Hivi huyu alinipenda kweli?

The_Emperor

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
871
125
Kwanza kabisa niwasalimu wote na poleni na majukumu ya kujenga taifa letu;Nilikua na rafiki yangu wa kike,nilimpenda kweli awe mpenzi wangu ila sikuwahi kumwambia kwa kuwa tulikuwa tumezoeana sana sana kama marafiki wa kawaida!Basi sikujua kumbe na yeye alikuwa na hisia kama zangu,kwa mdomo wake akawa ameniwahi kuniambia amefall in love na mimi;Ila mimi kwa ujinga wangu nikajifanya kama nilikua sina wazo la kuwa naye;Basi nikawa namchenga kama miezi 2 ingawaje nilikua nampenda siku zote hizo!Cha ajabu baada ya kipindi hicho nikamwambia sasa tunaweza kuanzisha mahusiano;Alichonijibu sikutegemea,alisema kwa kujiamini"We can be just friends"Nilibembeleza na kutoa machozi mtoto wa kiume lakini wapi!Mpaka sasa umepita mwezi1 na sioni mabadiliko!Je,huyu msichana alinipenda kweli?
 
pamoja na kuchelewa kumtongoza bado ulidengua, na wewe subir hyo miez miwili labda anataka kurevenge!
 
The_Emperor unajifanya sitaki nataka sasa amejikamatia buzi jingine
 
Kwanza kabisa niwasalimu wote na poleni na majukumu ya kujenga taifa letu;Nilikua na rafiki yangu wa kike,nilimpenda kweli awe mpenzi wangu ila sikuwahi kumwambia kwa kuwa tulikuwa tumezoeana sana sana kama marafiki wa kawaida!Basi sikujua kumbe na yeye alikuwa na hisia kama zangu,kwa mdomo wake akawa ameniwahi kuniambia amefall in love na mimi;Ila mimi kwa ujinga wangu nikajifanya kama nilikua sina wazo la kuwa naye;Basi nikawa namchenga kama miezi 2 ingawaje nilikua nampenda siku zote hizo!Cha ajabu baada ya kipindi hicho nikamwambia sasa tunaweza kuanzisha mahusiano;Alichonijibu sikutegemea,alisema kwa kujiamini"We can be just friends"Nilibembeleza na kutoa machozi mtoto wa kiume lakini wapi!Mpaka sasa umepita mwezi1 na sioni mabadiliko!Je,huyu msichana alinipenda kweli?

....mpe mwezi huyo naye kwake itimie miwili,...."ukuti, ukuti, wa nazi wa nazi...."
 
  • Thanks
Reactions: LD
mwanaume haringii, kisa cha kumdengulia miezi miwili mwenzio wakati unamjua tabia yake vizuri mana ni best friend wako!! ngoja na yeye akuringie double yake 4 mothz hahaha
ila usichoke kusubiri hio ni kawaida tu
 
ulimdengulia....
Akakubaliana na hali halisi....
Akakufuta moyoni......

Hesabu umeumia....
 
lol! ndio nimesikia leo kama wanaume nao huwa wanadengua! kha! haya endelea kusubiri na usubiri haswaaaa, wenzio wamalize mpaka firigisi, we uje umalizie juice ya utumbo tu!
 
Pozi mbaya jamani..mwanamke akipenda amependa...unaleta poz..akibembelezwa kidogo kwingine..umekwisha..atahamishia mapenzi yoteeeee huko....mpaaka akusahau..:A S-rose:.
 
ulibeep umepigiwa walalama nin? kudengua si kipimo cha penz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom