hivi hii inakuaje? whats up with security group???

serio

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
7,306
4,681
kuna ndugu yangu mmoja alipata kazi security group na huu ni mwezi wake wa pili kazini. anadai kwamba wanafanya kazi masaa (8) na overtime ya masaa manne(4) kwa siku. cha kushangaza, wameambiwa hawatapewa hela ya overtime kwa miezi minne ya kwanza kazini. hela ya overtime inasiniwa kwamba wamelipwa lakini hawapewi sababu kuu ikiwa, "wako kwenye miezi ya mtazamio"
Istoshe, ukipata tatizo kazini, kampuni haikupi msaada wowote ule, uwe polisi, jela au wapi, they dont want to know. na bila kuonekana kazini ndani ya siku tatu, huna kazi.
kwa mfano.. kuna laki tano zilipotea katika benki moja hapa mjini.(pesa zilipotelea ndani kwa teller), cha kushangaza walinzi (waliokua nje) ndio walikamatwa na kupelekwa polisi. walikaa ndani wiki mbili mpaka walinzi wenzao wa security group wakachanga changa 120,000/= kuwatolea dhamana.. kampuni haikushughulika nao, na sasa hawana kazi.
ndugu zangu, maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana kwa hali hii????
 
Hiyo ya kufika kazini siku 3 na kufukuzwa ni sheria ya kazi sio ya security group ila nayo inasisitiza kutofika kazini bila taarifa yoyote na bila sababu za msingi
 
Hiyo ya kufika kazini siku 3 na kufukuzwa ni sheria ya kazi sio ya security group ila nayo inasisitiza kutofika kazini bila taarifa yoyote na bila sababu za msingi

sawa, na hiyo ya overtime imekaaje?
 
naonna kuna uhuni hapa...ila kwani kavla hawajaingia kazini hwakusaini mkataba??
masharti ya mkataba yanasemaje??
 
yaani overtime inapitishwa lakini wafanyakazi hawapewi so hiyo hela inaishia wapi....wote wezi...na hela iibiwe kwenye till yeye mlinzi anahusika vipi wakati ukute hana access kabisa ya hao teller waliko..kuiba waibe wengine jela walale wengine ndio bongo hiyo
 
Back
Top Bottom