Hivi hawa wa Dume Challenge Vipi?

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Niko mbele ya runinga yangu naangalia hili shindano lililopewa jina la Dume challenge....washiriki wanapimwa kuanzia michezo hadi uelewa wa mambo ya kawaida kabisa ambayo kwa washiriki wale wanaonekana ni wakubwa kiumri kiasi fulani nilitegemea mtu hatoshindwa kujibu maswali. Paliponiacha hoi mtu ameulizwa swali ataje mikoa 5 ya Tanzania inayoanza na herufi "M" mtu anashindwa aliyefunga kazi ni yule jamaa anaitwa Mgune eti anataja mkoa wa Musoma wakati huo huo anataja mkoa wa Mara.....ndio yale yale ya Mheshimiwa, Pemba na Zimbabwe tunapata Tanzania?
 
Lakini hiyo ni kawaida yetu sisi watanzania, mara nyingi vitu vingi tunavijua lakini tupo slow sana kwenye kufukiri, tofauti na wenzetu wa Kenya na Uganda
 
Back
Top Bottom