzania Daima)

RAIS Jakaya Kikwete amenusurika kupata ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kulegea gurudumu na kisha kung’oka muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kuteremka katika gari hilo kwa dharura wakati akiwa ziarani jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9:15 katika Barabara ya Kilwa maeneo ya karibu na zilipo ofisi za makao makuu ya kampuni ya mafuta ya BP.

Kabla ya tukio hilo, msafara wa Rais Kikwete ulisimama ghafla na rais akahamishwa kutoka katika gari hilo aina ya Land Cruiser VX na kwenda katika gari jingine.

Watu walioshuhudia tukio hilo walilieleza Tanzania Daima kuwa, muda mfupi baada ya msafara wa rais kuendelea na safari, dereva wa gari alilohama rais alijaribu kulisogeza pembeni ya barabara, hatua iliyosababisha gurudumu la gari hilo kung’oka na kusababisha ligote chini upande wa mbele kulia.

Tukio hilo liliwashtua watu waliokuwa katika eneo hilo, ambao walianza kujadili ni nini kingetokea iwapo gurudumu hilo lingeng’oka wakati rais akiwa ndani ya gari hilo.

Mwandishi wa gazeti hili aliyekuwapo eneo la tukio alieleza hatua hiyo ilisababisha kuwasili katika eneo hilo kwa gari maalum la kubeba magari mabovu maarufu kwa jina la ‘breakdown’.

Tukio hilo la rais kulazimika kuhama kutoka katika gari alilokuwa amepanda lilikuwa ni la pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza akiwa katika maeneo ya Kimara Mavurunza.

Kikwete alikuwa katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi ya maji jijini Dar es Salaam.

Msafara huo ukiwa unaondoka Kimara ulisimama ghafla na kuzua taharuki kwa maofisa usalama na wananchi baada ya kuona Rais Kikwete akishushwa ndani ya gari alilokuwa amepanda na kuingia katika gari jingine baada kupata hitilafu huku mvua kubwa ikinyesha.

Tukio hilo la rais kushushwa katikati ya barabara ya Morogoro katika eneo hilo, lilichukua dakika nane na kusababisha msongamano wa magari kabla ya msafara huo kuruhusiwa kuendelea kuelekea Chang’ombe Toroli ambako alikuwa akienda kukagua mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na mashirika ya maji Dar es Salaam.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, alikiri kutokea kwa matukio mawili tofauti yaliyosababisha rais alazimike kuhamishwa kutoka katika magari aliyokuwa amepanda.

“Ni kweli matukio hayo yalitokea, katika tukio la kwanza gari alilopanda lilipata hitilafu baada ya gea kugoma kubadilika wakati katika tukio la pili, gari alilopanda lilipata pancha,” alisema Rweyemamu.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za gari la pili kung’oka gurudumu hata kusababisha kuitwa kwa gari la kubeba magari mabovu, Rweyemamu alikanusha habari hizo na akasema hazikuwa sahihi.

“Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyopata rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika Jiji la Dar es Salaam?” alihoji Rweyemamu.

Mwandishi wa habari hizi alimweleza Rweyemamu kuwa, gazeti hili liliona umuhimu wa suala hili kwa kuwa lilikuwa likigusa usalama wa kiongozi mkuu wa nchi moja kwa moja.

Jibu hilo lilisababisha Rweyemamu amuombe mwandishi afuatilie kuhusu ukweli wa taarifa hizo na ndipo baada ya muda usiozidi dakika 30 alipiga simu chumba cha habari na kulihakikishia Tanzania Daima kuwa hitilifu za magari alizokabiliana nazo Rais Kikwete zilikuwa ni za kawaida.

Akiwa katika ziara hiyo jana, Kikwete alishuhudia wananchi wakiwabana kwa malalamiko na wakati mwingine kuwazomea maofisa watendaji wa Shirikika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) na Mamlaka ya Maji Safi jijini Dar es Salaam (DAWASA).

Kufuatia hali hiyo ya kuzomewa katika eneo la Kimara, Rais Kikwete na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya kwa nyakati tofauti walilazimika kuingilia kati na kutoa ufafanuzi kwa wananchi waliokuwa wakiwabana kwa maswali maofisa hao wa Dawasa na Dawasco.

Ofisa Mtendaji wa Dawasco, Alex Kaaya na Archad Mutalemwa wa Dawasa walikumbana zahama hizo baada ya diwani wa kata hiyo kuanika kero ya upatikanaji wa maji inayowakabili kwa muda mrefu na hivyo kumlazimu Rais Kikwete kuwataka watoe majibu.

Ziara hiyo ilianzia kwa Kikwete kutembelea Makao Makuu ya Dawasco ambapo alipata fursa ya kupata maelezo ya utendaji wa mashirika hayo kuhusu kero ya upatikanaji maji jijini Dar es Salaam.

Akiwa hapo alielezwa na maofisa hao hatua zilizochokuliwa na mashirika hayo katika kuondoa kero hiyo kwa kuanzisha miradi wa uchimbaji visima, ikiwamo kuhakikisha wanavikarabati vyanzo vya maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuondoa tatizo hilo.

Kaaya alisema tatizo linalosababisha kero ya maji jijini ni uchakavu wa miundombinu, upotevu wa asilimia 50 ya maji, njiani na miundombinu iliyokuwapo sasa kutoendana na ongezeko la idadi ya watu.

Alisema miundombinu iliyopo ilijengwa mwaka 1976 na ilikuwa inatosheleza kwa wakati huo tofauti na sasa ambapo Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wanaofikia milioni saba.

Naye Mutalemwa akitoa ufumbuzi wa tatizo la maji jijini, alisema wanatarajia kuanzisha mradi wa uchimbaji visima Julai mwaka huu, na kubainisha kuwa wamejipanga ifikapo mwaka 2013 tatizo la maji liwe limekwisha jijini.

Aidha, akiwa hapo, Rais Kikwete alimnyanyua Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi na kumtaka aeleze kwa nini jiji linakabiliwa na uchafu, ambapo alizitupia mpira halmashauri kuwa ndizo zenye dhamana ya kuondoa uchafu na yeye hana mamlaka ya kuziagiza kusimamia.

Kauli hiyo ilionekana kumuudhi Rais Kikwete na kumuuliza Kingobi anataka apewe mamlaka gani ili aweze kuzisimamia halmashauri hizo na kumfanya mkurugenzi huyo kubakia kimya pasipo na majibu.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliagiza kujengwa kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Mavurunza hadi Segerea ili kupunguza kero ya usafiri.

Baada ya ziara hiyo, Rais Kikwete alikutana na viongozi wa Jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee na kuwataka kusimamia ipasavyo majukumu waliyopewa.

Jana alipita barabara za mashimo ambazo zinaharibu magari yetu kila siku kutokana ubovu wa barabara ambao unasabibiswa na utawala wake kutosimamia/kutotenegeza matengenezo ya barabara. Huo ni mfano wa magari ya walala hoi yanavyoharibika
 
Nashukuru kwa michango yenu,mengi mliyoyaongea nitayafikisha kwa wahusika na watayafanyia kazi.
 
Nakwambia hatuna watu! wanasapoti mambo ya hovyo hovyo tu na ya kisengesenge -- eti ni kawaida! Ni laana kubwa sana iliyoletwa na CCM!

hatusupport hata kidogo hili neno naona kama sio Lugha fasaha ya Kitanzania kaka Zak
 
Inanikumbusha kisa cha mtu mwingine kusema gari limechomoka tairi.. hivi ingekuwa rahisi namna hiyo magari yangekuwa yanachomoka matairi kila kukicha.. na sasa linapokuja kuwa ni gari la Rais.. hivi ingekuwaje kama wangekuwa masafa marefu? kweli mngesikia gari limepata ajali na Rais yumo ndani halafu maelezo ni kuwa limechomoka tairi? Really? Gari la Rais ambaye ana ndege la bilioni 50? Hayo matairi yameshikishwa kwa gundi?

Kwa uzembe wa kupenda majibu mepesi mepesi mtakubali mkisikia ati ndege imeruka kufika angani wakagundua hakuna rubani na Rais yumo ndani halafu wakamshusha kwa parachuti iliyopasuka kwa sababu ilikuwa imechakaa!

Umenivunja mbavu. kina salva wangesema ni kitu cha kawaida.
 
Mie naona jama nao wameanza kufanyakazi kwa kuiga style yake ya mizaha mizaha hata katika mambo very serious ndio maana wanafanya mzaha na maisha yake.
 
Tuache kukuza mambo jamani. Hata ukiwa unacheki gari ya Rais kwa kiwango gani, bado huwezi kuondoa possibility ya gari kukorofisha. Hizo ni mashine tu jamani......!!

Binafsi naamini hii kitu inaweza kutokea, na ndo maana kwenye misafara ya Rais kunakuwa na gari ya dharula ili ikitokea gari anayotumia imekorofisha Rais anahamia kwenye gari nyingine na safari iinaendelea!!!
 
Alipoulizwa kuhusu taarifa za gari la pili kung’oka gurudumu hata kusababisha kuitwa kwa gari la kubeba magari mabovu, Rweyemamu alikanusha habari hizo na akasema hazikuwa sahihi. “Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyopata rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika Jiji la Dar es Salaam?” alihoji Rweyemamu.

Stupid answer on sensitive issue. Are these people really aware of their responsibilities? Kweli serikali imeingiliwa na washikaji wa Rais na kila kitu kinafanyika kishikaji. Ni kama amepewa habari gari la mshikaji wako limepata breakdown lakini halijaumia wala yeye hajaumia. Kwani hizo adha hamkuzijua siku zote? Sasa mbona hausemi hiyo barabara iliyojengwa usiku usiku nayo siyo adha?
 
Back
Top Bottom