Hivi hawa CCM wanaongoza serikali ya mbuzi au?

Bigirita

Platinum Member
Feb 12, 2007
15,986
7,366
Kauli ya CCM Kuhusu Kuanzishwa kwa Chama Kipya cha Upinzani – CCJ

Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vinaandika sana habari za kuanzishwa kwa Chama kipya cha upinzani kiitwacho Chama cha Jamii (CCJ). Habari kuhusu ujio wa chama hiki zimekuwa zinapambwa na vibwagizo vingi kwamba kimenzishwa na vigogo wa CCM kwa lengo la kukisambaratisha Chama cha Mapinduzi. Baadhi ya vyombo vya habari na hasa makala katika magazeti yamekuwa yanatabiri na kutarajia kumeguka kwa CCM kutokana na kuanzishwa kwa CCJ.

Chama cha Mapinduzi kinapenda kuwaarifu WanaCCM na Watanzania kwa jumla kwamba.

Kwanza, Chama cha Mapinduzi ndicho kiliruhusu uanzishwe mfumo wa vyama vingi 1992; hii ilikuwa baada ya Watanzania 80% kutoa maoni kwamba mfumo wa chama kimoja (yaani CCM) uendelee, na 20% walitaka uanzishwe mfumo wa vyama vingi. CCM ilikuwa na sababu nzuri ya kuwasikiliza waliowengi (80%), yaani wengi wape!

Lakini kwa kutumia busara kubwa CCM ilitoa fursa ya Watanzania 20% waanzishe vyama vyao vya upinzani na wamekuwa wanavianzisha, hadi sasa vipo 17

source: CCM website

My take:
Hawa jamaa wananiudhi mbaya kabisa!!!!! kuna sababu ya kutenganisha kati ya serikali na CCM. wamejibu kwa kiburi na jeuri isiyo na mfano. wanajua watz hawawezi kufanya lolote, au rather, 80% ya watanzania hawatasoma hii na hata wakisoma au kusikia hawataona tatizo, kwani hawajui kama CCM ni mpangaji serikalini, na sio mmiliki wa serikali, Mwaka huu anatakiwa kulipa pango, akishindwa anaingia mpangaji mwingine.

wanazidi kuniudhi hawa...ggggrrrrrrrrrrrr!
 
si tulishaambiwa na mkuu wa kaya kuwa wengi wetu tunafuata upepo tu
 
Unajua hakuna tofauti na kutawaliwa!
Hata ANC wakati ule, mandela aligundua method ya resistance
Waliyokuwa wanatumia ya wafanyakazi kugoma Haiwezi kufanya kazi, wakaamua kuwasha moto wa ukweli
Sasa ss mambo ya kitaifa hatugomi, tunagoma ili tuta lijengwe barabaani baada ya mtu kugongwa na gari!
Kagoda aka ra akichukua mabilioni yetu wala hatufanyi kitu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom