Hivi hatuwezi kupanga mikakati humu badala ya kulalamika tu?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,671
Kuna mengi ya kuchukiza huwa yanajitokeza na kuripotiwa hapa JF
na wazalendo mbalimbali. Hivi hatuwezi kuzigeuza nafsi zetu tukawa
wapigania uhuru wa kweli badala ya kuishi kama vivuli zaidi?

Ninachokusudia hapa ni baada ya thread kuletwa hapa jukwaani
na ikathibitika kuwa kuna ukweli basi tuanze mkakati wa pamoja
wa kupambana na tukio hilo, hivi hiki ni kizazi gani? Hatukumbuki wakati
wa Tanu jinsi wenzetu walivyofanya mikutano ya siri hadi kufanikisha
malengo yao?

Mfano. Traffic kaonea mtu huko ubungo kama ilivyoripotiwa, Basi hata
kwa kuchapishwa Ujumbe wa pamoja ambao kila mwana JF atakubaliana nao
na kama una mapungufu tunashauriana halafu ujumbe huo kila mmoja
mwenye fursa anaprint kisha unabandikwa mitaani (Kila mmoja kule anakoishi)
ili hata wale wasiopita hapa JF wauone................. Usiogope kukamatwakwani
hayo yaliwakuta wapigania uhuru wengi na ndo ushujaa tunauzungumzia.
 
Mkuu hata mimi nilikua nawazo kama lako, haiwezekani kila siku tunaishia katika mtandao tu! Tena nilifikiria mbali zaidi, kwanini tusitafute mahali hapo ndo tukawa tunajadiliana mada face 2 face ev'weekend? Inawezekana tukapiga hatua! Nawasilisha!
 
Mi naona tutaweza kama tukianzisha kama get together events.
 
Hilo linawezeka kabisa,
Ila tu, mpaka baadhi ya watu wakila BAN
 
Back
Top Bottom