Hivi ilani ya JK na chama cha magamba (CCM) inatekelezeka!?

JOENVA

New Member
Jan 14, 2011
3
0
kwa mujibu wa takwimu ambazo zilipatikana wakati wa kampeni za uchaguzi uliomalizika kwa jk kuambulia 61% baada ya uchakachuzi, ilisemekana kuwa ahadi za ccm zilifikia thamani ya fedha za tazania zaidi ya trilioni 90. Ukipiga mahesabu ya haraka haraka, bajeti ya tanzania kwa mwaka sio zaidi ya trilion 12. Ukizidisha 12x5 (miaka yake ya uongozi, kama atabahatika kumaliza) unapata trilion 60. Kati ya hizo zote, bajeti ya matumizi ya kawaida ni zaidi ya % sabini, yaani 60 x70/100 = 42.5 t zinatumika kwa ajili ya kuendesh serikali, posho, safari za nje na ndani za mawaziri, takrima na mishahara. Kwa hesabu fupi tu, ni kiasi cha 17.8 t ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kipindi chote cha uongozi wake uliobaki. Hizo meli katika maziwa yote, hivyo viwanjavya ndege karibu kila mkoa, hizo hospitali za rufaa hadi kwenye kata, hizo bajaji kila zahanati, hizo wilaya na mikoa mipya iliyoanzishwa na takataka za ahadi za papo kwa papo ambazo zingine hata haziurekodiwa, zinatekelezwa kwa mtindo fedha kutoka wapi? Hebu nisaidieni, maana kila nikifikiria kwa kina, naona jamaa aliahdi kwa sababu alijua hakuna ambaye atamuuliza tena, si anamaliza. Na hata haya maamuzi ya kuwafukuza ra, ac na el, nafikiri msingi wake ni "tukose wote" kama ilivyokuwa kwenye uspika.
 
Back
Top Bottom