Hivi huyu alinipenda kweli?

Yuko wapi huyo nimpe mkono wa pongezi hata ingekua mi ningefanya hivyo, imagine kwa asili na tamaduni zetu ilivongumu kwa mwanamke kutamka live kuwa amefall af ukamshusha zaid kukataa, u deserve hicho anachokufanyia
 
huyu kweli ni wa kutiwa moyoni! kutongoza hawezi akitongoza anaringa... jipange upya hiyo kibarua ilishaacha majani!

Sio kutongoza siwezi bali ni ule urafiki uliokuwa hapo mwanzo ndio uliweka barrier!Hivi hujawahi kuwa na rafiki wa kike mmezoeana saaana!?
 
Nimekushangaa sana.. Unajua huyo dada mpaka kukwambia kama anakupenda ni kwamba alivumilia akashindwa ndio maana akaamua kupasua jipu... Sasa wewe unadhani alijisikiaje ulivyomkatalia?? Nahisi ameshapata anayempenda maana wewe ulimtolea nje..
 
  • Thanks
Reactions: LD
Ha ha ha hii topic imenichekesha balaa.....WAnaume bwana wananichekesha sana, unaweza ukampenda kweli, yani kweli kweli, na kwa kuwa ni rafiki yako unajua unakuwa umemzoea, yani kuna vihistoria na vistori ambavyo vinawaunganisha, achilia mbali hisia za kimapenzi.

Sasa kwa mdada ambaye ni muwazi na anapenda kuongea anaweza akajikuta tu anasema halafu unajua mi nakupendaga, tena nakupendea hiki hiki na hiki. Kama utani lakini kweli. Na ujue kwa hakika mdada aliyekuzoea akitamka hilo neno ujue amemaanisha sana. Kipo moyoni hicho kitu...Moyo unampasuka.

Wanaume sasa, looh huyu demu ananitaka, na kwenye vijiwe vya bia akifika stori ndiyo hiyo, analishwa humo weeeeh, demu atakutokea je wewe, kwanza yule demu hivi na hivi, makasoro kibao mnamtoa......Ukitoka hapo kumbe limoyo linakuuma NAMPENDA huyu dada lakini................he he he

Ujue msichana anapokuambia hivyo we unajifanya kumpotezea, anaumia, anajistukia, anajisikia vibaya sana....Hivi mimi kwa kwa nini hata nimemwambia, hivi kanionaje, loooh nimkimbie au nifanye nini, nitathubutu kuongea naye tena? Na mengine kibao yanamsumbua kiakili, kiroho na kimwili. Kwa sababu hakutegemea awe na ujasiri na uhuru kiasi hicho kwako halafu akutane na hicho ulichompatia.

Sasa basi kinachofuata baada ya hayo yote.....anajitahidi kuikataa ile hali, nakujisahaulisha. Kwa nguvu sana, hata kwa machozi. Siku akisema It's OVER...To hell........kwani yupo peke ake? Ndio basi, amefanya maamuzi magumu, na kwa bahati mbaya atokee mtu amuonyeshe upendo..........WE UNAKUJA KUSTUKA...unaona manyoya.

Acheni usharobaro..............Angalia maisha katika uhalisia wake kutoka kwenye huo uhalisi kuliko kawaida kawaida hii....na huu u-artificial artificial tunauwekaga kwenye maisha....................TUTAPOTEZA VILIVYO VYEMA
 
Nimekushangaa sana.. Unajua huyo dada mpaka kukwambia kama anakupenda ni kwamba alivumilia akashindwa ndio maana akaamua kupasua jipu... Sasa wewe unadhani alijisikiaje ulivyomkatalia?? Nahisi ameshapata anayempenda maana wewe ulimtolea nje..

Ana safari ndefu yakumuaminisha huyu dada kwamba kile alichomwambia hakikuwa kosa.............:A S-rose::A S-rose:
 
duh..miezi 2 umempiga chenga?!!,...dnt u thnk alifikiria mengi sana during those 2months..am sorry lkn sh hs decided to move on,hatakama anakupenda ye anaona bora aendelee na maisha yake tu...kama si hvyo basi na wewe usubiri miezi 2/3 uone niaje niaje.....koma kuringa...hahahahaa,pole lakini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom