Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 2,425
- 2,113
[QUOTE=Ntemi Kazwile;1586048]Mkuu,
Hapa kuna shida kubwa, kama mimi sipendi ushoga siwezi kuwa wakili wa kutetea mtu anamshitake mwenzake kwa kumwita shoga! Hata kama ni kazi yangu kutetea watu watendewe haki, nikifanya hivyo nitakuwa napingana na dhamira yangu ya kupinga ushoga na wala sitaweza kumtetea ipasavyo kwa sababu nafsi yangu inataka nimzomee huyo shoga ili aache ushoga sasa nitawezaje kumtetea asizomewe??
Marando anatuzuga huyu wala siyo jemedari wa kupinga ufisadi. Mbona sijawahi kumsikia Lisu akiwa wakili wa hao mafisadi?[/QUOTE]
Ndugu Mtemi,
Tufanye kwamba ungekuwa "criminal lawyer", je ungekuwa unatetea watu wa namna gani? wezi, wauaji, wabakaji? maana hao wote ungewachukia, ina maana basi ungeacha kazi ya uwakili.
Kumbuka kuwa hawa akina manji, na wengine wengi wanaotajwa kwenye media, kisheria ni watuhumiwa tu, na mahakama haijathibitisha kama wametenda makosa hayo. Kwa hiyo ukiwa kama wakili unawatetea watuhumiwa ukiwa na assumption kuwa "they are innocent". Ni jukumu la waendesha mashitaka (serikali) kuthibitisha mahakamani kuwa hawa watuhumiwa kweli wametenda hilo kosa. Kusipokuwepo mawakili wa utetezi,kila mtu anaweza kubambikizwa kesi.
Pia ufahamu kuwa mawakili wote ni sehemu ya mahakama, wao ni "officers of the court" wanatakiwa kuhakikisha kuwa mahakama inatenda haki. Na kila mtu awe fisadi, mwizi, muaji, shoga, wote wana haki zao kikatiba na kibinadamu. Wakili yuko pale kuhakikisha haki ya mtuhumiwa haivunjwi.