Hivi hawa mafundi wapo?

Ivi "KINYOZI" cku izi bado zipo?? naonaga "BARBERSHOP" tu.

Kweli hawapo tena..kuna mmoja alikua anakaa chini ya mwembe fulani karibia na nyumbani simuoni tena. Kaninyoa tokea nikiwa mtoto mdogo halafu hazeeki huyo babu.
 
Hiyo mashine haiitwi SINGER kweli? Maana enzi hizo mashine hizo ndo zilikua kiboko, ukimkuta nayo mtu barazani ujue anapiga nayo kazi na anaingiza pesa balaa.

Umenikumbusha mbali sana nakumbuka marehemu babu yangu (R.I.P mzee Karia) alikuwa nayo na mpaka leo ipo zaidi ya miaka 25 tangu atangulie bado inagonga mzigo! Sio mchina wa leo akimaliza miaka miwili una bahati.
 
Nanoaaaaaa, nanoaaaaa! Kuna mzee alikua akipita na kuimba wimbo huo! Alikuwa ananoa vibao vya mbuzi! Angeimba leo watu wangemfuatilia wakija anauza Noah kwa bei poa!
 
Back
Top Bottom