Hivi huyu mwanajeshi ana umuhimu gani?

... Kwa kuiwa Rais wa Tz ndiye Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Majeshi yote..huyo Jamaa hapo Nyuma anambebea Rais vyeo vyake vyote ndio maana unaona ana vyeo vya ki-polisi, jeshi, jeshi la Maji na La Angani..
 
halafu mbona yupo kwa rais wa tanzania tu?.....mbona marais wengine (pia wa africa) hawana njemba kama hiyo?

pia huyu jamaa ni body guard? ni JWTZ? ni UWT? (sio umoja wa wanawake tanzania, kwa wale ndugu zetu wapya) au yupo kwa masuala ya ki ceremony zaidi? ...

Maana kwenye hizo picha yupo peke yake.....ukiacha ile ya conference ya HIV/AIDS...halafu cha ajabu kwenye hiyo conference ndio wapo wengiii....sasa sijui wanahusikanaje na HIV/AIDS
 
mi hofu yangu ni kuwa kofia ya huyo riafande inafunika hadi macho yake...sasa mtu kama ana sniper juu ya paa atamuona kweli???manake ukisikia paaaaa!!! ujue imekukosa
 
yaaah namaanisha hivyo .....hili riafande rikisia paaaaaaaa!!!ujue imemkosa,na imeenda kwa mkwere!!!!kazi kwerikweri hapa
 
Uwepo wa huyo mjeshi ni ishara tu kwamba dola ipo na siyo kwamba ndiye anayetegemewa kwa kila kitu katika ulinzi halisi wa Mkuu wa Nchi. Wenyewe wapo na huwezi kuwajua kwa kuangalia hivyo wajameni.

Mkuu: Kama kweli wapo na wanafanya kazi, ilikuwaje siku ile wamwache JK mpaka anadondoshwa na upepo Jangwani? Hivi haya mambo ya ishara yapo kwetu tu? Manake nimejaribu kutazama sana marais wengine lakini hizo ishara hawazitumii, hata Marekani, Russia, Uingereza nk,, viongozi wao hawana ishara kama hizi, na ndiyo wanasifika kwa ulinzi wa viongozi wao kuliko sisi wana-ishara...

TANMO.....samahani sana inaelekea wewe mwenyewe au jamaa yako wa karibu alikuwa akiwania nafasi hiyo na kuikosa....matokeo yake mwamwangushia kejeli...? mlikuwa wapi 6 yrs ndo muone sasa....?
ENDELEA BABA TENA IKWEZEKANA BADILI NA SARE UVAE ZILE ZA YANGE YANGE...!

Mkuu: Kumbe hii nafasi huwa inawaniwa? Sijawahi kuihitaji mkuu wala ndugu zangu hawajawahi...

Naombeni mnisaidie kidogo, hivi mvuto wa sura ndio unalinda au ni nini? maana naona kama tunajichanganya! Na Mh. Raia tangu lini anabeba mafaili jamani hebu tuwe wazi, hebu nenda pale polisi ushuhudie IGP na Makamishna wake wanavyofungliwa milango na kubebewa bag zao. Si polisi tu, wapo wengi tu, sasa kwa Rais si zaidi jamani, hebu tuwe realistic katika mambo mengine bwana

Hata kama si rais anayewajibika kujibebea mafaili, basi kumtumia huyu Bwana ambaye inasemekana yupo kama ishara ya umadhubuti katika kumlinda rais, ni makosa zaidi. Angalau wangemtumia mtu mwingine kuifanya hiyo kazi. Hebu jiulize, ikitokea jambo litakalomlazimu kutumia mikono kumwokoa rais ilhali wakati huo huo amebeba mafaili si itambidi ashike moja aache moja? Atashika lipi basi kwa wakati huo? Isitoshe huwa tunaambiwa msafara wa Rais huambatana na watu kibao, hao wengine huwa ni wa kazi gani basi kama hata wa kubeba mafaili hayupo?


Hapa akimtengenezea koti Bwana Mkubwa..
titled.jpg
 
Huyo ni Mpambe or Katibu Myeka kitu kama hicho, ila kuna kikosi cha ulinzi cha Rais
 
ignorance is not an individual's fault. Wana jf mliopitia jkt nisaidieni huenda nimesahau, lakini nakumbuka mojawapo ya masomo ya nadharia yaliyokuwa yakifundishwa ni pamoja na mambo ya intelligence (usalama wa taifa). Uwepo wa huyo mjeshi ni ishara tu kwamba dola ipo na siyo kwamba ndiye anayetegemewa kwa kila kitu katika ulinzi halisi wa mkuu wa nchi. Wenyewe wapo na huwezi kuwajua kwa kuangalia hivyo wajameni. Penye ukweli tuwe wawazi, ingekuwa hivyo basi viongozi wengi wangekuwa wanarestishwa in peace shaghalabaghala tu. Hiyo ni taaluma ya aina yake tulione hilo.
i agree with u 100%
 
Mkuu hapo umekuwa biased, huyo mjeshi kaonekana ni mrefu kwa sababu Mkapa ni mfupi sana. Mlinganishe na hao wakoloni ndiyo useme.

Pamoja na hayo ni mrefu na smart kuliko huyu wa sasa...hampambi kabisa Rais ilhali yeye ni mpambe
 
huyo jamaa kazi yake si "aid n confidant" wa raisi.. kama raisi ndio mkuu wa nchi, including the army, huyo jamaa hauzi sura tu, yeye ndio mshauri wa jeshi kwa mzee mzima
 
Mkuu: Kama kweli wapo na wanafanya kazi, ilikuwaje siku ile wamwache JK mpaka anadondoshwa na upepo Jangwani? Hivi haya mambo ya ishara yapo kwetu tu? Manake nimejaribu kutazama sana marais wengine lakini hizo ishara hawazitumii, hata Marekani, Russia, Uingereza nk,, viongozi wao hawana ishara kama hizi, na ndiyo wanasifika kwa ulinzi wa viongozi wao kuliko sisi wana-ishara...



Mkuu: Kumbe hii nafasi huwa inawaniwa? Sijawahi kuihitaji mkuu wala ndugu zangu hawajawahi...



Hata kama si rais anayewajibika kujibebea mafaili, basi kumtumia huyu Bwana ambaye inasemekana yupo kama ishara ya umadhubuti katika kumlinda rais, ni makosa zaidi. Angalau wangemtumia mtu mwingine kuifanya hiyo kazi. Hebu jiulize, ikitokea jambo litakalomlazimu kutumia mikono kumwokoa rais ilhali wakati huo huo amebeba mafaili si itambidi ashike moja aache moja? Atashika lipi basi kwa wakati huo? Isitoshe huwa tunaambiwa msafara wa Rais huambatana na watu kibao, hao wengine huwa ni wa kazi gani basi kama hata wa kubeba mafaili hayupo?


Hapa akimtengenezea koti Bwana Mkubwa..
View attachment 23751
Umeeleweka mkuu, kumbe issue si kubebewa mafaili, bali ni nani anambebea hayo mafaili, kweli kukitokea issue itabidi aweke kwapani faili kwanza akirudi kwa mhe itakuwa too late!!!!!!!!!!!!
 
Kuna thread ilikuwepo hapa ya walinzi wa viongozi mbalimbali duniani ilielezza vyema kazi za huyo jamaa, mikoba, positioning, nk. huyo unayemuona ni mmoja tu na ana kazi yake

tunaweza tusimpende JK au rangi ya kijani lakini nadhani kuna haja ya kurejea hata kwenye mitandao kujua nini tunataka kuwakilisha aisee
 
Siamini kabisa kwamba yupo kwa sababu za kiusalama.Na kama yupo kwa sababu hizo basi alisha-prove failureRejea tukio la Janngwani.View attachment 23710Hapa kabebeshwa mafaili kabisa, sasa likitokea la kutokea atalinda mafaili au atafanya kumuokoa ******?View attachment 23711View attachment 23712Hapa tena, marais wengine wote hawana walinzi nyuma yao, ****** tu...View attachment 23713View attachment 23714Hapa tumuweke kwenye kundi la viongozi au?Manake amejumuika kabisa na viongozi wa kitaifa na wame-form mstari kabisa.View attachment 23715Hapa sijui anatekeleza Protocala au analinda?View attachment 23716Hapa sijui analinda nini..Besides, ni mfupi zaidi ya Object yake, kiasi kwamba haoni mbele ya JK kuna nini. Sasa hapo atamlindaje?View attachment 23717Inawezekana yupo kwa ajili ya kubeba mafail ya ******? Hayo mafaili yana uzito gani kiasi cha kumshinda ****** mwenyewe kubeba?Au, tumtofautishe vipi ****** na mamwinyi. Kuna hata clip niliona jamaa akimrekebishia koti ****** wakati ****** akimwaga upupu wake kwa waandishi wa habari... Inakera!!!Yaani kama ni utaratibu tu wameuweka, huyo jamaa anaharibu sana pozi..
hahahahaaaaaa, hiyo ya kubeba mafaili noumaaaa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom