hivi huu mkonga wa mawasiliano wa taifa unafanya kazi?

BGG

Senior Member
Apr 5, 2012
134
15
Hivi huu mkonga wa taifa umeshaanza kufanya kazi? Habari za mitaani ni kuwa unafanya kazi kupitia TCCL, kama habari hizo ni za kweli, basi mkonga wetu wa taifa la tanzania umechakachuliawa.kwani speed na uwezo wa internet zilizopo haziwezi kufanya kwa ufanisi yale tunayoyategemea. Km : telemedicine nk naomba kusaidiwa kujua mustakabali wa huduma za mkonga huu kama zipo, zinafanya kazi na je zinafanya kwa ufanisi na ni jinsi gani ya kuzipata kama zinafanya kiufanisi?
 
kulitokea matazizo meli ilizikata cables kwa bahati mbaya.muda si mrefu kilakitu kitakuwa shwari.
 
Imetokea lini? Maana hata modem zinazotumia mitambo ya simu za mkononi km airtel hazina speed na leo tumepewa 'error 502' vinahusiana?
 
Inategemea unamaanisha nini, mkonga upo ila kuusambaza nchi nzima ndo kazi inayoendelea sasa hivi. Pia Rwanda haujapitia kwetu umepitia Kenya --> Uganda, baada ya kutuona sisi wababaishaji.

Mkonga hauifanyi spidi kuwa mzuri automatically, makampuni ya simu inabidi yanunue capacity na hiyo ni gharama kubwa.
 
asante sana kwa taarifa, hizo capacity ndiyo bandwith? Zinauzwa na ttcl? Na ofisi yenye kompyuta ishirini hivi inatakiwa kununua kapacity kiasi gani?kavit
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom